Armenia-Azerbaijan:Takriban watu 100 wauawa katika mapigano ya usiku

Iliyochapishwa

Mapigano kati ya Armenia na Azerbaijan siku ya Jumatatu usiku yaliwauwa karibu wanajeshi 100, imeibuka.

Waziri Mkuu wa Armenia Nikol Pashinyan alisema wanajeshi wake 49 walikufa katika mapigano ya usiku, huku wizara ya ulinzi ya Azerbaijan ikisema wanajeshi wake 50 pia waliuawa.

Nchi hizo jirani zimepigana vita viwili na kushuhudia mapigano madogo ya mara kwa mara yakichukua miongo mitatu.

Siku ya Jumanne, Urusi ilisema ilipanga kusitisha mapigano baada ya machafuko  ya hivi karibuni.

Awali Armenia ilisema mapigano yametulia, badala ya kumalizika kabisa. Baadaye, Azerbaijan ilisema imekamilisha malengo yake kufuatia "uchokozi" kutoka kwa jirani yake.

Kiini cha mzozo huo ni mkoa wa Nagorno-Karabakh. Kulingana na mipaka inayotambulika kimataifa, ni sehemu ya Azabajani - lakini inakaliwa na Waarmenia .

Mgawanyiko wa kitamaduni unaenea zaidi ya siasa hadi dini, pia: Armenia ni nchi ya Wakristo wengi, wakati Azerbaijan ni Waislamu.

Nchi zote mbili zilikuwa sehemu ya Umoja wa Kisovieti kabla ya kuvunjwa kwake mwishoni mwa 1991.

Mzozo huo umesababisha vita kamili katika miaka ya 1980 na 1990, vita vya wiki sita mnamo 2020 na kuendelea kwa mapigano kwa miongo kadhaa.

Nchi hizo mbili zinalaumiana kwa kuzuka hivi karibuni kwa ghasia.

Armenia ilidai kuwa miji kadhaa kwenye mpaka ilishambuliwa kwa makombora na jirani yake na kwamba ilijibu uchokozi huo.

Azerbaijan ilisema miundombinu yake ilishambuliwa kwanza, huku msemaji wa jeshi Lt Kanali Anar Eyvazov akisema kuwa harakati za kijeshi katika mwezi uliopita "zinaonyesha kwamba Armenia inajiandaa kwa uchokozi mkubwa wa kijeshi".

Vurugu ziliendelea Jumatatu usiku kabla ya Moscow kusema ilikuwa imejadiliana usitishaji wa haraka wa mapigano kuanza mapema Jumanne asubuhi.

Nikol Pashinyan wa Armenia, hata hivyo, alisema "kiwango cha uhasama kimepungua, lakini mashambulizi ya pande moja au mbili kutoka Azerbaijan yanaendelea".

Baadaye siku ya Jumanne, Azerbaijan ilisema wanajeshi wake walikufa "kwa sababu ya uchochezi mkubwa wa Armenia" na iliishutumu Armenia kwa kukiuka makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyosimamiwa na Urusi.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alizungumza na Rais wa Azerbaijan Ilham Aliyev siku hiyo hiyo, akimtaka "kurejea kuheshimu usitishaji vita" na Armenia.

 

Mapigano hayo yamelaaniwa kimataifa. Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken alipiga simu za kibinafsi kwa viongozi wa mataifa yote mawili siku ya Jumanne, akiwataka wafikie suluhu la amani na kuzuia mapigano zaidi.

Bw Blinken alisema atasukuma "kusitishwa mara moja kwa mapigano na suluhu ya amani" kati ya nchi zote mbili.

Urusi iko karibu na Armenia, lakini ni ina nguvu kubwa katika eneo hilo na inadumisha uhusiano na pande zote mbili.

Msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov alisema kuwa Rais Vladimir Putin alikuwa "binafsi" akichukua jukumu la upatanishi.

"Rais kwa kawaida anafanya kila juhudi kusaidia kupunguza mvutano kwenye mpaka," alisema.

Uturuki, wakati huo huo, ina uhusiano na Azerbaijan na inaonekana kuunga mkono hatua zake za hivi punde. Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Mevlut Cavusoglu, alisema "Armenia inapaswa kusitisha uchokozi na kuzingatia mazungumzo ya amani".

Mapigano ya Jumatatu usiku yanaaminika kuwa mabaya zaidi tangu mzozo wa 2020, ambapo maelfu waliuawa. Vita hivyo vilimalizika kwa makubaliano yaliyosimamiwa na Urusi, ambayo yalishuhudia Armenia ikitoa wanajeshi wake katika maeneo yanayokaliwa na Nagorno-Karabakh.

Kikosi cha kulinda amani cha Urusi cha karibu watu  2,000 kilitumwa katika eneo hilo kama sehemu ya mazungumzo, ambapo bado  kipo huko hadi leo.