Chile limekuwa taifa lenye Rais mwenye umri mdogo zaidi duniani

Gabriel Boric, 36, ameapishwa kuwa rais mpya wa Chile - rais mwenye umri mdogo zaidi duniani.
Katika hotuba yake ya kuapishwa kwa taifa, Rais Gabriel Boric, mwanafunzi na mwanaharakati, alisema atashughulikia ukosefu wa usawa kati ya raia na wale ambao walizua maandamano ya ghasia mnamo 2019.
Pia alisema kuwa ataboresha sekta ya elimu na kuboresha mfumo wa afya, miongoni mwa mengine mengi.
Pia atafanya mabadiliko makubwa katika jeshi la polisi ambalo limekuwa likilaumiwa kwa kuua mamia ya waandamanaji.
Hatimaye, aliapa kuongeza wigo wa demokrasia ya Chile, wanawake kuwa na haki ya kupiga kura na kugombea nyadhifa mbalimbali.
Bw. Boric, muandamanaji mashuhuri katika chuo kikuu na mhusika mkuu katika machafuko ya 2019 nchini humo, alitoa wito wa mabadiliko katika nchi hiyo yenye utajiri wa mafuta, faida za kiuchumi lakini pia pale ambapo utofauti unaongezeka kati ya matajiri na maskini.
Lakini kwa kuwa chama chake hakina wingi wa kura bungeni na wapinzani wake wengi wa kisiasa nchini Chile, atakabiliwa na changamoto katika kutimiza ahadi zake za kurekebisha mfumo wa ushuru na kurekebisha mipango ya pensheni. na afya.
Lakini inaonekana yeye si aina ya mtu ambaye angekimbia kuacha majukumu yake kwa sababu ya changamoto hizi; Kwa sababu ameweka wazi kuwa anataka mabadiliko - na kwamba wanawake ndio wengi katika baraza lake la mawaziri , mabadiliko yameanza katika serikali ya Chile.














