'Nilijifunza lugha ya ishara ili kumchumbia mke wangu'

Iliyochapishwa

Abdol anatuambia kuhusu hali isiyo ya kawaida ya kukutana kwake na mpenzi wake wa roho, mkewe ambaye ni kiziwi na bubu.

Hiyo ilikuwa miaka mitatu iliyopita. Akielekea kuchumbiana, Abdol anaamua kuburudisha pumzi yake kwa chapa anayoipenda zaidi ya kutafuna mint.

“Nilisimama kwenye duka la kwanza kulipia pipi za kutafuna na muuzaji akaniambia hakuna. Kwa hivyo naendelea hadi duka la pili ambalo bado naambiwa hakuna ubani. Nikasema sawa, kwa hivyo naendelea na safari yangu na kwenda duka la tatu. Na bado naambiwa kuwa hakuna ubani{ chewing gum}.

Kisha anakubali kuendelea na safari yake, kwa kuogopa kumsubiri rafiki yake.

Mita chache kutoka mahali anapofanyia mikutano, anamwona muuzaji mbele ya meza yake ambayo juu yake kuna pakiti za sigara, biskuti na peremende nyinginezo.

Ishara ya hatima

Abdol kisha anaamua kujaribu bahati yake mara ya mwisho. Hatuambii iwapo aliweza kupata ubani wake {chewing gum}. Lakini hakika amepata mwenzi wake wa roho..

Baada ya kumsalimia bila kupata jibu, anamwomba muuzaji huyo amuuzie ubani huo.

Badala yake anampa pakiti ya sigara. Anaweka  chini akiashiria alikuwa amevurugwa akili na anampatia pakiti nyengine . Wakati huu, ni pakiti ya biskuti

Anakuwa na wasiwasi na anapokaribia kukata tamaa, mwanamume aliyekuwa karibu naye anamweleza kwamba mwanadada huyo ni kiziwi na bubu.

“Niligeuka kumwangalia tena. Nilihisi ujumbe mzito. Kuna kitu kikali ambacho kilivuma ndani yangu,” anakumbuka Abdol.

Aliniambia Abdol, hii ni yako, usiende uiache hapa. Kwa hiyo nikamwambia yule bwana akamwambia yule msichana kwamba ninamwona ni mrembo sana na ningependa kuwa na uhusiano naye.

Jibu la muuzaji lilikuwa ni hapana. Amewaona wanaume wakipita ambao walidhani wangeweza kuchukua fursa ya udhaifu wake kwa urahisi. Abdol lazima alisisitiza kwamba akutane naye siku iliyofuata. Hawakuachana kamwe.

Ishara za mapenzi

Ili kuweza kuwasiliana katika mahusiano yao , Abdol anaamua kujifunza lugha ya ishara

Alienda kujifunza lugha ya ishara katika taasisi ya Deaf Youth of Faso mjini Ouagadougou. Kilichonigusa sana ni wakati alivyoniambia anataka kujifunza lugha ya  ishara. Kwa mtu anayeweza kusikia , nilimuuliza kulikuwa na hamu gani ya kutaka kujifunza lugha ya ishara?

‘Aliniambia kwamba mkewe ni bubu na kiziwi. Hilo lilinipatia nguvu na ari ya kutaka kuendelea kujifunza ili kujaribu kumpatia elimu ya somo hili ili aweze kuwasiliana na mkewe’.

Abdol anaishi zaidi ya kilomita 30 kutoka kwa taasisi hiyo . Alilazimika kuvuka eneo kubwa la mji ili kufika darasani.

Lakini hiyo sio changamoto aliyopitia pekee : mwanzoni marafiki zake wengi na hata watu wa karibu wa familia waliona aibu nilipomkutanisha nao , lakini sasa yote hayo yamepitwa na wakati.

Abdol na mkewe sasa wanajivunia mtoto wa kike wa miaka miwili. Nadhani nilikuwa na bahati kwasababu ni mke mrembo sana na alinipatia mtoto mzuri sana.

Wanandoa hao wanafurahia Maisha mazuri : Kuishi na mwanamke mlemavu sio jambo la kawaida duniani . sio laana tunaweza kupendana na kuelewana

Abdol hahisi aibu kuonekana na mkewe, ndio maana amekuwa akitoka naye na kwenda kucheza densi katika klabu za burudani.

 

Lakini je anwezaje kucheza densi ilihali hasikii muziki huo? "Hasikii lakini nahisi midundo na ninamshika karibu yang una kucheza naye densi pamoja"

Ulemavu wa mkewe Abdol unko mbali na kuwa kikwazo kwao kama wanandoa , na badala yake huutumia kama nguvu yao .  “lengo letu ni kuimba kwa kutumia lugha ya mabubu na viziwi, hicho ndicho mimi na mke wangu tanataka kufanya.