'Sikujua nina mimba ya miezi mitano' - je hali ya kukataa mimba kwa wanawake ikoje?

Iliyochapishwa

Yacine Bal sasa ni mama wa watoto wawili. Lakini mnamo 2015, alipata ujauzito ambao ulimpa wakati mgumu.

Wakati huo akiwa binti mdogo ambaye ametoka tu kuolewa , alikuwa mama wa mtoto wa kike wa miezi 7 ambaye alikuwa bado ananyonya, Yacine Bal alikuwa anatarajia kupata mtoto wa pili bila yeye mwenyewe kujua.

"Tofauti na ujauzito wa binti yangu mkubwa ambao ulikuwa una changamoto nyingi , nilikuwa naumwa muda wote, huo ambao haukuonekana nilikuwa naonekana kawaida tu.

Nilikuwa nafanya kazi vizuri na nikiwa mkubwa wa familia, nilikuwa mratibu wa sherehe za familia," anasema Bi. Yacine Bal, ambaye bado haelewi kilichomkuta.

Hakuwa na dalili za kumshuku kuwamjamzito.

Hakuwa na uchovu, hakuna kichefuchefu na hedhi alipata kama kawaida, hakuna dalili inayoweza kumfanya ahisi kuwa amebeba ujauzito.

Kulikuwa na sherehe ya familia ambapo mama yake, Maguette Guèye, aliona mabadiliko: "Alifikiri nilikuwa na tumbo dogo, ambalo ni gumu sana.

Halikuonekana sana lakini alifikiri nilikuwa na fibroids hivyo akasisitiza niende kumuona daktari. Sikutaka kwenda hospitali , lakini aliishia kunishawishi.

Daktari wake wa magonjwa ya wanawake anapomwambia kwamba ana ujauzito wa wiki 25, na kwamba anatarajia mtoto wa kiume, Yacine Bal alishtuka.

Yacine alikuwa na uhakika kwamba upandikizaji aliouweka kama njia ya uzazi wa mpango na kunyonyesha kwa binti yake kulimlinda kutopata ujauzito.

Yacine Bal na mumewe walikuwa wamefanya uamuzi wa kungoja miaka minne au mitano kabla ya kupata mtoto wa pili.

Msichana huyo alikuwa amechagua aina hii ya uzazi wa mpango ambayo ilimhakikishia kwamba hakutakuwa na hatari ya kusahau. Hivyo kwa msichana huyo ujauzito ni jambo ambalo lilimshangaza na hakulitarajia kabisa.

Kukataa mimba kukoje?

Kwa mujibu wa Dk. Sokhna Seck, daktari wa akili wa Senegal, anasema kuwa mwanamke "kukataa mimba ni kukataa hali halisi yenye kuhuzunisha.

Kunaweza kuchambuliwa kama kukataa kwa mwanamke kuwa mjamzito. Labda kwa sababu mimba ya awali ilienda vibaya na mwanamke hataki kupitia hali ile tena.

Kuna aina kadhaa za kukataa mimba: kukataa kabisa mimba wakati wa kujifungua. Kukataa mimba kwa muda fulani wakati mwanamke anapofahamu hali yake kama mama kijacho kabla ya tarehe ya kujifungua, wakati mwingine hata kuchelewa sana.

Dk. Abdoulaye Diop, mtaalamu wa magonjwa ya wanawake anayeishi Dakar, anataka kutofautisha kati ya mimba iliyofichwa ambapo mwanamke anafahamu hali yake na kuificha, na ujauzito uliojificha ambapo mwili unashiriki katika "kuficha" mimba. "Wanawake wanakuwa wanaokataa mimba kwa dhati kwa kuwa hawaoni dalili.

Kwa ujumla, mara tu anapogundua kwamba ana ujauzito na hali ya kuikataa imeisha , mwili wa mama huyo hubadilika, wakati mwingine kwa muda mfupi sana.

Yacine Bal anakumbuka "nilipoingia katika ofisi ya daktari, nilikuwa na tumbo la kawaida na nilipotoka baada ya daktari kuniambia hali yangu tumbo lilikuwa limeongezeka ghafla. Nilikuwa na tumbo la mwanamke mjamzito wa miezi mitano.

Aibu na kutokuelewa

Tangazo la ujauzito huu lilibadilisha maisha ya familia ya Yacine Bal.

Wenzi hao hawakuwa wamejiandaa kulea watoto wawili.

Yacine Bal alilemewa na maswali mengi: "jinsi ya kupata pesa? watu watanifikiriaje . Nilikuwa na miaka 26 lakini bado nilikuwa nasoma. Kila mtu anajua kuwa tayari ninalea mtoto sio rahisi, tena wawili ... "

Wanandoa hao ambao waliishi Dakar wakati huo na binti yao wa miezi 7, walilazimika kufanya uamuzi wa kuendelea na ujauzito huu wakiishi tofauti.

Yacine Bal anarudi kuishi na mama yake huko Thiès, mji ulio kilomita 68 kutoka Dakar.

Licha ya dhihaka za baadhi ya wanawake wanaomzunguka, anaweza kutegemea familia yenye uhusiano wa karibu ambayo itamsaidia katika muda wa miezi minne wanayokaa kabla ya kujifungua.

Hadi sasa, hakuna utafiti juu ya mimba kutoonekana nchini Senegal na hakuna chochote katika bara la Afrika.

Hata hivyo, ukosefu wa data haumaanishi kiwango cha hali hiyo kiko chini. Dk. Abdoulaye Diop anasema amekumbana na visa vingi katika taaluma yake.

"Kutokujua kuwa mtu una ujauzito kwa sehemu nadra kuliko unavyofikiria. Ninaona kesi moja au mbili kwa mwezi katika ofisi yangu. Shida ni kwamba wanawake hawa wanaona aibu kwa kutoelewa kilichokuwa kikiendelea katika miili yao hivyo hawazungumzi," aeleza.