Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 01.04.2024

Joao Neves na Antonio Silva wakishangilia bao la Benfica

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Joao Neves na Antonio Silva wakishangilia bao la Benfica
Iliyochapishwa

Liverpool wameungana na Manchester United na Chelsea katika mbio za kumsajili kiungo wa kati wa Benfica na Ureno Joao Neves, 19, ambaye ana kipengele cha kutolewa cha euro 120m (£102.6m). (O Jogo, via Sport Witness)

Manchester United na Manchester City wanavutiwa na beki wa Bayer Leverkusen Mholanzi Jeremie Frimpong, 23. (Sun)

Manchester City wanatazamia kufufua upya azma yao ya kumnunua kiungo wa kati wa West Ham na Brazil Lucas Paqueta mwenye umri wa miaka 26 msimu huu. (Football Insider)

Lucas Paqueta

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Lucas Paqueta alifunga mabao matano na kusaidia mengine saba katika mechi 41 alizochezea West Ham msimu uliopita

Leeds United wanapania kumsajili tena kiungo wa kati wa Uingereza Kalvin Phillips, 28, kwa takriban pauni milioni 30 kutoka Manchester City msimu huu ikiwa the Whites watapata nafasi ya kurejea katika Ligi Kuu ya Uingereza. (Sun)

Newcastle itaongeza juhudi za kumsajili mchezaji wa safu ya ulinzi msimu huu na kumpa mlinzi Mwingereza Paul Dummett, 32, mkataba mpya baada ya nahodha Jamaal Lascelles kuondolewa kwa hadi miezi tisa kutokana na jeraha la goti. (Newcastle Chronicle)

Kocha wa zamani wa Sheffield United, Paul Heckingbottom anaongoza orodha ya wagombea wanaotarajiwa kuwa meneja wao wa kudumu wa Sunderland. (Sun)

Phillips

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Phillips alicheza dakika 380 pekee za soka la Premier League akiwa na Manchester City kabla ya kujiunga na West Ham kwa mkopo

Barcelona wako tayari kupokea ofa ya kumuuza Raphinha msimu huu wa joto ili kupunguza wasiwasi wa kifedha, lakini mshambuliaji huyo wa Brazil mwenye umri wa miaka 27 hataki kuondoka. (Sport - kwa Kihispania)

Tottenham wanapanga kumtoa kwa mkopo Alejo Veliz, 20, kwa klabu tofauti msimu ujao kwani wanahisi mshambuliaji huyo wa Argentina wa Chini ya miaka 20 hajacheza mechi za kutosha katika kipindi chake cha sasa akiwa na Sevilla. (Fabrizio Romano)

Meneja wa Sporting Lisbon Ruben Amorim angependelea kujiunga na Liverpool iwapo atapewa kazi hiyo, lakini atafanya uamuzi kuhusu mustakabali wake mwishoni mwa msimu huu. (Correio da Manha - kwa Kireno)

Raphinha

Chanzo cha picha, Getty Images

Tottenham wamejiunga na mbio za kumsajili kiungo wa kati wa Leeds United, 18, Archie Gray, huku Liverpool pia ikimnyatia mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza chini ya miaka 21. (Football Insider)

Imetafsiriwa na Ambia Hirsi