Mamluki: mambo matano ya kujua kuhusu mamluki barani Afrika

Chanzo cha picha, Getty Images
Mali imeashiria kuwa inapanga kudumisha uhusiano imara na Urusi ili kukabiliana na matatizo yake ya kiusalama.
Wakati wa safari huko Moscow, waziri wa mambo ya nje, Abdoulaye Diop, alisema kuwepo kwa taifa hilo la Mali kunakabiliwa na tishio.
Aliongeza kuwa hali ya kutokuwa na utulivu ikiendelea, Urusi ni mshirika wa kutegemewa.
"Kila wakati Mali imekuwa katika hali ngumu tangu tupate uhuru, Urusi imekuwa nasi siku zote. Leo tuko katika hali ngumu na bado tunamgeukia rafiki huyu ili atusaidie," Bw Diop alisema.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi, Sergei Lavrov, alipuuzilia mbali wasiwasi wa Ufaransa kuhusu mamluki wa Urusi nchini Mali.
Alisema Urusi itaendelea kuipatia nchi hiyo silaha na risasi.Sio mara ya kwanza kwa nchi ya Afrika kujipata na mamluki.
Utumiaji wa mamluki kwa pande zinazozozana limekuwa suala chungu kwa baadhi ya mataifa. Ili kujua ni kwa nini baadhi ya majimbo yanasita kuzitumia, tuliwasiliana na wataalamu wawili wanaozungumzia suala hili: Kanali Mamadou Adje, afisa mkuu wa zamani wa jeshi la Senegal na Dk Boubacar Ndiaye, mtafiti kuhusu masuala ya usalama.
Mamluki ni nini?
Mamluki ni shughuli ambayo kwa muda mrefu imekuwa kwenye sehemu ya historia ya migogoro inayohusisha ya silaha. Baadhi ya wapiganaji wakati mwingine hukimbilia huduma za kulipwa kutoka upande mmoja wa wapiganaji wanaoshiriki katika mgogoro ama mapigano.
`` Vita na mamluki vimekuwa vikienda sambamba kila mara kwa kuwa vita vinatafuta faida zaidi,'' alisema kanali mstaafu wa jeshi la Senegal Mamadou Adje.
Kwa mujibu wa Kanali huyo, "mamluki ni yule anayekwenda katika eneo la kigeni kujihusisha na vita, mtu ambaye sio mshiriki wala hausiki na mzozo ama vita hiyo.
Anazimwa kupigana vita hiyo isiyomuhusu kwa ahadi ya kulipwa pesa kutokana na uwezo ama talanta zake vitani.
Umoja wa Afrika (OAU) unatafsiri mamluki ni"mtu yeyote:
- Ambaye ameajiriwa mahsusi nchini au nje ya nchi kupigana katika mzozo unahohusisha silaha;
- Ambaye anashiriki moja kwa moja katika uhasama;
- Ambaye anashiriki katika uhasama kwa nia ya kupata manufaa yake binafsi(malipo)
- Ambaye si raia wa upande wowote wa mzozo wala mkazi wa eneo linalodhibitiwa na Mshirika wa mgogoro;
- Aambaye si mwanachama wa jeshi la Chama kwenye mzozo; na ambaye hajatumwa na nchi nyingine isipokuwa mshirika mmoja kwenye mzozo kwa misheni rasmi kama mwanachama wa jeshi la taifa husika ama kundi husika"

Chanzo cha picha, Mamadou
Je mamluki ni halali?
Sheria ya kimataifa kuhusu masuala ya kibinadamu ni moja ya sheria zinazosimamia uhusiano kati ya wapiganaji wa mzozo unaohusisha silaha.
Hatupigani vita tena kama hapo awali, hatufanyi tena tunachotaka katika vita. Hii inasaidia kuunda uwanja wa vita kidogo,'' anaelezea Kanali Adje, aliyewasiliana na wahariri wa BBC Afrika.
Baada ya Vita vya pili vya dunia, kulikuwa na mkutano wa Geneva. Ni Mkataba wa Geneva ambao ulifafanua nani ni askari. Ili kupigana vita, lazima uwe mwanajeshi, na kama wewe si mwanajeshi, wewe ni mpiganaji. Mpiganaji ni yule aliye katika uwanja wa vita akiwa amevaa sare, na ambaye amevaa beji ya kipekee, ambaye ni wa muundo unaotambuliwa na ambaye anafanya hivyo kwa mujibu wa sheria za vita. Kando na hayo, wewe si mpiganaji,'' alisema kanali huyo.
Ufafanuzi ambao, kwa mujibu wa Kanali huyo, hauzingatii mamluki. Hawashiriki katika mzozo ingawa wapo kwenye uwanja wa vita.
Kwa kuongezea Dkt Boubacar Ndiaye anasema; ''mamluki huyo halindwi na sheria za kimataifa iwapo atakamatwa kama mateka ama mfungwa wa kivita. Hawana hadhi ya upiganaji kama inavyofafanuliwa na mikataba ya kimataifa juu ya migogoro ama ya silaha ama vita vinavyohusisha silaha. ''
Aidha, sheria ya kimataifa inakataza matumizi ya mamluki katika migogoro ya silaha. Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa mwaka 1889 pia unapinga kuajiri, kutumia, kufadhili na mafunzo ya mamluki.
Je, historia ya matumizi ya mamluki barani Afrika ikoje?

Chanzo cha picha, Getty Images
Barani Afrika, baada ya uhuru kwa mataifa kadhaa ilikuwa ni kipindi cha kutokuwa na utulivu. Baadhi ya mataifa yamelazimika kukabiliana na harakati za ukombozi.
Mataifa ya Afrika yalikuwa yakikabiliwa na vuguvugu la ukombozi, mataifa hayakuweza kukabiliana na matatizo yaliyoletwa na vyama hivi vya ukombozi.
Majeshi ya kitaifa hayakuwa na uwezo wa kupinga harakati hizi za ukombozi. Kwa hiyo tulitoa wito kwa askari kutoka nje kuimarisha uwezo wa ulinzi, hata kama ni kinyume cha sheria. Kwa hivyo tangu uhuru hadi 1973, walitawala sana Afrika.
Bob Denard (mamluki maarufu wa Ufaransa) alikuwa kila mahali, alikuwa Katanga, Comoro n.k. Mataifa makubwa (Ufaransa) nayo yaliwatumia kuyumbisha nchi bila kuwatambua watu hawa. Walikuwa nadra lakini walikuwa hitaji la ulinzi,'' anasema Kanali Adje.
Unaona yaliyotokea Afghanistan, Sahel n.k. Majeshi mengine yameshindwa, na jeshi lako linaposhindwa, unatafuta njia za kuliimarisha. Tunapinga uvunjani wa sheria lakini ni muhimu kuimarisha uwezo wake wa ulinzi. Hatuwezi kuzuia taifa kufanya maamuzi ya kuimarisha uwezo wake wa ulinzi,'' aliongeza afisa mkuu wa zamani wa jeshi la Senegal, Adje













