Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Uingereza: Mpango wa kuondoa daraja la kufuli za mapenzi umeahirishwa kwa mwaka mmoja
Baraza la Kaunti ya Derbyshire nchini Uingereza halitaondoa kufuli 10,000 za mapenzi katika daraja la Weir kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Katika miongo kadhaa iliyopita, maelfu ya watu walimiminika kwenye daraja la Bakewell, Derbyshire ili kusherehekea upendo wao au kukumbuka muda waliopoteza.
Lakini baraza la eneo la Derbyshire mapema mwaka huu lilisema wanataka kuziondoa kufuli hizo ili kufanya ukarabati kwenye daraja hilo.
Hata hivyo hawajazitoa mpaka sasa.
Kwa muda mrefu, watu wengi wamekuwa wakipata hisia tofauti juu ya hizi "kufuli za mapenzi" kwa kuwa kuna ambao wanapata hisia za mapenzi na wengine kuwavunjaka moyo.
Mwanaharakati Richard Young, amabye anataka kufuli hizo zibaki anasema , kuahirishwa kwa mbapogo wa kutoa kufuli hizo ni habari njema.
Bwana Young, alitengeneza kurasa ya Facebook kwa ajili ya kufanyia kampeni kufuli zibaki mjini.
Anasema kucheleweshwa kutolewa kunatoa muda wa ziada kupana ni jambo gani la mbadala linaweza kufanyika.
"Kama baraza linasema kufuli zitaondolewa kwenye daraja na kutoruhusiwa kurudishwa basi watutengea sehemu nyingine ya karibu kuweka kufuli hizo, eneo ambalo litawawezesha watu kutundika kufuli zao .
"Hatufahamu umuhimu wa ukarabati wa daraja hilo lakini baadhi ya kufuli zina thamani kubwa katika maisha ya baadhi ya watu."
Ni jambo linaloumiza moyo
Bwana Young anasema kufuli hizo zinaaminika kuwa kama 10,000 - na zimewekwa na watu kutoka maeneo mbalimbali duniani, wameweka kufuli kama ishara ya kusheherekea mapenzi yao na kuweka kumbukumbu katika maisha yao.
"Kufuli za watu ambao walipoteza watoto wao wapendwa au wazazi zipo hapo.
Ni jambo ambalo linahuzunisha sana.
Anasema daraja hilo lenye mto Wye, lilipata umaarufu kutokana na kufuli hizo za mapenzi- Bakewell Love Locks Bridge.
"Ni eneo linalovutia utalii wa bure," aliongeza.
Josh na Leah ni wapenzi waliokutana Julai 2021 na wamekuja katika daraja hilo la Bakewell ili kuweka kufuli.
Josh anasema: "Tumesikia kuhusu daraja hili na tunadhani ni namna nzuri ya kuimarisha mapenzi yetu kuwa ya milele.
"Natamani wasiondoe kufuli hizi . Kwasababu wazo lilikuwa ni kuwa hapo daima kama mapenzi ni kuwa pamoja milele , tunasubiri baraza kama litaamua kuleta sthari kwa kila mtu."
Gee Atkins na mume wake waliweka kufuli katika daraja hilo siku ya harusi yao mwaka 2017.
Frances Bell, kutoka Tinsley, South Yorkshire anasema yeye aliweka kufuli katika daraja hilo siku ya kumbukumbu ya kwanza ya kifo cha baba yake.
Lilikuwa eneo ambalo walikuwa wanalitembelea kila mara, pamoja.
Kwa mfano taarifa inayosema: "Tunahitaji kufanya ukarabati wa kawaida na tunahitaji kuondoa kufuli hizo ili kufanya kazi hiyo.
"Hata hivyo kazi hiyo ni muhimu sana, na haina haraka itafanyika mwaka 2023.
"Hivyo tunhitaji kuwa na mpango wa kuziweka hizo kufuli au watu wa karibu wapewe fursa ya kuondoa kufuli zao.