Chumba cha siri kilichookoa maisha ya binti huyu

Anne

Chanzo cha picha, Sotheby's

Iliyochapishwa

Kazi kuu ya mchoraji toka Urusi Wassily Kandinsky inaweza kuuzwa kwa bei itakayoweka rekodi katika mnada huko London katika wiki chache. Lakini nyuma ya mauzo kuna simulizi ya familia moja ya majonzi na ushujaa, yote yaliyowekwa katika muswada ambao haujachapishwa, anaandika Stephen Smith.

Simulizi hiyo ni ya msichana mdogo, mwenye umri wa miaka saba, kujificha kwenye chumba cha siri.

Mwanamke mmoja anamwambia, "Kaa kimya, nyamaza, usipige kelele (kuzugmza), hakuna mtu anayeweza kujua kuwa uko hapa, hakuna mtu! Unanisikia?" Mwanamke huyo alikuwa binti wa kazi (yaya) aliyekuwa anamlea binti huyo mdogo, ambaye alimtunza akiwa na mama yake na nyanya yake nyumbani kwao.

"Ukipiga kelele na mtu akasikia, tunaweza kuuawa wote na Wajerumani. Umenisikia sawa?" alimwambia binti huyo ambaye hakujua kwamba hataiona nyumba yao tena kwa miaka mingi na kwamba hatamwona tena mama yake au nyanya yake.

Hapajui mahali hapa alipo, palikuwa ni nyumbani kwa yaya, haijui wala familia ya yaya. Lakini hakujua angekaa hapa kwa miaka miwili na nusu ijayo, akiwa amefichwa kwenye chumba hiki kidogo, bila kuzungukwa na marafiki na wengine isipokuwa mdoli tembo wa kuchezea anayeitwa Jumbo, na yote kwa sababu ya kujificha kwa siri.

Msichana huyu mdogo aliitwa, Dolly, ni Myahudi. Ilikuwa mwaka 1943 huko Amsterdam iliyokuwa inakaliwa na Nazi.

Simulizi ya Dolly ina ulinganifu wa ajabu na historia maarufu ya wakati wa vita ya Anne Frank. Wakati Dolly amejificha Anne na yeye alikuwa amejificha katika nyumba nyingine iliyo umbali usiozidi maili mbili. Wasichana hao wawili hawajuani na hawajawahi kukutana.

Anne na familia yake walitekwa mnamo Agosti 1944 na kupelekwa Auschwitz. Mama na baba na nyanya ya Dolly pia waliuawa huko Auschwitz, lakini yeye alinusurika.

Dolly's mother and father Luise and Herbert

Chanzo cha picha, SOTHEBY'S

Maelezo ya picha, Mama na baba yake Dolly - Luise na Herbert

Simulizi ya Anne ya kuishi mafichoni, The Diary of a Young Girl, inakuwa mojawapo ya nyaraka muhimu zaidi za maangamizi ya watu. Simulizi ya Dolly kuhusu jinsi alivyonusurika kwenye vita hiyo imo katika kumbukumbu ambayo haijachapishwa lakini hadithi yake inahusishwa na kazi ya sanaa badala ya kitabu.

Ni kazi bora ya kisasa, kwa kweli, na iko katikati ya kampeni ya kuthibitisha madai ya familia ya Dolly kwa mkusanyiko wa sanaa ambayo walipoteza katika vita.

Mchoro huo utauzwa London katika muda wa wiki chache na unaweza kuingiza zaidi ya £35m ($42m), itakuwa rekodi ya dunia kwa msanii aliyeitengeneza. Wanasema kwamba kila picha ina simulizi yake na hii inaelezea simulizi ya familia ya Dolly, walikuwa nani na nini kiliwapata.

Stern Villa huko Potsdam

Chanzo cha picha, Sotheby's

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Johanna Stern na mumewe Siegbert walikuwa wamiliki wa biashara ya kuvutia ya nguo iliyokuwa maarufu kama Graumann na Stern, katika miaka ya 1920 Berlin.

Walikuwa na watoto wanne - Annie, Hilda, Hans na Luise - walioishi katika jumba la kifahari lililobuniwa na mbunifu huko Potsdam, nje kidogo ya Berlin. Walikuwa wanahudumu pia katika jumuiya ya Wayahudi, wakisaidia kuanzisha shirika la hisani la kuwasaidia Wayahudi wa Ulaya Mashariki wanaoishi katika umaskini.

Siegbert Stern alifariki kifo cha kawaida mwaka 1935, lakini kutokana na kuongezeka kwa vitisho vya Nazi, Johanna hatimaye alilazimika kuikimbia Ujerumani.

Johanna aliwasili Uholanzi kupitia Uswizi mwaka wa 1937 na aliweza, kwa msaada wa mwanawe Hans, kubeba baadhi ya samani zake na kazi zake za sanaa.

Mnamo 1941 Wanazi wa Ujerumani waliiteka Uholanzi na Johanna Stern alitangazwa kuwa hana utaifa. Alilazimika kujificha huko Bussum, karibu na Amsterdam, lakini alitekwa na kuuawa huko Auschwitz mnamo Mei 1944.

Mmoja wa binti wa Stern, Luise, na mume wake, ambao pia walikuwa wamejificha huko Amsterdam, pia walikamatwa kabla ya kuuawa. Lakini waliweza kumkabidhi binti yao mwenye umri wa miaka saba, Dolly, chini ya uangalizi wa yaya wao, anayeitwa Anna ambaye alifanikiwa kumficha mtoto huyo katika chumba huko Amsterdam kilichookoa maisha yake.

Uzoefu wa Dolly wa kujificha ulikuwa wa kuhuzunisha sana.

Alivyonusurika kuuawa

Dolly in later life

Chanzo cha picha, Sotheby's

Maelezo ya picha, Muonekano wa Dolly katika miaka ya mwisho wa uhai wake

Wanazi waliwalazimisha Wayahudi kama Dolly kuvaa alama ya nyota ya njano ili kuwatambua lakini Anna yule binti wa kazi ama yaya alikuwa ameichomoa hiyo alama kwenye koti la Dolly na kumwambia msichana huyo kuwa kuanzia sasa atamwita mama mdogo. Sehemu ya nyumba ya Anna ilitumika kama chumba cha ushauri wa daktari na kilikuwa kidogo na chenye kiambata kilichojificha.

Hii ikawa nyumba ya binti Dolly kwa miezi 30 iliyofuata.

Mara kadhaa wakija Wanazi Anna alimficha Dolly uvunguni au kumfungia kwenye kabati chini ya sinki. "Akifunikwa funikwa na mafagio na matambara ya deki na vifaa vingine vyenye vumbi.

"Wakati maofisa wa Ujerumani walipokuwa jikoni, Anna alionyesha ni watu wasio na hatia. Alifanya utani wa Kijerumani kuonyesha tu kwamba hakukua na myahudi ama mtu asiyetakiwa mule ndani, lakini mara tu walipoondoka alianguka na kutetemeka mwili mzima." Kwa hofu kwamba kama wangejua na yeye angeuawa.

Kwa msichana mdogo, moja ya mambo magumu zaidi ilikuwa kukaa kimya kabisa kwa muda mrefu bila kujigusa na kupiga kelele. Hatimaye washirika waliweza kuikomboa Amsterdam mwaka wa 1945 na Dolly alitoka mafichoni, msisimko na utulivu wake ulionyeshwa kwake kwa sauti za kila siku.

"Kama wengine wengi sikuwa na viatu. Tatizo hili lilitatuliwa na vitambaa vya mbao vilivyouzwa kila mahali. Soli ya mbao na kamba mbili juu. Nilipenda kupiga kelele. Niliruhusiwa kuwa pale na kila mtu alijua hilo. Niliruhusiwa kuishi tena, kuishi maisha ya kawaida."

Dolly aliishi hadi mwishoni mwa miaka ya 70, na alifurahia maisha yake, kama inavyoeleza kumbukumbu zake.