Mzozo Ukraine: Wanawake wenye jinsia tofauti na waliozaliwa nayo wamekwama Ukraine

Nikita, 29, is wearing red lipstick and posing for the camera

Chanzo cha picha, Handout

Maelezo ya picha, Nikita, mwenye umri wa miaka 29, sasa yuko katika makazi ya watu wenye jinsia tofauti
Iliyochapishwa

Mamia ya wanawake waliozaliwa na jinsia tofauti wanaojaribu kuikimbia Ukraine wamezuiliwa mpakani.

Mashirika ya kutoa misaada yameiambia BBC kuwa asilimia 90 ya wanawake waliozaliwa na jinsia tofauti ambao walikuwa wanajaribu kuwasaidia kutoroka nchini humo wameshindwa kufanikiwa.

Wanaume wa Ukraine wenye umri kati ya miaka 18-60 wamepigwa marufuku kuondoka nchini, na vitambulisho vingi vya watu wa waliobadili jinsia bado vina majina yao ya kuzaliwa na jinsia.

Hii imewalazimu wengine kudanganya kuwa wamepoteza hati zao za kusafiria au kutumia njia zisizo halali.

Wengine, kama Nikita mwenye umri wa miaka 29, ambaye amekwama na kuhisi hatari.

Kama ilivyo kwa watu wengi waliobadili jinsia nchini Ukraine, Nikita hajapitia mchakato wa kubadilisha jina na jinsia kwenye pasipoti yake, ambayo inahitaji uchunguzi wa kina na taarifa za kitibabu.

Hii ina maanisha nakala zake zinamtambua kuwa ni mwanaume.

Baada ya kutoroka nyumbani kwake huko Chernihiv, Nikita alijaribu kuvuka mpaka na Moldova, lakini anasema alikejeliwa kwa jinsia yake na wasimamizi wa mpakani na kushindwa kuondoka.

Machapisho yake kwenye mitandao ya kijamii siku chache kabla ya uvamizi wa Urusi yanaonesha msichana anayejiamini, mchangamfu aliyejiremba na anapenda kuimba na kucheza.

Lakini anapozungumza kutoka kwa makao yake ya sasa - makazi ya jinsia mchanganyiko huko Turnipol - yeye yuko kimya, amejitenga na anasema anahisi kama "yuko kwenye ngozi ya mtu mwingine".

A woman looks at the camera seriously wearing a hoodie and red t-shirt

Chanzo cha picha, Nikita

Maelezo ya picha, Nikita anasema anahisi kutokuwa salama kwenye makazi hayo, kwa hivyo inambidi kuvaa nguo za kiume

Vitu vyake ambavyo vingeweza kutosha kwenye mkoba mdogo na amechukua hatua za kuficha utambulisho wake: kuficha nywele zake ndefu, kutovaa vipodozi vyovyote na kubadilisha nguo zake na kuvaa za kiume.

Alisema: "Najihisi kuwa siko huru sababu nilibadili jinsia kuwa mwanamke, lakini hati yangu ya kusafiria inasema kuwa mimi mwanaume."

Ingawa wapenzi wa jinsia moja+ hawajapigwa marufuku kuhudumu katika jeshi nchini Ukraini, Nikita hajisikii salama kufanya hivyo na anaamini kuwa atakataliwa kwa sababu ya utambulisho wake.

Aliongeza: "Sidhani kama wanajeshi wangenielewa na sijui wangefanyaje kama wangegundua kuwa mimi ni mwanamke ambaye niliyebadili jinsia. Haingekuwa salama kwangu kujiunga."

Anastasiia Domani ni mkuu wa moja ya mashirika kuu ya Ukraine ya waliobadili jinsia, Cohort.

Anasema watu wengi waliovuka mipaka ambao amekuwa akiwasaidia hawajapitia mchakato wa kubadilisha pasipoti zao, na kusimamishwa kwa baadhi ya huduma za matibabu wakati wa vita kunamaanisha kuwa hawataweza sasa.

A woman pours a bag of medication onto a table

Chanzo cha picha, Olena Shevchenko

"Kwa sasa, ushauri wetu kwa watu ambao wamebadili jinsia ambao bado wana utambulisho wa jinsia ya kuzaliwa nayo na jina kwenye pasipoti zao ni kwamba wasitembelee mpaka," alisema.

"Takriban 90% au hata zaidi ya wanawake tunaowasaidia wanakataliwa mpakani kwa sababu hawana utambulisho sahihi wa jinsia zao kwenye pasipoti zao."

Tangu uvamizi wa Urusi uanze, kumekuwa na jitihada mbalimbali za makundi ya wapenzi wa jinsia moja na wanaharakati na mashirika ya kutoa misaada yanayotoa usaidizi, huku wengi wakichagua kusalia nyuma ili kusaidia.

Kama mwanamke ambaye alizaliwa na jinsia tofauti na kupitia mhakato wa kubadilisha pasipoti yake, Anastasiia angeweza kuvuka mpaka kwa usalama lakini akachagua kubaki huko Kyiv.

Baada ya kumsaidia mke wake wa zamani na binti yake kuhama kwa usalama, amebadilisha nyumba yake kuwa sehemu ya juhudi zake za kusaidia watu waliobadili jinsia kutoka Ukraine.

Anasaidia kushauri watu wanaotarajia kuvuka mpaka, kupanga na kusambaza dawa na kutuma pesa kwa wale wanaoishi kwenye makazi ili kununua chakula na kutoa mkopo wa simu za rununu ili waweze kuwasiliana na familia na marafiki.

Olena Shevchenko shouting over a megaphone at a pride demonstration

Chanzo cha picha, Insight Ukraine

Maelezo ya picha, Olena Shevchenko amekuwa mwanaharakati na mpenzi wa jinsia moja tangu mwaka 2008

Olena Shevchenko, ni mkuu wa Insight Ukraine, shirika la kutoa misaada la wapenzi wa jinsia moja ambalo limeanzisha makazi maalum huko Lviv na Chernivtsi kwa ajili ya wapenzi wa jinsia moja ambao wamelazimika kukimbia makazi yao.

Pia hutoa usaidizi wa kisaikolojia, ushauri na usaidizi wa kusambaza dawa kama vile homoni za jinsia tofauti kwa wale ambao hawawezi kukimbia Ukraine na wanatatizika kuzipata.

Tangu habari kuhusu makazi hayo kuenea, wamekuwa na maombi ya kutaka msaada.

"Mara nyingi mimi hupokea zaidi ya barua pepe 50 za kuomba usaidizi - yani ninahisi kama siku inakuwa haiishi. Ni saa 24/7," Olena alisema.

"Tunaposaidia wapenzi wa jinsia moja. Wanavuka mpaka na tunapata hisia za furaha sana, wakituambia walivuka salama.

"Kwa watu wa waliobadili jinsia , ni hali tofauti kabisa. Hatujui kama itafanikiwa au la. Hatujui la kuwaambia."