Maisha yanakuwaje kwa mwanamke mwenye "ugonjwa wa akili"?

.

Chanzo cha picha, Somsara Rielly/BBC

Iliyochapishwa

Victoria alijua kuhusu mke wa mpenzi wake, lakini baada ya miaka michache alishuku kuwa alikuwa na wapenzi wengine.

Hakukuwa na uthibitisho, lakini mienendo yake ilikuwa ikisema kila kitu, anasema.

Simulizi zake hazikuwa na mpangilio.

Uso wake ulionekana tofauti aliposema uwongo.

"Ninakuwa na kumbukumbu nzuri sana linapokuja suala la mazungumzo, " anasema.

Hakujua kudanganya hata kidogo. Sina hakika kwa nini mkewe hakuwahi kumshika."

Akilini mwake, kilichokuwa kinazunguka ni namna ya kumwadhibu hadi Victoria hadi alipopata ufumbuzi.

Ilimchukua muda kidogo, na kumlazimu kufanya kana kwamba hakujua kinachoendelea.

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Kwa muda wa miezi kadhaa, wakati bado anakutana naye kama rafiki yake wa kiume, Victoria alituma picha za uchi za mpenzi wake kwa mkewe.

Taarifa hizi alizipata kwa masikitiko makubwa na kuanza kujiuliza, ni nani anayeweza kufanya jambo kama hilo.

Mkewe alihuzunika sana.

Alikiri kwa Victoria kwamba alikuwa akilala na wanawake wengine.

Hakumshuku, naye akamfariji.

Na kisha, Victoria alipochoka na kuwa tayari kumaliza uhusiano huo, alimtumia mkewe picha nyingi tu, ya mwisho picha yake mwenyewe na mume wa mwanamke huyo.

Kwa ufunuo huo wa maisha yao, Victoria aliachana na maisha yao kabisa.

Victoria alipokuwa akiwaambia watu hadithi hii, uzembe wake ungewashtua watu.

"Watu waliniuliza, Kwa nini umfanyie hivi mke wake? Mkewe alikufanyia nini hadi kustahili hayo? Alikuumiza vipi?" anasema.

Na kufikiria, kweli hakuna haki maishani".

Akasita.

Nadhani huo ni mfano mzuri wa tabia iliyokithiri ya kisaikolojia niliyokuwa nayo.

Saikolojia sio utambuzi rasmi wa afya ya akili na haijaorodheshwa katika toleo la tano na la hivi punde la Mwongozo wa Uchunguzi na Takwimu wa Matatizo ya Akili.

Badala yake umejumuishwa chini ya neno pana la ugonjwa wa akili, ingawa nneno hilo ‘psychopathy’ hutumiwa sana katika mazingira ya kimatibabu ya kimataifa.

Inaeleweka kwa mapana kuwa ugonjwa wa neuropsychiatric (uhusiano kati ya ugonjwa wa akili na ugonjwa wa ubongo), ambapo mtu anakuwa hana huruma au majuto, mara nyingi husababisha tabia isiyo ya kiungwana na wakati mwingine ya uhalifu.

Neno hili lilitumiwa na madaktari wa Ulaya na Marekani mwanzoni mwa miaka ya 1900 na likawa maarufu kufikia 1941, kufuatia kuchapishwa kwa kitabu ‘The Mask of Sanity’ na daktari wa akili wa Marekani Hervey M Cleckley.

Wanasaikolojia na wataalamu wa magonjwa ya akili kwa ujumla wanakubali kwamba kati ya mtu mmoja na wawili katika kila watu 100 katika idadi ya jumla wanakidhi vigezo vya ugonjwa wa akili, lakini Abigail Marsh, mwanasaikolojia na mwanasayansi wa neva katika Chuo Kikuu cha Georgetown, huko Washington DC, anadai kwamba karibu 30% ya watu kwa ujumla wanaonyesha kiwango fulani cha sifa za matatizo ya kisaikolojia.

Kwa wale ambao wana tatizo la ‘psychopathy’, inaweza kumaanisha kuwa wanajitahidi kudumisha urafiki wa karibu na kujiweka katika hali hatari, lakini hali hiyo pia huathiri watu walio karibu nao.

"Kuwa karibu na mtu asiye na huruma au mtu mlaghai mara nyingi huwa mbaya kwa watu walio karibu nao, na huchosha watu wenye tatizo la psychopathy lililokithiri," anasema Marsh.

Anasema kwamba tafiti nyingi kuhusu watu wenye tatizo hilo zimefanywa kwa wahalifu.

Kwa ujumla, utafiti unaonyesha kwamba tatizo hilo ni la juu kati ya wahalifu wa kiume (labda 15-25% ya wafungwa wanaume) ikilinganishwa na wahalifu wa kike (ambapo hupatikana katika 10-12%).

Lakini bado ni nyanja ambayo bado kwa idadi ya watu wengi kwa ujumla, wakati utafiti mdogo unafanywa kwa wanawake.

.

Chanzo cha picha, Somsara Rielly/BBC

Maelezo ya picha, Wanawake walio na ugonjwa wa akili huwa na tabia ya chini ya unyanyasaji kuliko wanaume, lakini zaidi inakuwa ni kama udanganyifu kati ya watu.

Victoria anasema tabia yake ya ujanja ilianza kuonekana kama njia ya kujifurahisha.

Alizaliwa Malaysia.

Ulevi wa baba yake na ukosefu wa uwajibikaji wa kibinafsi kwa matokeo ya unywaji wake ulifanya nyumba yake kutokuwa na furaha.

Alifanikiwa sana shuleni lakini mara nyingi alichoshwa.

Kwa kujifurahisha angefurahia kusambaza taarifa za siri ambazo watu walimweleza, siri alizoapa kutunza.

Nani alimchukia nani.

Nani alikuwa na mapenzi na nani.

Mivutano kati ya watoto katika shule ya sekondari mara nyingi inaweza kupatikana nyuma yake.

Victoria alijua jinsi ya kuwadanganya wengine ili wawajibike kwa makosa aliyofanya, au nini cha kusema ili kujiondoa kwenye matatizo.

Alimsadikisha mwalimu kwamba alimrushia chaki kutokana na shinikizo la watu wa rika lake.

marika.

"Ni kile alichotaka kusikia,"anasema.

 Alitaka kuamini kwamba mtoto mwerevu hakuwa mtoto mbaya, ni mtoto anayeongozwa kwa urahisi.

"Hivi majuzi Victoria amekuwa akipata usaidizi wa kudhibiti hisia zake.

Lakini pia amekuwa akipata usaidizi, labda la kushangaza, kutoka kwa wengine kama yeye.

Victoria anarejelea jumuiya ya mtandaoni ya wanawake kama yeye.

Inaangazia zaidi blogu ya mwandishi ME Thomas, labda mmoja wa wanawake wanaojulikana sana walio na ugonjwa wa akili.

Thomas alipata zaidi ya 99% alipopimwa saikolojia na John Edens, mwanasaikolojia wa uchunguzi katika Chuo Kikuu cha Texas.

Mfano wa hili tatizo ni kama vile kumwambia mtu anampenda wakati anataka kitu kutoka kwao, anasema Thomas.

Ni jambo ambalo amefanya mara chache, anasema, na limesababisha kuvunjika kwa mahusiano kadhaa.

Utafiti mmoja wa 2012 katika Chuo Kikuu cha Zurich pia uligundua kuwa kicheko hutumiwa mara nyingi na watu wenye tatizo hili kama kifaa cha kudanganya kwa makusudi, kuwasaidia kudhibiti mazungumzo, kwa mfano.

Au nyakati fulani walimcheka, si pamoja na mtu waliyekuwa wakizungumza naye.

Thomas anasema wakala wake anamwambia asitumie neno ‘mdanganyifu’ wakati wa kujizungumzia, lakini badala yake anasema kwamba alijua jinsi ya kushawishi watu tangu utoto wake.

Lakini ujanja ni neno analotumia.

Alisema ubora huo ulimsaidia kuwa mwanasheria mzuri, ambayo bado ni taaluma yake.

Anapozungumza, watu hawawezi kuweka lafudhi yake.

Wanafikiri anaweza kuwa anatoka Israel au Ulaya Mashariki, ingawa ameishi maisha yake yote huko California.

"Unapata lafudhi kutokana na kuunganishwa hadi kuwa na utambulisho. Sijawahi kupata utambulisho," anasema.

"Nina hisia dhaifu ya ubinafsi."

Kwenye blogi yake, anashirikisha mawazo yake ya kila siku na kuwahoji watu wengine wanaoishi na tabia za kisaikolojia.

Wasomaji wake wengi hupata kimbilio katika machapisho na video zake, anasema, kwani ni mahali ambapo wanatambua mifumo yao wenyewe na kushiriki uzoefu bila mtu kuwahukumu.

.

Chanzo cha picha, Somsara Rielly/BBC

Maelezo ya picha, Jenetiki na mazingira ambayo mtu anakulia hufikiriwa kuwa na sehemu katika tatizo hili la akili

Msomaji mwingine ni Alice, mwanamke Mjerumani mwenye umri wa miaka 27.

Alice anasema kwamba inafadhaisha kusoma makala au kutazama watu walio na ugonjwa wa akili kama watu waovu ambao lazima wote waepukwe.

"Tupo kama kila mwingine yeyote yule."

Kama Thomas, Alice anaanza kupendwa mara moja, labda kwa sababu anatabasamu sana.

Anakiri mapema kwamba anaiga kile anachojua kinafaa kijamii.

Alice amefanya hivi maisha yake yote.

Bibi yake alipokufa, aliona huzuni ya dada yake na kuakisi tabia yake.

Anasema pia anajifanya mbishi kwani inamruhusu kujiepusha na mengi na kusema yaliyo moyoni mwake bila kusababisha hofu.

Alijifunza haya mapema akiwa na umri wa miaka 12 akiwa likizoni kwenye meli na alijiuliza kwa sauti ingekuwaje ikiwa wangepata ajali na kutazama watu wakizama.

Mwitikio kutoka kwa wazazi wake na marafiki wao ulimfundisha kwamba ilikuwa muhimu kuitunga kama mzaha usiofaa, badala ya mawazo yasiyofaa.

Ingawa Thomas anaelezea tabia yake kuu ya kisaikolojia kama udanganyifu na Victoria anasema hana huruma, Alice anaashiria ukosefu wake wa huruma kama tabia yake inayoonekana zaidi.

"Sina huruma yoyote ya kihisia, lakini nina huruma nyingi za utambuzi, " asema, tabasamu lake bado liko mahali.

"Kwa hivyo ikiwa mtu ataumia, kama kuumiza goti lake au kuvunjika mkono, naweza nisihisi chochote kwa ajili yake kihisia lakini najua anatakiwa kupata msaada hivyo nitafanya."

Lakini hii, anasema, inamfanya kuwa mtu mzuri wa kuwa karibu naye katika dharura.

“Watu wananiambia matatizo yao na mimi sijapata kihisia juu yao, na ninaweza kuwasikiliza, kuwapa ushauri wenye mantiki,” anasema.

"Watu wengine wanaweza kutaka kujitenga kwa sababu husababisha hisia zao wenyewe, lakini hiyo haifanyiki kwangu".

Alice sio peke yake anayefikiria kwamba tabia zake zinaweza kuwa faida kwa jamii.

"Kila mtu anamjua mtu aliye na sifa za kisaikolojia," anasema Marsh, ambaye ameanzisha shirika lisilo la faida linaloitwa Psychopathy Is.

Inatoa mojawapo ya majukwaa machache ya mtandaoni yanayotoa usaidizi kwa watu walio na ugonjwa wa akili na wale walio karibu nao.

"Wataalamu wengi, ikiwa ni pamoja na Marsh, wanaamini kuwa ni wakati wa kuondokana na unyanyapaa unaozunguka ugonjwa wa psychopathy.

Sababu za kimsingi za ugonjwa wa akili bado hazijaeleweka vizuri, ingawa utafiti unaokua wa uchunguzi wa neva unasaidia kubainisha baadhi ya uwezekano wa matatizo ya neva katika ubongo ambayo yanaweza kueleza dalili. Utafiti, kwa mfano, umeonyesha kuwa wanaume walio na tatizo hilo la akili wana mwitikio mdogo katika maeneo ya ubongo kuhusiana na hofu na kuna baadhi ya vidokezo kwamba athari sawa zinaweza kupatikana kwa wanawake.

Lakini kama utafiti mwingi juu ya saikolojia, matokeo haya yako mbali na uthibitisho na bado yanahitaji kuchunguzwa zaidi.

Jenetiki na mazingira ambayo mtu hujikuta ndani yake pia ni sehemu muhimu za fumbo.

Lakini ili kupata majibu hayo itahitaji jamii pana zaidi kukuza uhusiano uliokomaa zaidi na saikolojia, Marsh anaamini.