Uhusiano wa kushangaza kati ya kile unachokula na ubora wa usingizi wako

Iliyochapishwa

Kutopata usingizi wa kutosha kunaweza kusababisha mzunguko mbaya wa kula kupita kiasi na kukosa usingizi zaidi, lakini pia kuboresha mzunguko wako wa kula kwa afya kunaweza kuboresha usingizi wako.

Tania Whalen hawezi kupata usingizi wa kutosha wakati wa zamu zake anapofanya kazi asubuhi sana na usiku katika taasisi ya zimamoto huko Melbourne, Australia. Ili kumsaidia apate asisinzie katika zamu ya usiku ambayo inayomtaka kujibu simu za dharura na kuwatuma wafanyakazi, mara nyingi huchukua vitafunio kazini.

"Inaweza kuwa keki au vitu vingine vya kula ambavyo anaweza kula wakati wa mapumziko, na kumpa nguvu ," anaeleza.

Tania alikuwa akifanya upande wamashine katika kituo hicho cha zimamoto, akinunua krisps au chokoleti majira ya usiku akiwa kazini.

Alijua lishe hii haikuwa na faida kwake - lakini ilikuwa ngumu kuacha.

Na tabia ya Tania haikuwa ya kawaida. Wakati watu hawajapumzika vya kutosha, wanatamani chakula.

"Kuna mabadiliko hutokea katika ubongo na mwili wako unapokosa usingizi wa kutosha, na kukufanya upende kula kupita kiasi na kuongezeka mwili," anasema Profesa Matthew Walker, mkurugenzi wa Kituo cha Sayansi ya Kulala kwa Binadamu katika Chuo Kikuu cha California. .

Tunapokaa macho kwa muda mrefu, tunahitaji nguvu zaidi, lakini sio nyingi: kulala ni mchakato wa kushangaza na akili na miili yetu hufanya kazi kwa bidii, anasema Profesa Walker. Licha ya hili, tunapokosa usingizi, huwa tunakula mara mbili au tatu ya kiasi cha kalori tunachohitaji.

Hii ni kwa sababu usingizi huathiri homoni mbili zinazodhibiti hamu ya kula. Hali inayoashiria ubongo wako kuwa umekula vya kutosha. Wakati viwango vya usingizi ni vya juu, hamu yetu hupunguzwa na hufanya kinyume chake: wakati kiwango chake ni cha juu, huhisi kuridhika na kile amekula.

Utafiti umeonesha kuwa wakati watu wanakosa usingizi, homoni hizi mbili huenda kwa njia tofauti: kuna kushuka kwa alama ambayo inamaanisha kuongezeka kwa hamu ya kula, wakati ambao unawaacha watu kutooridhika.

Ni kama hatari maradufu, anasema Profesa Walker. "Unaadhibiwa mara mbili kwa kosa lile lile la kukosa usingizi".

Kwa nini hili inatokea hivyo?

Profesa Walker anaamini kuwa kuna maelezo ya mabadiliko hayo. Wanyama ni nadra sana kujinyima usingizi isipokuwa wana njaa na wanahitaji kukesha ili kutafuta chakula. Kwa hivyo wakati hatupati usingizi wa kutosha, kutoka kwa mtazamo wa mageuzi, ubongo wetu unafikiri tunaweza kuwa na njaa na huongeza hamu yetu ya chakula ili kutusukuma kula zaidi.

Na kutopata usingizi wa kutosha huathiri si tu kiasi gani tunachokula, lakini pia kile tunachokula.

Utafiti mdogo wa Profesa Walker ulionesha kuwa washiriki walikuwa na uwezekano mkubwa wa kutamani vyakula vya sukari, chumvi na wanga wakati ambao hawajalala usiku.

Kitu ambacho si habari njema kwa wafanyakazi wa zamu ya usiku waliochoka kama Tania Whalen. Kwa kweli, hali inaweza kuwa mbaya zaidi kwao, kwa sababu sio tu kile wanachokula ndio shida, lakini pia wakati wa kula.

Miili yetu imeundwa kufuata mzunguko thabiti wa saa 24, anasema Dk Maxine Bonham, profesa mshiriki wa lishe bora na chakula katika Chuo Kikuu cha Monash huko Melbourne.

"Tunatarajia kufanya kazi, kula na kufanya mazoezi wakati wa mchana, na kulala usiku, na miili yetu imeundwa kwa ajili hiyo. Kwa hiyo unapofanya kazi usiku, unafanya kinyume kabisa na kile ambacho mwili wako unatarajia."

Na hiyo inamaanisha kuwa tunapata shida kumeza chakula tunapokula chakula usiku.

Kula usiku kunaweza kusababisha viwango vya juu vya glukosi na vitu vyenye mafuta mengi kwenye damu kwa sababu mwili hauwezi kunyambua virutubishi ndani ya saa chache, Dk. Bonham anasema.

Wafanyakazi wa zamu ya usiku wanajulikana kuwa katika hatari kubwa ya kuongezeka uzito, kupata kisukari cha aina ya 2 na ugonjwa wa moyo.

Watu wanaofanya kazi za usiku pia wana uwezekano mkubwa wa kuwa na uzito kupita kiasi. Wanaweza kula kwa kuchoshwa au kukesha, na huenda kusiwe na kitu chochote cha afya ambacho wanakula.

Hayo yote yalimfanya Dk. Bonham na wenzake kuanzisha jaribio la kuona ikiwa wangeweza kuwasaidia watu wanaofanya kazi za usiku kupunguza uzito kupita kiasi na kuboresha afya zao kwa ujumla.

Waliajiri wafanyakazi 220 hivi wa zamu ya usiku ambao walitaka kupunguza uzito na kuwaweka kwenye lishe tofauti kwa miezi sita. Tania Whalen, mfanyakazi wa wazima moto, alijiandikisha kwa mpango wa kufunga: kwa siku mbili kwa wiki, ilibidi atumie kalori 600 tu katika saa 24.

"Ilikuwa ngumu," Tania anasema. "Nilikuwa na wasiwasi kwamba nisingeweza kufanya hivyo. Wiki kadhaa nilihisi kama zamu ya saa 12 ilikuwa saa 20."

Lakini alijikita kwenye kusoma, kucheza michezo mbalimba, kutembea na kunywa chai.

Matokeo ya utafiti huo bado haujajulikana, lakini Tania anaamini kuwa uzoefu umekuwa mzuri na umemsukuma kufanya mabadiliko mengine - kwa mfano, sasa anatembea kilomita 5 kila siku. "Hakika nina nguvu zaidi na hamu zaidi ya kuendelea zaidi, na nimepungua uzito," asema.

Inafurahisha, Tania anafikiri kwamba ilimsaidia pia kulala vizuri. "Hata kwa saa chache za usingizi huwa sijirushi na kugeuka sana na nimeacha kukoroma, au hivyo ndivyo mume wangu ananiambia."

Haijulikani ikiwa uboreshaji huu unatokana na lishe mpya, mazoezi, kupunguza uzito, au kitu kingine chochote, lakini inazua swali la ikiwa kile unachokula kinaweza kuathiri usingizi wako.

Kufikia sasa, tumezungumza juu ya jinsi usingizi - au ukosefu wake - unaweza kuathiri kile unachokula. Lakini vipi ikiwa ungeweza kula ili kupata usingizi mzuri wa usiku?

Dk. Marie-Pierre St-Onge ni mtafiti wa lishe na usingizi huko New York. Alitumia miaka kadhaa kusoma athari za kukosa usingizi wa kutosha kwenye lishe, mnamo 2015, aliwasiliana na kamati inayohusika na kuandika miongozo ya lishe kwa Wamarekani. Je, wawashauri watu juu ya nini cha kula ili kuboresha usingizi wao, waliuliza?

"Majibu yangu ya kwanza yalikuwa ni kushangaa kwa nini sikufikiria hilo."

Melatonin, homoni inayokuza usingizi na kuongezeka jioni, hutoka kwa asidi ya chakula inayoitwa trytophan. "Kwa hivyo ikiwa homoni inayodhibiti usingizi wako inatolewa kabisa na asidi ambayo lazima itumike katika chakula, basi ina maanisha kwamba chakula ni muhimu katika kudhibiti usingizi," anasema.

Hata hivyo, Dk. St-Onge hakupata tafiti zilizochunguza uhusiano huu. Kwa hivyo yeye na timu yake walianza kuangalia utafiti wakiangalia maswala mengine ya kiafya, ambayo yalikuwa yamerekodi usingizi wa washiriki na jinsi wanavyokula. Kuchunguza data hii ilitoa muongozo wa wazi, anasema.

Watu waliofuata lishe bora- wanaotumia matunda na mboga nyingi, samaki na nafaka - walikuwa na hatari ya chini ya 35% ya kukosa usingizi kuliko watu ambao hawakufuata lishe hii, na walikuwa na uwezekano mara 1.4 zaidi wa kupata chakula kizuri kuliko kupata usingizi mzuri wa usiku.

Kwa nini lishe hii inafaa wakati wa kulala? Vyakula kama vile samaki, karanga na mbegu vina virutubishi vingi ambavyo hutoa melatonin. Na tafiti kadhaa ndogo zimeonesha kuwa vyakula maalum kama nyanya na matunda ya kiwi, ambayo yanaweza kusaidia watu kulala kwa urahisi na kulala kwa muda mrefu.

Pia kuna vyakula vya kuepuka kula kabla ya kulala. Watu wengi wanajua kafeini, ambayo ni kichocheo, lakini labda hawajui kuwa vyakula vyenye chumvi vinaweza kukufanya uwe na kiu, ambayo inaweza kuvuruga usingizi. Utafiti wa Dk. St-Onge pia unapendekeza kwamba kula vyakula vya sukari kunaweza kusababisha usiku kuvuruga usiku wako zaidi. Timu yake inajaribu kujua ni kwanini.

Uchunguzi juu ya ushawishi wa chakula bora na usingizi bado ni mdogo, hivyo Dk St-Onge anaamini kwamba jambo dogo linaweza kuchukuliwa ukweli wa kisayansi. Walakini, wanaongeza uwezekano kwamba kula vyakula fulani kunaweza kusababisha usingizi bora zaidi.