Wanandoa wa Urusi walivyotoa habari za ujasusi kwa Ukraine

g
Maelezo ya picha, Sergei na Tatyana Voronkov walikuwa wamekatishwa tamaa kwa muda mrefu na maisha ya Urusi ya walipoamua kuhamia Ukraine.
Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 7

Wakati Sergei na Tatyana Voronkov walipohama kutoka Urusi kwenda kijiji kidogo cha Ukraine, walitarajia kuishi maisha ya utulivu, lakini mambo yaligeuka na kuwa tofauti sana na matarajio yao.

Baada ya uvamizi mkubwa wa Moscow, wenzi hao walijikuta katika eneo linalokaliwa na waliamua kuwa watoa habari za ujasu kwa jeshi la Ukraine.

Kilichofuata ni kuwekwa kizuizini, kuhojiwa, na kutoroka kwenda Ulaya kwa kutumia hati za uongo - na pete ya mpira.

Ilikuwa muda mfupi baada ya Moscow kuinyakua Crimea mnamo 2014 ambapo Sergei na Tatyana Voronkov walipoamua kuondoka Urusi.

Wanandoa hao walikuwa wamekatishwa tamaa kwa muda mrefu na mwelekeo wa nchi yao chini ya utawala wa Rais Vladimir Putin, lakini kunyakuliwa kinyume cha sheria kwa Crimea na kuzuka kwa mapigano mashariki mwa Ukraine kulionekana kuwa hatua ya mabadiliko.

"Tulikuwa tukienda kwenye maandamano [ya kupinga vita], lakini tuligundua haraka kuwa hayakuwa na maana," anasema Sergei, ambaye sasa ana umri wa miaka 55.

"Nilikuwa nikiwaambia marafiki zangu kwamba ni jambo baya kwamba tulikuwa tumechukua Crimea na tulikuwa tukijihusisha na Donbas [eneo kubwa la viwanda mashariki mwa Ukraine]... Walikuwa wakiniambia kwamba ikiwa hatukupenda, tunaweza kuondoka. Kwa hivyo tuliamua kuondoka."

Tatyana, mwenye umri wa miaka 52, ambaye alizaliwa Donbas lakini ni raia wa Urusi kama mumewe, alisema wafanyakazi wenzake ofisini hawakupenda maoni yake dhidi ya Kremlin na aliishia kuacha kazi yake muda mfupi baada ya kunyakuliwa kwa Crimea.

g

Chanzo cha picha, Family Archive

Maelezo ya picha, Sergei na Tatyana huko Moscow kabla ya kuhamia Ukraine

Kwa miaka mitano iliyofuata, wenzi hao walisafiri kwenda Ukraine kila baada ya miezi sita kutafuta nyumba mpya.

Mnamo mwaka wa 2019, walikaa Novolyubymivka, kijiji cha watu wapatao 300 katika mkoa wa Zaporizhzhia kusini mashariki mwa nchi, ambapo walifuga ng'ombe. Sergei pia alipata kazi kama mpimaji ardhi katzi ambayo alikuwa anaifanya wakati wa utumishi wake katika jeshi la Muungano wa Usovieti.

Mnamo Februari 24, 2022, roketi za kwanza za Urusi ziliruka juu ya nyumba yao.

"Asubuhi nilisikia sauti ya filimbi, kitu kikiruka, na nikatoka nje," Tatyana anakumbuka.

"Roketi ilikuwa ikiruka juu ya nyumba. Nilienda mtandaoni kuona kilichotokea na nikapata kwamba kyiv tayari ilikuwa imepigwa mabomu."

g

Chanzo cha picha, FAMILY ARCHIVES

Maelezo ya picha, Sergei na Tatyana huko Ukraine kabla ya uvamizi. Hawana picha za maisha yao ya kabla ya vita, baada ya kufuta data zote kutoka kwa simu zao na akaunti za mitandao ya kijamii.
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Mnamo Februari 26, kijiji cha Novolyubymivka, kilichopo karibu kusini mwa mkoa wa Zaporizhzhia, kilikuwa chini ya uvamizi wa Urusi, ingawa mwanzoni wanandoa hao hawakuwa na mawasiliano ya moja kwa moja na vikosi vya uvamizi.

Lakini siku chache baadaye, wakati msafara wa jeshi la Urusi ulipopita karibu na nyumba yao, Tatyana aliamua kuchukua hatua.

Alipoona msafara huo ukipita, Tatyana alikimbilia ndani, akachukua simu yake, na kumwandikia mtu anayemfahamu huko Kyiv, ambaye aliamini alikuwa na mawasiliano katika huduma za usalama za Ukraine.

Rafiki huyu aliwatumia kifaa cha mawasiliano cha chatbot maalum kwenye programu ya ujumbe wa Telegram. Chatbot iliwafahamisha kuwa watawasiliana na mtu aliye na kitambulisho cha kipekee.

Wanandoa hao waliombwa kutoa eneo na maelezo ya mifumo ya vita vya elektroniki na vifaa vya kijeshi walivyoona, hasa mifumo ya makombora na mizinga. Habari hii ilisaidia jeshi la Ukraine kulenga na kuwaangamiza wanajeshi wa Urusi katika mkoa huo kwa kutumia ndege zisizo na rubani na silaha.

"Hatukufikiria ni usaliti," Tatyana anasema, ingawa wote ni raia wa Urusi.

"Itakuwa uhaini ikiwa Urusi ingeshambuliwa na tunafanya kazi na adui. Lakini hakuna mtu aliyeishambulia Urusi. Hii ilikuwa vita dhidi ya uovu."

Wanandoa hao wanasisitiza kuwa habari waliyoitoa kwa jeshi la Ukraine haikusababisha mashambulizi dhidi ya raia au miundombinu ya raia.

h

Chanzo cha picha, Anadolu Agency via Getty Images

Maelezo ya picha, Msafara wa kijeshi wa Urusi ukielekea eneo la Donbas mnamo Februari 2022.

Kwa miezi miwili, Sergei alikusanya na kuratibu taarifa za ujasusi na Tatyana alizisambaza kutoka kwa simu yake, na kufuta athari zote za ujumbe baadaye.

Wanandoa hao waliendelea kuwasiliana na rafiki yao kwa barua huko Kyiv hadi mwisho wa Aprili 2022, wakati Novolyubymivka ilipoteza mtandao wake.

Wakati huo, watu wenye silaha walikuwa wakija kila wakati kijijini, wakiingia na kutafuta mali. Waliivamia Voronkovs mara kadhaa.

Walipoulizwa kwa nini hawakuondoka katika eneo lililokaliwa, wanandoa hao walijibu: "Tungeenda wapi?"

Hawakutaka kurudi Urusi na hawangeruhusiwa kuingia Ukraine isiyokaliwa na hati zao za Urusi. Zaidi ya yote, "walihisi nyumbani" mahali walipokuwa na walitaka kuendelea kusaidia Kyiv katika juhudi za vita.

Yote yalimalizika kwa kukamatwa kwa Sergei.

Kuhojiwa katika chumba cha chini ya jengo chenye baridi

g

Chanzo cha picha, Family Archives

Maelezo ya picha, Sergei na wanyama wake wa nyumbani kwake huko Novolyubymivka

Kama raia wa Urusi, wanandoa hao waliwavutia walishukiwa na mawakala wa usalama wa Urusi tangu mwanzo wa kazi.

Lakini ilikuwa mwishoni mwa Aprili mwaka jana ambapo Sergei alikamatwa na watu wenye silaha katika kituo cha mkoa wa Tokmak.

Mnamo Mei 26, watu ambao walijitambulisha kwa Sergei kama mawakala wa FSB walimrekodi akikiri kwenye video.

Siku mbili baadaye, kwa mshangao wa Sergei, aliachiliwa bila kutarajia - ingawa karibu hati zake zote zilihifadhiwa na watekaji wake, isipokuwa leseni yake ya udereva.

Hata leo, Sergei na Tatyana hawaelewi ni kwanini aliachiliwa baada ya kukiri kwake.

Sergei alikwenda kwa ofisi ya pasipoti ya Tokmak na kuomba hati mbadala, lakini mamlaka ya uvamizi wa Urusi haikuwa na haraka ya kumpa pasipoti mpya.

Sergei anasema wanaume hao, ambao hawakuwa wamevaa sare za kijeshi, walimpeleka kwenye nyumba na kumuweka kwenye chumba cha chini chenye baridi - karibu mita mbili kwa upana na kina cha mita tatu - ambapo alilala akichuchumaa.

Anaelezea jinsi siku iliyofuata alivyohojiwa na begi juu ya kichwa chake na kutishiwa kwa vurugu, na maafisa wakimuuliza ikiwa alikuwa amepitisha habari za kijasusi za Urusi kwa Waukraine.

Baada ya kukataa kuhusika kwake, siku ya nne uhusika wake, akiogopa kwamba ikiwa angefanyiwa vurugu, angeweza kuwahusisha wengine kwa bahati mbaya.

Wakati huo huo, Tatyana anasema alisafiri eneo hilo katika kumtafuta mumewe, akipiga simu kwenye hospitali na vyumba vya kuhifadhia maiti.

Mtoto wa wanandoa hao, ambaye bado anaishi nje ya Moscow, alianza kuwasiliana na mamlaka ya Moscow, kuanzia Kamati ya Upelelezi ya Jimbo hadi ya rais.

Siku ya kumi baada ya kukamatwa kwa Sergei, vikosi vya usalama vilikwenda nyumbani kwa Tatyana huko Novolyubymivka kufanya upekuzi. Waligundua $4,400 kwenye bustani—akiba ambayo wanandoa hao walikuwa wameificha.

Tarehe 7 Me, siku 39 baada ya kukamatwa kwa Sergei ndipo Tatyana alipokea habari juu ya mahali alipo mumewe. Huko Tokmak, polisi waliniambia: " FSB [huduma za usalama za Urusi] zimemteka nyara kwa Ujasusi."

g

Chanzo cha picha, family Archive

Maelezo ya picha, Sergei na wanyama wake wa nyumbani kwake huko Novolyubymivka

Kutoroka kwa kutumia kofia iliyotengenezwa kwa taili

Walipoondoka Novolyubymivka, akina Voronkov waliamua kubuni hadithi ikiwa wangekamatwa na vikosi vya Urusi na hata kutumia vifaa kuifanya iwe ya kushawishi zaidi.

Wanandoa hao walipakia gari lao na vifaa vya ufukweni—ikiwa ni pamoja na kofia ya majani yenye ukingo mpana na kofia iliyotengenezwa kwa taili—na walipanga kusema walikuwa wakienda kando ya bahari ili Tatyana, ambaye anaugua pumu, apate hewa safi.

Wanandoa hao hapo awali walikataliwa kuingia Urusi, lakini mwishowe waliweza kurudi baada ya Sergei kupata cheti kinachothibitisha kuwa alikuwa ameomba pasipoti mpya.

Baada ya kucheleweshwa zaidi kupata pasipoti yake na jaribio lililozuiliwa la kuondoka Urusi kupitia Belarus, Sergei alinunua pasipoti bandia kwa jina lake kupitia Telegram.

Wanandoa hao waliweza kusafiri kwa basi hadi Belarus na kuvuka mpaka kwa kutumia pasipoti bandia ya Sergei. Kutoka hapo, walivuka hadi nchi ya Lithuania, ambayo ni mwanachama wa Umoja wa Ulaya na mshirika wa karibu wa Ukraine.

Mgawanyiko wa familia

Lakini walinzi wa mpaka wa Kilithuania waligundua kuwa hati za Sergei zilikuwa za kughushi na kumweka katika kituo cha kizuizi kabla ya kesi.

Sergei hakuuona uzoefu huo kuwa mbaya.

"Baada ya kila kitu ambacho nimepitia, nilihisi kama nilikuwa katika nyumba ya wageni, nyumba ambayo huwezi kuondoka," alisema. "Tunaoga mara mbili kwa wiki. Shuka za vitanda zilibadilishwa mara kwa mara, na tulipewa chakula kizuri."

j

Chanzo cha picha, Family Archive

Maelezo ya picha, Sergei alifanikiwa kuingia Lithuania mwanachama wa EU kwa kutumia pasipoti bandia, lakini baadaye alifuatwa na mamlaka ya Lithuania.

Mahakama ya Lithuania ilimpata Sergei na hatia ya kutumia pasipoti bandia na kumhukumu kifungo cha siku 26, ambazo tayari alikuwa ametumikia kizuizini kabla ya kesi.

Wanandoa hao sasa wanatarajia kupewa hifadhi nchini Lithuania. Wanaishi katika kituo cha mapokezi cha wanaotafuta hifadhi.

Jeshi la Ukraine lilituma barua ya shukrani kwa Voronkovs, kwa ombi la kamanda wao wa zamani huko Kyiv, kuunga mkono ombi lao la hifadhi. BBC imeona nakala ya barua hii.

Mama ya Sergei mwenye umri wa miaka 87 bado anaishi Urusi. Ana maoni tofauti na mtoto wake, na mwanzoni mwa uvamizi, walibishana na kuacha kuzungumza kwa muda. Mtoto wa Voronkovs, ambaye pia anaishi Urusi, aliacha kuwasiliana na wazazi wake baada ya kujua walichofanya.

Licha ya uhusiano huu wa kifamilia, wenzi hao wana hakika kwamba hawatarudi Urusi.

"Ikiwa tu ataanza kuonyesha ubinadamu kidogo," anasema Sergei. "Hivi sasa, sioni chochote cha kibinadamu hapo.

Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi