Mwanaume aliyejitenga porini kwa miaka 40

The Hermit of Treig Ken Smith

Chanzo cha picha, Uruna Productions

Maelezo ya picha, Ken anasema uvuvi ndio msingi wa uhuru wa maisha
Iliyochapishwa

Takribani miaka 40, Ken Smith ameamua kuishi bila huduma ya umeme au maji ya bomba katika kibanda chake ambacho amekitengeneza katika mkondo wa maji katika maeneo ya nyanda za juu za Uskoti

"Ni maisha mazuri," anasema Ken. "Kila mtu anayatamani ila hakuna anayejaribu kuyaishi."

Si kila mtu atakubaliana kuwa mtindo wa maisha ya kujitenga ya Ken, yanayojumuisha kuvua samaki, kukusanya kuni na kufua nguo zake ndio bora zaidi. Haswa kwa mtu ambaye ana umri wa miaka 74.

Nyumba yake aliyojenga kwa magogo iko umbali wa saa mbili kutoka barabara iliyo karibu zaidi kwenye ukingo wa Rannoch Moor, Loch Treig.

"Inajulikana kama eneo la upweke," anasema. "Hakuna barabara hapa lakini walikuwa wakiishi hapa kabla ya kujenga bwawa."

Akiangalia makazi yake akiwa mlimani anasema : "Magofu yote yako chini kule. Alama iliyobaki ni moja tu na ni yeye."

Mtengeneza filamu Lizzie McKenzie aliwasiliana mara ya kwanza na Ken miaka mitano iliyopita na kuthibitisha miaka miwili iliyopita kuwa anaweza kumpiga picha.

Ken, ambaye asili yake ni kutoka Derbyshire, anasimulia katika kipindi namna ambavyo alianza kufanya kazi akiwa na miaka 15, akijenga vituo vya zima mote.

Lakini maisha yake yalibadilika alipofika umri wa miaka 26 alipopigwa na kundi la wahuni nyakati za usiku.

Alipata matatizo katika ubongo na kupoteza fahamu kwa kipindi cha siku 23.

The Hermit of Treig Ken Smith

Chanzo cha picha, Uruna Productions

Maelezo ya picha, Ken Smith ameishi mwenyewe kwenye kibanda chake kwa kipindi cha miaka 40

"Walisema nisingeweza kupona tena. Walisema sitaongea tena," anasema.

"Walisema sitatembea tena lakini natembea sasa.

"Hapo ndipo nilipoamua kuamua kuishi maisha yangu bila kufuata masharti ya yeyote bali yangu mwenyewe," alisema.

Ken alianza kusafiri na akavutiwa kukaa porini.

Huko he Yukon, eneo la Canada lililopo mpaka wa Alaska, alikuwa anajitafakari nini kitatokea kama ataenda kuishi nyanda za juu .

Na hicho ndicho alichofanya , aliweza kutembea maili 22,000 kabla ya kurudi nyumbani.

Wakati alipoondoka, wazazi wake walifariki na alikuja kupata taarifa mpaka wakati aliporudi nyumbani.

"Ilinichukua muda kuwa mimi si kitu tena," alisema.

One of the many photographs Ken has taken over the years

Chanzo cha picha, Ken Smith

Ken alitembea kwa umbali mrefu nchini Uingereza na alikuwa Rannoch nyanda za juu za Scottish wakati ambao aliwafikiria wazazi wake na kuanza kulia.

"Nilikuwa nalia huku ninatembea," alisema.

"Niliwaza eneo ambalo limetengwa zaidi nchini Uingereza?" Ken alisema kwenye makala.

"Nilizunguka maeneo kadhaa ya ufukwe na eneo ambao lilikuwa halijajengw nyumba yeyote.

"Mamia na mamia ya maili ambayo hakuna kitu. na kufanikiwa kupata eneo hili la pori."

Anajua alipata eneo ambalo alikuwa anataka kukaa.

Ken anasema huo ndio wakati ambao aliamua kuacha kulia na kuacha kutembea tena.

Alijenga nyumba au kibanda kwa kutumia magogo ingawa mwanzoni alijaribu kubuni kwa kutumia fimbo ndogo ndogo.

Ken with his log cabin soon after it was built in the early 1980s

Chanzo cha picha, Ken Smith

Maelezo ya picha, Ken akiwa katika kibanda chake mnamo miaka ya 1980

Miongo minne, ameishi katika nyumba yake hiyo ya magogo akiwa hana umeme, gesi wala maji ya bomba -na wala mawasiliano ya simu.

Kuni za kupikia alikuwa akizifuata porini na kurudi katika makazi yake yaliyokuwa mbali.

Aliotesha mbogamboga na matunda ambavyo ndio vilikuwa vyakula vyake vikuu.

"Kama unataka kuishi maisha ya uhuru jambo unalopaswa kufanya ni kujifunza kuvua samaki," alisema.

Siku kumi baada ya muongoza filamu Lizzie kuondoka katika makazi ya Ken, mwezi Februari 2019, Ken aliyekuwa amejitenga alirudishwa nyumbani baada ya kupooza kutokana na athari za kukaa nje kwenye barafu.

Alitumia GPS ili kujua eneo alipo , ambayo alikuwa amepewa siku zilizopita, ambayo ilituma majibu moja kwa moja kwenye kituo cha kilichopo huko Houston, Texas.

Ilitoa taarifa kwa walinzi wa pwani nchini Uingereza na Ken alisafirishwa kwa ndege hadi hospitali ya Fort William ambapo alitumia wiki saba kupata nafuu.

Wafanyakazi walifanya kila wawezalo kuhakikisha anarudi kuishi kwa kujitegemea na madaktari walijaribu kumrudisha kwenye ustaarabu ambao angekuwa na watu wa kumuangalia. Lakini Ken alitaka tu kurudi kwenye kibanda chake.

The Hermit of Treig Ken Smith

Chanzo cha picha, Uruna Productions

Hata hivyo, alipata "maono mara mbili" baada ya kuugua kiharusi na kupoteza kumbukumbu yake inamaanisha Ken amelazimika kukubali msaada zaidi kuliko alivyokuwa hapo awali.

Mhusika mkuu wa eneo hilo, ambaye anatunza msitu anakoishi Ken, amekuwa akimletea chakula kila baada ya wiki kadhaa, ambacho analipa kutoka kwa pensheni yake.

"Siku hizi wamekuwa wakarimu sana kwangu ," Ken alisema.

Mwaka mmoja baada ya kuokolewa , Ken aliondolewa tena baada ya kuumia wakati jengo lake la mbao lilipomdondokea.

Lakini alisema anahofia maisha yake ya baadae.

"Hatuishi duniani milele," Ken anasema.

"Nitabaki hapa hadi siku zangu za mwisho zifike."

"Nimekuwa na matukio mengi lakini inaonekana nimenusurika yote.

"Ninalazimika kuugua tena wakati fulani. Kitu kitatokea kwangu ambacho kitaniondoa siku moja kama ilivyo kwa kila mtu mwingine.

"Lakini nna matumaini nitafika miaka 102."