DRC:Maandamano yazuka mjini Goma kuhusu ukosefu wa usalama

Iliyochapishwa

Polisi wanatumia vitoa machozi au milio ya risasi hewani kuwatawanya baadhi ya waandamanaji ambao wamekuwa wakifunga barabara kwa mawe katika maeneo mengi ya mji wa Goma nchini DRC tangu mapema leo asubuhi, wakazi wa eneo hilo waliiambia BBC.

Ingawa hali imeanza kurejea kawaida kwa sasa, maafisa bado hawajatoa taarifa yoyote, lakini wakazi wa eneo hilo wanazungumzia kuhusu vifo vya watu wawili.

Kile ambacho hapo awali kilikuwa ni wito wa miji mikuu, ikimaanisha kwamba watu wote walipaswa kukaa nyumbani kugeuka kuwa makabiliano kati ya polisi na baadhi ya waandamanaji.

Mvutano huko Goma ulikuwa katika manispaa 10 kati ya 18 za Goma.

Mkazi mwingine wa eneo hilo aliambia BBC. Utawala, usafiri wa umma na shule zimesalia kufungwa

Mashirika ya kiraia yalitoa wito wa siku ya kususia kushutumu kuongezeka kwa ukosefu wa usalama katika jiji hilo.

Wiki iliyopita, watu watano waliuawa na watu wenye silaha.

Kile ambacho maafisa walithibitisha kuwa uvumi ulioenea katika mitandao ya kijamii kuhusu kuwepo kwa polisi wa Rwanda ili kutuliza ukosefu wa usalama huko Goma umeongeza hasira.