Je ni hatua gani zinazopaswa kuchukuliwa Man United baada ya kushindwa na Man City 3-0 ?

RE

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES

    • Author, Danny Murphy
    • Nafasi, BBC
  • Iliyochapishwa

Jambo baya kwa Manchester United ni kwamba Manchester City walikuwa na wakati mzuri huko Old Trafford, hawakujituma sana kuwafunga 3-0.

Walipoteza kwa sababu ya ubora wa hali ya juu wa wapinzani wao, hawakuweza kulinda lango lao wala kushindana nao kimwili. Hili si jambo geni kwa United - nilipowatazama hivi karibuni, nilihisi ni rahisi kuwafunga.

Walikuwa vizuri msimu uliopita - ikiwa ni pamoja na ushindi wao dhidi ya City huko Old Trafford mwezi Januari. Ni aina ya uchezaji nilioutarajia kutoka kwao msimu huu, lakini nilipoona safu ya United nilipata wasiwasi.

Niliwahi kusema kwamba wanapokuwa na wachezaji kama Christian Eriksen na Bruno Fernandes katika timu yao, licha ya kuwa wote ni wanasoka wenye vipaji, inamaanisha kwamba safu yao ya ulinzi haitokuwa nzuri.

Tumeona Arsenal na Newcastle wakiishinda City katika wiki chache zilizopita baada ya kuwaweza kimwili, lakini United hawakukaribia hilo - walihitaji nguvu zaidi na ukakamavu.

Nini kinafuata kwa United?

DF

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES

Kumekuwa na michezo msimu huu ambapo kocha Erik ten Hag amefanya mabadiliko wakati wa mapumziko, lakini kwa ujumla wachezaji wakongwe kama Fernandes, Eriksen au Casemiro hawatolewi mara kwa mara kwa kutocheza vizuri.

Hilo halitokei kwa City, au Liverpool ama Arsenal. Ikiwa wachezaji wao hawafanyi vizuri ipasavyo, mameneja wao huwatoa kwenye timu.

Ten Hag alisema kabla ya mchezo huo kuwa alifurahishwa na mpangilio mzuri wa ulinzi wa timu yake lakini nimeitazama United katika wiki chache zilizopita na siamini hilo.

Dhidi ya FC Copenhagen na Brentford, United haikupata matokeo ya kuridhisha.

Siku ya Jumapili, walicheza vizuri katika kipindi cha kwanza, na kuwalazimu City kufanya makosa, lakini unapaswa kudumisha hilo kwa dakika 90. Hawakuweza, na tuliona kilichotokea.

Iwapo anataka kucheza na kupata ushindi, basi Ten Hag hana budi kupata wachezaji bora zaidi uwanjani.

Man City walitengeneza nafasi

ED

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Ni kawaida kwa mchambuzi kuikosoa timu, na pia kuipongeza upande ambao inafanya vizuri, lakini ninahisi ni lazima nifanye yote mawili hapa.

Tunajua jinsi City walivyo wazuri, na jinsi wanavyokuchosha na harakati zao na uwezo wao wa kiufundi. Zaidi ya hayo, maamuzi yao ni mazuri wawapo uwanjani.

Dhidi ya United, walijua wakati kupiga pasi, kurudisha pasi, wakati wa kwenda golini na wakati wa kurudi na kuwakatisha tamaa wapinzani, hadi wakati muafaka wa kuwaumiza.

Inaonekana ni rahisi, lakini kuwa na kila mchezai kwenye timu anayefanya wajibu wake ni nadra sana, na ulikuwa mchezo wa kuvutia kutazama.

Hata hivyo, United iliwasaidia sana Man City na kuifanya iwe rahisi kwao kuliko ilivyopaswa kuwa.

Haikuwa kwamba City waliendelea kuifungua United kupitia ustadi wa ajabu, ingawa kulikuwa na mambo machache ya ustadi. Badala yake, matatizo mengi ya United - kutokufanya mambo ya msingi unayohitaji kuyafanya katika mchezo.

City walitengeneza nafasi na kushinda.