Teknolojia mpya ya kupunguza maumivu wakati wa hedhi

th

Chanzo cha picha, PAULA FISCHER

Maelezo ya picha, Paula Fischer alishiriki katika majaribio ya kutengeneza vazi la mwili ambalo linalenga kupunguza maumivu wakati wa hedhi
Iliyochapishwa

Paula Fischer aliposoma kwa mara ya kwanza kuhusu utengenezaji wa vazi la mwili linaloweza kuvaliwa ambalo husaidia kupunguza maumivu ya hedhi, kijana huyo mwenye umri wa miaka 33 anasema "alifurahi sana kulijaribu".

Kama wanawake wengi, yeye hupata usumbufu mkali wakati wa hedhi, na alikuwa na matumaini ya kupata suluhisho mbadala kwa dawa za kutuliza maumivu, ambayo ilisaidia kwa saa kadhaa tu.“Mara nyingi nilikuwa na maumivu makali sana wakati wa siku zangu za hedhi hivi kwamba sikuweza kuamka kutoka kwenye kochi kufanya kazi yangu,” asema Paula, anayeishi Budapest, Hungary.

 "Hii iliathiri kila kitu - uchangamfu wangu, motisha, uwezo wangu wa kufanya kazi."Kisha miaka miwili iliyopita, aliona arifa kwenye mitandao ya kijamii kutoka kwa kampuni mpya ya Hungary , Alpha Femtech, ikiomba watu wa kujitolea kusaidia katika kupima na kutengeneza vazi jipya la mwili ambalo linalenga kupunguza maumivu wakati wa hedhi.

Waombaji walipaswa kukamilisha uchunguzi kuhusu mzunguko wao wa hedhi, na kisha daktari ambaye ni mtaalamu wa afya ya wanawake alichagua washiriki wanaofaa zaidi. Paula alikuwa mmoja wa wale waliochaguliwa.

Suti itakayotolewa, inayoitwa Artemis, itapatikana kununuliwa nchini Uingereza na EU kwa mara ya kwanza baadaye mwaka huu. Inafanya kazi kupitia paneli za joto zilizojengwa ndani na tens (transcutaneous electrical nerve stimulation) na pedi za gel.

th

Chanzo cha picha, MARTON MARTOS

Maelezo ya picha, Wanamitindo waliovalia mavazi ya Artemis, huku mashine ya tens na kifurushi cha betri kikionekana kwenye kiuno cha mwanamke upande wa kushoto.

Ya mwisho, ambayo hutumiwa mara nyingi na wanawake wakati wa kujifungua, hutoa mapigo ya umeme. Hizi zinasemekana kuzuia ishara za maumivu kufikia ubongo. 

Wakati huo huo, paneli za joto hupunguza makali kwenye mfuko wa uzazi na misuli iliyo karibu.

Ili kuwasha vazi hilo, mtumiaji huambatisha kifurushi kidogo cha betri, saizi ya kiganja, na mashine ya tens ambayo hutoshea kwenye mfuko mdogo kwenye suti, au inaweza kubanwa tu. 

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Hii basi huunganisha bila waya kwa kutumia Bluetooth kwenye programu kwenye simu ya rununu ya mtumiaji, ambayo hutumika kurekebisha viwango vya joto na umeme.

Paula anasema kuwa alipovaa vazi hilo la mwili wakati wa kupima hedhi yake "ilikuwa hali tofauti kabisa", bila maumivu kidogo. 

Anaongeza kuwa nyenzo za suti hiyo, ambazo zimetengenezwa kwa mchanganyiko wa pamba na nyuzi bandia ni "starehe ... nzuri kuvaa".

Madhara pekee ambayo anasema alikuwa nayo ni kwamba hedhi yake ilikuwa nzito kuliko kawaida. "Nadhani kutokana na athari za kupumzika kwa misuli."

Suti hiyo ya mwili imeundwa na mwanzilishi mwenza wa Alpha Femtech, Anna Zsofia Kormos, ambaye ana shahada ya udaktari ya teknolojia inayoweza kuvaliwa na inalenga hasa afya ya hedhi. 

Mshirika wake wa kibiashara, Dora Pelczer, anatoka katika tasnia ya matangazo ya kibiashara.

"Tulizungumza na wanawake 350 kuhusu tabia zao za hedhi, ili tuweze kutengeneza bidhaa ambayo ni rafiki kwa mtumiaji," asema Bi Pelczer. 

Anaongeza kuwa yeye na Bi Kormos walitaka suti hiyo ya €220 ($140; £194) ionekane kama bidhaa ya mtindo kuliko kifaa cha matibabu.

Dubliner Rebecca Powderly sio tu ana hedhi chungu, lakini pia anapaswa kuvumilia hali ya matibabu inayoitwa endometriosis.

Inasemekana kuathiri mwanamke mmoja kati ya 10, endometriosis hutokea wakati tishu zinazofanana na ukuta wa tumbo la uzazi hukua mahali pengine ndani ya mwili, kama vile kuzunguka ovari na kibofu.

 Uvimbe huo husababisha vidonda vya ndani na makovu, na maumivu yanaweza kuwa makubwa.

Ili kujaribu kujifariji, Rebecca anasema alikuwa akitembea na chupa ya maji ya moto. 

Msichana huyo mwenye umri wa miaka 28 angefanya hivyo hata nyakati za usiku, jambo ambalo anasema lilimsababishia kupata "mionekano isiyo ya kawaida".

Lakini tangu Septemba, Rebecca amebadilisha chupa ya maji ya moto kwa bidhaa nyingine ya teknolojia inayoweza kuvaliwa ambayo imeundwa kupunguza maumivu ya hedhi.

th

Chanzo cha picha, REBECCA PODA

Maelezo ya picha, Rebecca Powderly anasema kutumia mashine ya tens husaidia kupunguza kiwango chake cha maumivu

Imepewa jina Myoovi, ni mashine ndogo isiyotumia waya ambayo mtumiaji huibandika kwenye ngozi yake ama chini ya kitovu au sehemu ya chini ya mgongo.

Kitengo cha kati chenye umbo la diski chenye kipenyo cha karibu 8cm (inchi tatu) huweka pedi ya tens gel , betri inayochajiwa na USB na vitufe vya kudhibiti. 

Hii inaingia kwenye ukanda wa kitambaa chenye umbo la kipepeo unaoweza kubadilishwa, ambao, kama plasta kubwa, inanata upande mmoja, na inasemekana kuwa nzuri kwa matumizi kati ya mara 20 na 30 kabla ya kuhitaji kutumia nyingine.

"Tens ina utendakazi wa kipekee," anasema Rebecca. "Ni ngumu kuelezea. Kwenye mipangilio ya juu mapigo yanaweza kuwa makali, lakini inafanya kazi kwa maumivu yangu.

th

Chanzo cha picha, MYOOVI

"Kwangu mimi ahueni ya maumivu huanza mara moja. Haiondoi kabisa maumivu ya kuchomwa na kisu ninayopata, lakini inayapunguza.

Naona ahueni kubwa ninayopata ni kutokana na maumivu ya mara kwa mara, yasiyo na nguvu ninayopata.

"Myoovi ilizinduliwa mnamo Oktoba 2021, kwa bei kutoka £60. Kwa hiyo unapata moja ya diski, na vipande viwili .Bidhaa hiyo imetengenezwa na kampuni mpya inayotumia jina hilo hilo huko Manchester. 

Afisa mkuu mtendaji Dk Adam Hamdi, alikuja na wazo hilo baada ya kuona ufanisi wa mashine za tens wakati akifanya kazi kwa NHS.

Alitaka kuunda toleo lililo rahisi kubeba , bila waya, ili wanawake walio na uchungu wa hedhi, endometriosis, au hali nyingine inayoitwa polycystic ovary syndrome , waweze kuitumia popote.

Dk Karen Morton, daktari wa uzazi na mwanajinakolojia, na mwanzilishi wa nambari ya usaidizi ya matibabu ya Dk Morton, anaelezea jinsi mashine za tens hufanya kazi.

 "Zinatumia nadharia iitwayo 'gating theory of pain' - kwa kuweka kichocheo kwenye uti wa mgongo juu ya mahali ambapo maumivu huingia, kuzuia njia ya maumivu kufika kwenye ubongo wako," anasema. 

"Joto linaweza kufanya vivyo hivyo."Hata hivyo, anasisitiza kuwa wanawake wowote wanaosumbuliwa na hedhi au maumivu mengine ya uzazi wanapaswa kwanza kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu.

Dk Steve Allder ni daktari mshauri wa magonjwa ya mfumo wa neva - daktari anayetambua na kutibu magonjwa ya ubongo, uti wa mgongo na mfumo mpana wa neva.

Anasema kuwa ingawa tafiti zimeonyesha kuwa mashine za tens zinafaa katika kupunguza maumivu, kuna changamoto ibuka kuzitumia. 

"Haijulikani wazi ni muda gani, idadi, na marudio ya matibabu, kwa sababu ya uwezekano wa maendeleo ya tabia na uvumilivu katika matumizi ya mara kwa mara ya tens'

Dk Hamdi kutoka Myoovi anasisitiza kuwa hakuna kikomo cha muda gani vifaa hivyo vya tens vinaweza kutumika, na badala yake inategemea jinsi mtu anavyostareheshwa na hisia za umeme.

Huko Budapest, Paula anasema ana nia ya kupata vazi la Artemis ambalo hatalazimika kurudisha. "Siwezi kungoja iwe sokoni ili hatimaye niweze kuitumia mara kwa mara."