Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mwanaume aliyeoa wanawake 60 na kuwaficha akamatwa
Abu Baker kutoka Jamalpur nchini India, amekamatwa huko Purbadhala, Bangladesh, kufuatia malalamiko ya mke wake Rosy Khanum.
Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 45 anadaiwa kumlaghai mke wake.
Kwa miaka 25 iliyopita, Abu Baker ameoa wake 60, na mke wake wa mwisho ana umri wa miaka 20.
Mkewe mwenye umri wa miaka 60 aliwasilisha kesi mahakamani, akidai kuwa amemtelekeza na kutumia hati ghushi kuoa.
Gazeti la Dhaka Tribune linaripoti kwamba wakati Abu Baker alipokuwa akioa mke wake wa sasa, alijifanya kuwa hajaoa.
Alipokuwa akifunga ndoa na Rosy Khanum, alisema anaitwa Shaheen Alam na akamwomba baba wa msichana huyo amlipe gharama za harusi.
Abu Baker alidai $2,000, lakini baba wa msichana huyo alikataa ombi hilo na kutoa $900.
Hata hivyo, alipotoa mahari, alitoweka kwa mchumba wake, hali iliyomfanya mkewe kuripoti katika kituo cha polisi cha Purbadhala.
"Sababu ya kufanya hivyo ilikuwa ni kupata pesa za kuoa, na nilitaka kupata pesa kutoka kwa wake 59 niliowaoa hapo awali, na hakuna hata mmoja wao aliyejua," alisema Abu Baker.
Mwanaume huyo ambaye ni mwalimu alikamatwa na polisi na kuhojiwa kuhusu hali yake. Aliwaambia alikuwa ameoa wake 60 katika kipindi cha miaka 25, wote walitoa pesa.
Polisi wa Islampur wanasema mwanaume huyo alitumia herufi ghushi na majina mbalimbali na kila mara alijifanya kuwa hajaoa.
Alisema alikuwa akiishi katika jiji moja na wake zake watatu na watoto saba.
Huko India, Wahindu huamini kimapokeo kwamba bibi-arusi hulipa mahari yake kabla ya ndoa na hivyo kupata riziki kwa mchumba wake.