Evil Corp: Safari yangu ya kusaka 'wadukuzi mamilionea' wa Urusi

- Author, Joe Tidy
- Nafasi, Mwandishi wa taarifa za uhalifu wa mtandao
- Iliyochapishwa
Watu wengi wanaosakwa na sana na FBI kwa mashambulizi ya mtandao ni Warusi. Wengine wakidaiwa kufanya kazi na serikali wakipata mshahara wa kawaida, wengine wanatuhumiwa kujipatia utajiri kutokana na mashambulizi ya kikombozi na wizi wa mtandaoni. Kama wangeondoka kwenye ardhi ya Urusi basi wangekamatwa - lakini nyumbani (nchini kwao) wanaonekana kuwa huru.
"Tunapoteza muda wetu," niliwaza huku nikimtazama paka akilamba mzoga wa kuku aliyetupwa. Hakika hakutakuwa tena na dalili yoyote ya mhalifu wa mtandao anayedaiwa kuwa mamilionea kwenye eneo hili katika mji ulioharibika ulio kilomita 700 (maili 400) mashariki mwa Moscow.
Lakini niliendelea kuwa na mkalimani na mpiga picha, na kumfukuza paka huyo kutoka kwenye mlango wa jengo la ghorofa. Tulipobisha hodi kwenye mlango mmoja, kijana mmoja alijibu na mwanamke mmoja mzee mwenye udadisi akachungulia tulipo kutokea jikoni.
"Igor Turashev? Hapana, sitambui jina, "alisema.
"Familia yake imesajiliwa hapa, kwa hiyo wewe ni nani?" tuliuliza.
Baada ya mazungumzo ya kirafiki tulieleza kuwa sisi ni waandishi wa habari kutoka BBC, na ghafla hali ilibadilika.
"Sikwambii alipo na wala usijaribu kumtafuta, hukupaswa kuja huku," kijana huyo alisema kwa hasira.
Sikulala vizuri usiku ule, nikifikiria ushauri unaokinzana ambao nilikuwa nimepewa na watu wa idara ya usalama. Wengine walisema kujaribu kuwasaka wahalifu wa mtandao wanaotoka kwenye ardhi yao ilikuwa hatari. "Watakuwa na walinzi wenye silaha," niliambiwa. "Utaishia shimoni mahali fulani," mwingine alionya. Wengine walisema itakuwa sawa - "Wao ni wasomi wa kompyuta tu."
Wote walisema hatutafika popote ama hatutaweza kuwakaribia.

Chanzo cha picha, US Department of Justice
Wanaoengwa na uhalifu huo ni kuanzia wafanyabiashara ndogo ndogo hadi mashirika ya kimataifa kama Garmin, pamoja na mashirika ya misaada na shule. Ni wale tu tunaowajua.
Idara ya Sheria ya Marekani inasema watu hao ni "majambazi wa benki waliowezeshwa na mtandao" wanaofanya mashambulizi na kujipatia kikombozi, au kuingilia akaunti ili kuiba pesa.
Tangazo hilo lilimfanya Maksim Yakubets, ambaye wakati huo alikuwa na umri wa miaka 32 pekee, kuwa mpambe wa mdukuzi wa Kirusi.
Picha za genge hilo zilizopatikana na Shirika la Kitaifa la Uhalifu la Uingereza, zilionyesha wanaume hao wakiendesha gari aina ya Lamborghini, wakifurahia pesa na kucheza na mtoto wa simba.

Chanzo cha picha, National Crime Agency
Mashitaka ya FBI kwa watu hao wawili yalitokana na kazi ya miaka mingi, ikiwa ni pamoja na mahojiano na waliokuwa wanachama wa genge na uchunguzi mkubwa wa mtandao. Baadhi ya taarifa zilianzia toka mwaka wa 2010, wakati polisi wa Urusi walikuwa wakijitayarisha kushirikiana na wenzao wa Marekani.
Nyakati hizo hazipo tena, zimepita. Serikali ya Urusi mara kwa mara hupuuza shutuma za udukuzi za Marekani dhidi ya raia wake. Kwa kweli, sio tu wadukuzi wanaruhusiwa kuendelea, wanaajiriwa na huduma za usalama pia.
Uchunguzi wetu kuhusu Maksim Yakubets ulianza mahali pasipotarajiwa - uwanja wa gofu umbali wa masaa mawili nje ya jiji la Moscow. Hii ilikuwa ukumbi wa harusi yake ya kuvutia aliyofunga mnamo 2017
Kwa kweli, uso wa Yakubets haujaonyeshwa kamwe kwenye picha ya video iliyorekodiwa na kampuni ya utengenezaji wa video za harusi, lakini anaweza kuonekana akicheza muziki ulioimbwa na mwimbaji maarufu wa Urusi kukipambwa na rangi nzuri ukumbini hapo.

Chanzo cha picha, National Crime Agency
Tukiwa tunazunguka kwenye uwanja wa gofu nilijaribu kupiga hesabu. Kwa kile tulichokuwa tunaambiwa, harusi hii kuu ingegharimu zaidi ya makadirio ambayo nilisikia hapo awali ya karibu $250,000. Lakii gharama ilikuwa karibu na dola nusu milioni, au hata $600,000.
Hatujui siku hiyo maalum ililipiwaje, lakini ikiwa Yakubets alilipa bili hiyo ni ishara ya jinsi maisha yake yalivyo ya kifahari. Wala Igor Turashev, 40, anajiweka kama mtu wa kawaida. Kwa kutumia rekodi za umma, mwenzangu Andrei Zakharov, ripota wa BBC Urusi alipata kampuni tatu zilizosajiliwa kwa jina lake. Zote zina ofisi katika jengo kubwa la kifahari mjini Moscow, Federation Tower, ghorofa kubwa katika eneo la kitajiri.
Kama Andrei alivyoeleza, Turashev hatafutwi nchini Urusi kwa hivyo hakuna anayemzuia kukodisha eneo hili la gharama kubwa la ofisi katikati mwa jiji.
Inaweza pia kuwa rahisi kwake kupatikana miongoni mwa makampuni ya kifedha, ikiwa ni pamoja na baadhi ya makampuni ambayo yanahusika na fedha za siri, kama vile Bitcoin, ambayo Evil Corp inadaiwa kukusanya kutoka kwa waathiriwa wanaopaswa kulipa kikomozi kwa wizi wa mtandao - inaripotiwa kuwa kila shambulizi moja lina thamani ya mpaka dola $10m.
Ripoti ya Bloomberg kwa kutumia utafiti kutoka kwa wachambuzi wa Bitcoin Chainalysis inadai kwamba Jengo la Federation Tower ina makampuni mengi ya crypto ambayo hutumika kama "mashine za pesa kwa wahalifu wa mtandao".
Tuliipiga simu za kampuni zake bila majibu na tukajaribu mawasiliano mengine yaliyounganishwa na Turashev na kigogo mwingine muhimu wa Evil Corp inaeitwa Denis Gusev, na tukatumia njia nyingi kwa simu na barua pepe, lakini hakuna aliyejibu. Andrei na mimi tulitumia muda mrefu kutafuta mahali anapofanyia kazi Maksim Yakubets.
Aliwahi kuwa mkurugenzi wa kampuni ya mamake ya chakula cha mifugo, lakini siku hizi anaonekana hana biashara wala hajaajiriwa popote. Hata hivyo, tulichopata ni eneo ambalo huenda anaishi, kwa hiyo usiku mmoja tulienda kugonga.
"Maksim Yakubets hayupo hapa. Hajakuwa hapa kwa miaka pengine 15. Mimi ni baba yake," alisema.
Tulipigwa na butwaa baba yake Yakubets kukubali kufanya mahojiano ya kupendeza ya dakika 20 kwenye kamera, akilaani kwa hasira mamlaka ya Marekani kwa kumfungulia mtoto wake mashtaka.
Zawadi ya dola milioni 5 za Marekani kwa kukamatwa kwa mwanawe - fedha kubwa zaidi kuwahi kutolewa kwa mhalifu wa mtandao - ilisababisha familia kuishi kwa hofu ya kushambuliwa, Bw Yakubets alisema, akitaka tuchapishe maneno yake.

Chanzo cha picha, US Department of Justice
"Wamarekani walileta shida kwa familia yangu, kwa watu wengi wanaotujua, kwa jamaa zetu. Lengo lilikuwa nini? Haki ya Marekani imegeuka kuwa haki ya Soviet. Hakuhojiwa, hakuhojiwa, hakukuwa na taratibu ambazo zingeweza kuthibitisha hatia yake."
Yakubets na Turashev ni sehemu tu ya orodha inayokua ya raia wa Urusi watakaopewa vikwazo vya mtandao huku nchi za Magharibi zikihangaika kujibu mashambulizi ya mtandaoni. Watu wengi wa Urusi na mashirika yamewekewa vikwazo na kushtakiwa kuliko watu na mataifa mengine duniani.
Hata hivyo Evil Corp inaonekana kutoathirika na hilo. Watafiti wa usalama wa mtandao wanadai wafanyakazi bado wanafanya mashambulizi ya mtandaoni wakiwalenga watu wa Magharibi.
Marekani inadai kuwa Maksim Yakubets na wadukuzi wengine wanaotafutwa - ikiwa ni pamoja na Evgeniy Bogachev, ambaye imetolewa kitita cha $3m kwa atakayesaidia kukamatwa kwake - walikuwa wakifanya kazi moja kwa moja na Idara za kijasusi.
Huenda isiwe bahati mbaya kwamba baba mkwe wa Yakubets, anayeonekana kwenye video ya harusi, ni mwanachama wa zamani wa ngazi ya juu wa FSB. Katika miezi sita iliyopita Marekani na washirika wake wameenda mbali zaidi ya kuweka vikwazo vya mtandao, na kuanza kutumia mbinu kali zaidi.
Nao wameanza kudukua magenge ya uhalifu mtandaoni na wamefanikiwa kuwaondoa baadhi yao nje ya mtandao, angalau kwa muda. Wadukuzi wa serikali ya Marekani wamefanikiwa mara mbili kurejesha mamilioni ya dola za Bitcoin zilizoibwa kutoka kwa waathiriwa.
Juhudi za kimataifa zinazohusisha Europol na Idara ya Sheria ya Marekani pia zimeshuhudia wadukuzi wanaodaiwa kukamatwa nchini Korea Kusini, Kuwait, Romania na Ukraine.
Shughuli hiyo imesababisha baadhi ya magenge makubwa ya mtandaoni yanayodhaniwa yapo nchini Urusi kusimamisha shughuli. REvil, Blackmatter na DarkSide zote zimetangaza kwenye mabaraza kwamba hazifanyi kazi tena kwa sababu za utekelezaji wa sheria.
Hata hivyo, watafiti wa usalama wa mtandao wanasema makundi zaidi yanajitokeza, na mashambulizi yanatokea kila wiki. Jambo hilo halitaisha, wanasema, mradi tu matapeli wa mtandaoni wanaendelea na maisha yao nchini Urusi.














