Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Je kuna faida na madhara kiasi gani unapotumia vidonge vya vitamini bila ushauri wa daktari?
Kutumia virutubisho vya lishe ili kukidhi upungufu wa virutubishi mwilini sio jambo geni, lakini je unafahamu faida na madhara yake?
Virutubisho hivi au vitamini vinaweza kupatikana madukani katika aina nyingi tofauti – dawa za maji, tembe, vinywaji au hata vya poda - ambazo zinaweza kupunguza upungufu wa virutubishi mwilini mwako kama vile vitamini, madini, kalsiamu, chuma na protini.
Hata hivyo, madaktari wanasema kwamba virutubisho hivi haviwezi kuwa sawa na lishe bora. Wanasema kuwa hali ya kutumia virutubisho hivyo imeongezeka kwa wanawake wenye umri wa zaidi ya miaka 30.
Dkt Sunila Garg aliimbia BBC kuwa, "virutubishi hivi au Multivitamins pia ni muhimu kwa walaji mboga, lakini 'kiwango kimoja hakiwezi kuwa sawa kwa watu mbali mbali’’ hivyo wagonjwa watumiaji wanapaswa kuchukua virutubisho kwa ushauri wa daktari badala ya wao wenyewe."
Dkt Raj Aron aliiambia BBC kwamba katika kazi yake hukutana na wanawake wagonjwa wenye umri wa miaka 30 hadi 40 ambao huanza kutumia multivitamini peke yao. Hata hivyo, hii haipaswi kufanyika kwa sababu pia ina madhara.
Akielezea kuhusu sula hilo, Dkt Seema Gulati wa Taasisi ya Kitaifa ya Kisukari, Unene na Cholesterol nchini India (NDOC) alisema, “Imezoeleka mijini kuwa watu hujitibu au kwenda kwenye maduka ya dawa kwa kuelewa ugonjwa wao wenyewe.” . Iwe dawa ya maumivu au vitamini, jambo ambalo wakati mwingine haliwaponyi."
Kulingana naye, "Matumizi ya dawa kwa kupata taarifa kutoka Google, au taarifa kutoka kwenye mitandao ya kijamii yanaongezeka. Dawa nyingi zinapatikana bila hata idhini ya madaktari jambo ambalo lina madhara’’
Madhara ya Virutubisho (multivitamins) kwenye mwili
Madaktari hawa wote wanasema kwamba kirutubisho anachopendekeza daktari na kiasi anachopendekeza daktari kinapaswa kutumiwa kwa vile hakuna faida ya kutumia virutubisho kupita kiasi kilichoagizwa na daktari.
Wakati huo huo, madaktari wanasema kwamba matumizi virutubisho hivi kupita kiasi yanaweza pia kuacha athari kwenye mwili.
Vitamini- Dkt Seema Gulati anaeleza kuwa kuna vitamini nyingi zinazoyeyushwa na mafuta, kama vile vitamini E na Omega 3.
Kutumia vitamini hizi bila ushauri wa daktari, kunaweza kusababisha kurundikwa kwake mwilini. Hii inaweza kuwa na athari mbaya kwa mwili.
Kiwango kikubwa cha Vitamin A na Vitamin E- kunaweza kusababisha matatizo kama vile kutapika, kushindwa kuona vyema n.k.
Wakati, vitamini E inaweza kupunguza shinikizo la damu, lakini pia inaweza pia kuathiri mapafu, anasema Dkt. Seema Gulati ambaye ni mkuu wa kituo kinachofanya kazi ya utafiti kuhusu lishe na utendaji wa mwili. Anashauri zitumike kwa kadri ya muda ulivyoshauriwa na daktari.
Kulingana naye, vitamini nyingi huyeyuka mwilini na zikiingia mwilini kwa wingi, pia hutolewa kupitia kinyesi.
Vitamin B- Vitamini hii husaidia katika kutengeneza chembechembe nyekundu za damu mwilini. Pia hufanya kazi ya kuimarisha ubongo na seli za neva. Kutokana na upungufu wake mwilini mtu anaweza kuwa na athari zifuatazo:
Ngozi huanza kugeuka njano.
Kuhusi Udhaifu .
Kupungua kwa gesi, kuvimbiwa na kupoteza hamu ya kula .
Tatizo la mapigo ya moyo na ugumu wa kupumua .
Vitamini hizi zinapatikana katika aina mbili, ambazo kipimo chake ni kidogo. Wakati huo huo, vitamini vhizi pia hupewa wagonjwa wa kisukari, lakini iwapo watatumia virutubisho hivi kwa muda mrefu bila sababu yoyote, basi inaweza kuwa na madhara.
Vitamin D - Dkt. Raj Aron anaeleza kuwa upungufu wake unaonekana kuanzia kwa watoto hadi vijana. Sababu kuu ya hilii ni kufanya shughuli nyingi za ndani.
Jua linachukuliwa kuwa chanzo asili cha Vitamini D, lakini sasa watu hawawezi kutoka. Ikiwa mionzi ya jua itafikia mwili wakati wa shughuli za kimwili, basi vitamini D hiyo pia husaidia katika kunyonya kalsiamu katika mwili.
Wanapendekeza kwamba tunapaswa kutumia Vitamini D kwa miezi mitatu tu, lakini watu huongeza muda huu. Katika hali hiyo, unaweza kuwa na matatizo ya ugumu wa kupumua, matatizo ya uzagwaji wa chakula mwilini, uchovu, kizunguzungu, kuchanganyikiwa, kukojoa mara kwa mara, shinikizo la damu na madhara mengineyo.
Dkt Seema Gulati anasema licha ya kwamba watu wanakuwa makini kwa afya zao na pia wanajitahidi kufuata mpangilio wa chakula miili yao inachokihitaji (kufanya diet), Kutokana na hili uwiano wa chakula kinachohitajika huharibika na vitamini pia hupotea kutoka kwa chakula.
Madaktari wanasema kuwa lishe bora haipaswi kulinganishwa na virutubisho, kwani lishe bora husaidia kupunguza mapungufu yote ya virutubisho mwilini.
Ingawa wakati umri wa mwanamke unapoanza kuongezeka zaidi ya 30, virutubisho hivi husaidia, ni muhimu kuzingatia kuwa vinapaswa kutumiwa tu kwa ushauri wa daktari. Mbali na hayo, yeye pia anashauri yoga na mazoezi