Malkia Elizabeth II: Nchi 6 zinazotaka kujitenga na utawala wa kifalme wa Uingereza

Queen

Chanzo cha picha, Getty Images

Iliyochapishwa

Barbados iliamua Novemba mwaka jana kwamba Malkia Elizabeth II hatakuwa tena mkuu wake wa serikali. Kwa hili, ikawa Jamhuri ama nchi changa zaidi ulimwenguni, jina ambalo inalishikilia hadi sasa. Lakini sio nchi pekee ya Caribbean ambayo iliamua kufanya hivyo. Kuna nyingine sita: Antigua and Barbuda, Bahamas, Belize, Grenada, Jamaika, and Saint Kitts na Nevis.

Serikali zao zimeanzisha taratibu za kuukana utawala wa kifalme au angalau zimeeleza nia yao ya kuwa jamhuri na pamoja na hayo, kuwa na mkuu wao wa nchi. Jamaica iliyo na watu wengi zaidi, imeunda kamati ya kusimamia mchakato wa mabadiliko ya katiba. Belize imetenga fedha katika bajeti yake kwa tume ya awali na huko Grenada wanasiasa kadhaa wanataka kura ya maoni.

Historia fupi kuhusu utawala huu

Kwa kuongezea katika nchi hizi 6, zipo nchi zingine 8 ambazo Malkia Elizebeth II bado ni mkuu wa nchi hizo; Australia, Canada, Visiwa vya Solomon, New Zealand, Papua New Guinea, Saint Lucia, Saint Vincent and the Grenadines, na Tuvalu.

Nchi hizi 14 zinazoitwa "Commonwealth realms" zilikuwa sehemu ya Milki ya Uingereza, ambayo zilipata uhuru. Ndani yao kuna sura ya "gavana mkuu", sawa na rais katika Jamhuri, ambaye ni mwakilishi wa malkia katika kila taifa na ambaye nguvu yake ni ya ya kisherehe zaidi kuliko kuwa na nguvu halisi.

Jumuiya ya Madola au Jumuiya ya Madola ya Uingereza ni jumuiya ya nchi zilizounganishwa moja kwa moja na Uingereza ambazo hudumisha uhusiano wa karibu wa kibiashara na mabadilishano katika maeneo mengine kwa manufaa ya pamoja kama lengo.

Licha ya kutokuwa tena taifa la "ufalme", ​​Barbados bado ni mwanachama wa Jumuiya ya Madola, ambayo kwa jumla inaleta pamoja mataifa 54, yakiwemo mawili ambayo hayajawahi kuwa makoloni ya Uingereza: Msumbiji na Rwanda.

Na sasa, kwa nini Jamaica na nchi nyingine tano zilizotajwa zinataka kujitenga na ufalme wa Uingereza?

Zama za mtumwa na harakati za BLM

"Kadiri nafasi ya malkia inavyozidi kuonekana katika siasa za ndani za nchi hizi, utawala wa kifalme wa Uingereza unaonekana kama masalio ya ukoloni," Solon Solomon, profesa wa Sheria ya Umma na Kimataifa katika Chuo Kikuu, anaiambia BBC.

Kwa wasomi, "haja ya kuachana na ukoloni wa zamani ni, msukumo fulani ama nguvu fulani kabla ya Mwanamfalme William" alipotembelea Jamaika, Belize na Bahamas katikati ya Machi.

Malkia

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Waandamanaji wa Bahamas wakiandamana kutaka fidia kutokana na maswahibu ya ukoloni

Huko Jamaica, William, mwanamfalme, alionyesha "huzuni yake kubwa" kwa kipindi cha utumwa na kusema kwamba "haipaswi kamwe kutokea", maneno ambayo baadhi ya wenyeji waliona kuwa hayatoshi kwa kutokuwa na msamaha wa wazi.

Mia

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wziri Mkuu wa Barbados Mia Amor alipokuwa nazungumza na umma, November 30.

Wanataaluma wanasema kwamba "athari ziitakuwepo" imetokea: mara Barbados ilipochukua hatua na kuwa Jamhuri, majirani zake wameona hali nzuri ya kushughulikia mipango kama hiyo. Kwa hivyo nini kitabadilika ikiwa nchi hizi zitakuwa jamhuri ama zitajitenga na ufalme wa Uingereza?

Kitu kitu cha kufanana, lakini sio sana kwa Uingereza

Wasomi wanakubali kwamba kwa nchi zinazotarajia hakuna kitu kitakachobadilika hasa katika hatua hiyo ni kidogo sana.

Huko Barbados, kwa mfano, majina ya idara zingine, kama vile polisi, yalibadilishwa kwa kuondoa sifa za "kifalme".

Na nafasi ya Gavana Mkuu ikawa ya Rais wa Jamhuri, ambaye sasa ni Mkuu wa Nchi na hamuwakilishi tena Malkia, ingawa kazi zake zinaendelea kuwa za sherehe na hana uwezo wa kuingilia maswala ya umma na serikali. .

Walakini, kwa Uingereza, na haswa kwa utawala wake wa kifalme, mabadiliko kama yale ya Barbados yanajumuisha "hasara kubwa", anasema msomi Solon Solomon.

Kuhusu familia ya kifalme, "kupotea kwa falme wakati wa utawala wa Elizabeth II hutuma ishara za kutisha kwa warithi wake, Princes Charles na William."

Queen

Chanzo cha picha, Getty Images

"Hakuna wengi wanaotamani mabadiliko"

Ili kuwa Jamhuri, mataifa sita ya Carribea yanahitaji wabunge wengi na, karibu katika hali zote, kura ya maoni ambayo raia wake wanaunga mkono mpango huo.

Lakini, je, kuna maoni mengi ya umma yanayounga mkono kubadilisha hali iliyopo?

"Mfano wa Barbados pengine unaonyesha hali halisi katika maeneo mengine. Wengi wa wakazi hawana wasiwasi kuhusu hilo," anasema Profesa Goddard.

Msomi wa Barbadia anaamini kwamba, kwa upana wake, katika falme za Caribbean za Jumuiya ya Madola "unapata idadi nzuri ya watu wasiojali , wengine wengi wanaounga mkono harakati na wachache wachache ambao wanataka kuendelea na malkia".

Vyovyote iwavyo, anasema, "kwa watu wengi katika nchi hizi hatua hiyo isingekuwa na athari yoyote katika maisha yao ya kila siku."