Moto mkubwa wawaka katika jengo la bunge la Afrika Kusini mjini Cape Town
Moto mkubwa unawaka katika jengo la Bunge katika jiji la Cape Town nchini Afrika Kusini.
Picha za video zinaonyesha moshi mweusi mwingi ukijaa angani, huku miali mikubwa ya moto ikitoka kwenye paa la jengo hilo.
Maofisa wanasema moto huo ulianzia kwenye afisi za ghorofa ya tatu na kuenea kwa kasi hadi kwenye Bunge la Kitaifa (baraza kuu la bunge), anaripoti mwandishi wa BBC Nomsa Maseko mjini Cape Town.
Brigedia Nomthandazo Mbambo alisema mtuhumiwa anatarajiwa kufunguliwa mashtaka chini ya Sheria ya mambo muhimu ya Taifa, ambayo inalinda maeneo yenye umuhimu wa kimkakati. Ingawa maelezo zaidi hayajapatikana bado.
Katika taarifa yake Jumapili usiku, bunge la Afrika Kusini lilithibitisha kuwa kumekuwa na "uharibifu mkubwa" katika upande wa jengo jipya la Bunge hilo, ambao unajumuisha ukumbi wa Bunge la Kitaifa ambapo wabunge huketi. Pia ilisema baadhi ya ofisi "zimeharibiwa vibaya".

Chanzo cha picha, CITY OF CAPE TOWN
Makumi ya wazima moto wako walionekana wakipambana na moto huo; ingawa bado haijafahamika chanzo cha moto huo.
Tukio hilo linakuja saa chache baada ya mazishi ya Askofu Mkuu Desmond Tutu katika Kanisa Kuu la St George, karibu na bunge.
Rais Cyril Ramaphosa ametembelea eneo la tukio hilo na kusema kuwa ni "tukio baya na la kulaaniwa".

Chanzo cha picha, Reuters
Bw Ramaphosa alisema habari za moto huo ni "kurudisha nyuma mambo yaliyokuwa yamepitwa na wakati" na akaongeza kuwa Askofu Tutu pia angekuwa hai angehuzunishwa na tukio la hivyo.
Alisema mfumo wa kunyunyizia maji wa jengo hilo haujafanya kazi ipasavyo, na amewasifu wazima moto kwa kupambana na moto huo kwa muda mfupi.
Mpaka sasa mwanaume mwenye umri wa miaka 51 alikuwa anashikiliwa na kuhojiwa na mamlaka, polisi imesema.


Chanzo cha picha, Rowan Spazzoli/Reuters
Maofisa wanasema moto huo ulianzia kwenye ofisi za ghorofa ya tatu na kuenea haraka hadi kwenye Bunge la Kitaifa (baraza kuu la bunge), anaripoti mwandishi wa BBC Nomsa Maseko mjini Cape Town.
Hakuna watu waliojeruhiwa walioripotiwa na hakuna dalili ya kile kilichosababisha moto huo, mwandishi wetu anaongeza.

Chanzo cha picha, CITY OF CAPE TOWN
Maafisa wa kikosi cha zimamoto na uokoaji walisema inaweza kuchukua saa nyingine nne kuzima moto huo kabisa kwa sababu ya mazulia na sakafu ya mbao iko katika jengo hilo.
Waziri wa miundombinu , Patricia de Lille, awali alisema moto katika Baraza la Mikoa (baraza la juu) umezuiwa, lakini bado unaendelea kuwaka Bungeni.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe

Mjumbe wa kamati ya usalama Cape Town , JP Smith, aliwaambia waandishi wa habari kuwa paa lilikuwa limeporomoka kwa kiasi na kwamba kengele ya kutambua moto haikulia wakati moto huo ulipoanza kuwaka.
"Paa la jengo limeporomoka upande mmoja na moto umeenea hadi kwa mkutano mpya, kulingana na maafisa.
"Wamegundua nyufa kubwa kwenye ukuta, jambo ambalo linatia wasiwasi.
"Wazima moto wanaripoti kwamba walikuwa kwenye eneo la tukio kwa muda kabla ya mfumo wa kutambua moto kuanza na kisha kutoa tahadhari. Kwa hivyo inaonekana kwamba mfumo huo ulichelewa kwa kiasi fulani."
Hakuna mikutano inayoendelea Bungeni kwa sasa kwa sababu ya likizo.

Chanzo cha picha, Reuters
Jengo la Bunge huko Cape Town lina sehemu tatu, na kongwe zaidi ya 1884. Sehemu mpya zaidi zilizojengwa katika miaka ya 1920 na 1980 la Bunge la Kitaifa.
Mwaka jana, moto uliteketeza sehemu ya maktaba ya Chuo Kikuu cha Cape Town, ambayo ilikuwa na mkusanyiko wa kipekee wa kumbukumbu za Kiafrika.













