Nchi 5 zinazofanya maisha kuwa rahisi kwa kutumia teknolojia

Iliyochapishwa

Njia mpya za mawasiliano zimetengeza utamaduni mpya duniani, katika maeneo mengi sasa imekuwa ni ngumu kutenganisha maisha ya kidijitali na maisha ya kila siku ya kawaida.

Kasi ya juu ya mtandao, simu na malipo mtandaoni bila kutumia pesa taslimu vinaendesha uchumi wa dunia kwa sasa.

Nchi nyingi zimekubaliana na ukuaji huu wa teknojia wa siku zijazo kwa kuongeza huduma za mtandao na namna ya kuzipata kwa urahisi. Sasa unajua ni nchi gani zipo mstari wa mbele kwa kuunganisha kizazi kijacho katika masuala ya Kidigitali? Shirika la Global Community Network Internationals limetoa repoti kuhusiana na maisha ya kidigitali inayoitwa "Digital Life Abroad".

Ripoti hiyo iliyoangalia uzoefu wa wataalamu ambao sio wazawa wa nchi husika, inaonesha mahali ambapo huduma za malipo ya serikali mtandaoni zinapatikana kwa wepesi, urahisi wa kupata namba ya simu, malipo ya mtandaoni bila kutumia pesa taslimu na urahisi wa kupata mtandao wa internet wa kasi na bila malipo. Orodha ya nchizilizotajwa na ripoti hiyo ni hii hapa;

1: Estonia

Estonia inashika nafasi ya kwanza katika orodha ya kimataifa. Hakuna kizuizi katika masuala ya mtandao na huduma za serikali zinapatika mtandaoni nchini humo.

Tangu ilipopata uhuru kutoka umoja wa Kisovient mwaka 1991, imewekeza kiasi kikubwa katika miundombinu ya kidigitali. Upigaji kura wa kieletroniki, Afya na huduma za benki za kieletroniki zilianzishwa chini ya mpango wa kieletroniki wa serikali e- Estonia

Lakini pia kuna huduma za ukaazi za kieletroniki kwa kuwaunganisha raia ambao sio wazawa wa nchi hiyo kupata huduma ya utambulisho, huduma za kibenki na kufanya malipo na kufungua kampuni.

Mpango huo unavutia wasafiri wa kidigitali na wafanyabiahara wa kigeni wanaotaka kufungua kampuni katika umoja wa ulaya na kutengeneza fursa mpya za uchumi wa Estonia.

Alexandra Nima ni mjasiriamali wa Austria anayeishi katika mji mkuu wa Tallinn anasema kuwa Mtandao wa internet ni kama haki ya msingi kwa binadamu katika nchi hiyo, hata katika visiwa vya mbali vya Estonia vinapata internet,"kila kitu kuanzia kujiandikisha kama mkazi hadi kufungua kampuni vipo mtandaoni na ni ya haraka iwezekanavyo.

Hata hivyo kutegemea sana miundombinu ya kigitali pia kuna athari, Estonia ndio nchi ya kwanza kupata shambulizi la mtandaoni mwaka 2007.

Dave Phillips alikuwa balozi wa Marekani nchini Estonia wakati wa shambulizi hilo la mtandao anasema, shambulizi lilizima tovuti na kusimamisha shughuli zote za internet, kadi za benki na mitandao wa simu za mkononi ilikwama.

Baada ya shambulizi hilo la mtandao, NATO ilitengeneza mwongozo wa kushughulikia mashambulio kama hayo na Estonia ilipendekeza Ulinzi bora wa Mtandao wa NATO ili kuzuia mashambulio yajayo.

Finland

Finland Ni ya pili katika maisha ya kidijitali na ya kwanza kwa malipo mtandaoni bila kutumia pesa taslimu mkononi. Mnamo mwaka 2010, serikali ilifanya kuwa ni haki ya kisheria kwa raia wote kuunganishwa na internet ya kasi (broadband). Finland ndio nchi ya kwanza kufanya hivyo.

Heiki Vanenen, Mkurugenzi Mtendaji na mwanzilishi wa jukwaa la maoni ya wateja HappyOrNot, anasema Intaneti ya haraka na uhuru wa kujieleza umefanya mfumo wao wa ikolojia kuwa endelevu na salama. "Kila mtu anauwezo wa kupata habari, Inatoa fursa sawa kwa wote kujifunza na kushawishi mustakabali wa nchi wa baadae"

Mwandishi na mwanzilishi wa blogu ya 'Finland My Home kutoka Scotland na ameishi katika mji wa Helsinki kwa miaka 8 Peter Sinen anasema upatikanaji wa huduma za serikalini katika mtandao ni muhimu sana kwa wahamiaji wapya".

Sinan anasema kuwa maisha ya kidijitali yanamaanisha kuwa kila kitu kinaendeshwa na kompyuta na teknolojia, kama vile malipo katika maduka makubwa. Pia anapendekeza huduma za mtandaoni ziwe katika lugha ya Kiingereza ili kumruhusu kufanya kazi za kila siku bila kujifunza au kuelewa lugha ya Kifini.

"Kuna habari nyingi kwenye mtandao nchini Finland kwa lugha ya Kiingereza kuanzia kuweka nafasi ya kumuona daktari hadi kuelewa haki kama mfanyakazi, Mengi yamebadilika tangu nilipohamia hapa kama mwanafunzi mwaka wa 2004."

Shirika la Afya Duniani (WHO) hivi majuzi liliiorodhesha Finland kuwa moja ya nchi zenye afya bora zaidi. Zaidi ya nusu ya watu kati ya umri wa miaka 30 na 64 hufanya mazoezi mepesi kwa dakika 150 au dakika 70 za mazoezi ya nguvu kwa wiki.

Israel

Israel inashika nafasi ya tatu katika Nyanja ya upatikanaji wa internet isiyo thibitiwa na rahisi kupata namba ya mtandao ya ndani. Ina kituo cha teknolojia chenye nguvu na cha juu. Raia wa wamekubali kwa furaha jina la utani la nchi hiyo "Start-up Nation" na wachache wako mbali na programu za kijamii na mawasiliano.

Maria Pinellis, mkazi wa Israel na balozi wa Kimataifa anasema wazee pia wana simu janja (Smartphones) Wanatumia muda kwenye Facebook au kutuma ujumbe kwenye WhatsApp au kuzungumza kwa njia ya video kwenye Messenger.

Rafael Hope Mkurugenzi Mtendaji na mwanzilishi mwenza wa biashara ya habari mtandaoni Amen V'Amen, anasema unaweza kuona wanawake wenye umri wa miaka 70 wakipiga simu za video kwa wajukuu zao wanaoishi Amerika au mahali pengine."

Anasema kwamba mtandao hapa ni wa haraka, nafuu na wa kuaminika unasaidia wajasiriamali wapya na wpenzi wa masuala ya kidijitali. "Mimi binafsi hufanya kazi zangu nyingi nikiwa nyumbani au kwenye mgahawa wa kahawa."

Anasema Maduka mengi ya kahawa yanatoa Wi-Fi ya bure, Watoa huduma za mtandao wa ndani katika maeneo mengi ya miji mikuu pia hutoa Wi-Fi ya bure kwa wateja wao. Wale wanaotaka kuanzisha biashara kwa kawaida huelekea Tel Aviv, inayojulikana kama jiji ambalo halilali kamwe.

Canada

Canada imekuwa na alama nzuri katika kila Nyanja ya kidijitali, hasa katika upatikanaji wa huduma za serikali mtandaoni na malipo ya mtandaoni yasiyo tumia na pesa taslimu.

"Miji mikubwa kama Toronto inafaa zaidi kwa maisha ya kidijitali Eric Wichopen mwandishi katika ukurasa wa Penguin & Pia anasema Katika miji mikubwa, teknolojia imekubalika na huduma za mtandao ni za haraka, hivyo kasi ya maisha ya digitali pia ni ya haraka.

Maduka madogo na mapya yanatumia njia mpya za malipo ikiwemo malipo kwa njia ya simu. Kuunganishwa katika mtandao nchini Kanada ni ghali zaidi kuliko nchi zingine, lakini sekta ya mawasiliano ya simu iko katikati na hakuna huduma ya jumla katika maeneo ya mbali.

Kwa ujumla upatikanaji wa huduma za serikali mtandaoni unatajwa kuwa namba 8 na upatikanaji wa huduma za mtandaoni umeorodheshwa namba 11 hovyo kuwapa wajasiriamali fursa, urahisi wa kuanzisha, na kuendesha biashara kutoka popote.

Korea Kusini

Korea Kusini ni namba moja kwa upatikanaji wa mtandao wa kasi majumbani. Pia imefanya maisha ya watu kuwa ya haraka zaidi. Choi Ye Yoon, mkazi wa Seoul anasema kuwa Maisha ya kila siku nchini Korea Kusini ni ya haraka. Kuagiza chakula, kuletewa na kulipa hufanyika ndani ya muda mchache.

Choi anasema anapenda huduma ya benki ya Kakao, ambayo inaunganisha huduma zake za kidijitali na programu ya Messenger. Kasi ya mtandao nchini Korea Kusini ndiyo yenye kasi zaidi duniani iwe katika masuala ya burudani kama vile game hadi kuangalia video mtandaoni ni vya kasi.

Anasema huwezi kuchoka hata kwenye treni kwani wanaweza kupata huduma za instagram au Youtube. Lee Namu (Martin), mkazi wa Seoul anakubalina juu ya kasi ya internet nchini korea kusini na kueleza kuwa inaweza ikashangaza dunia kwa kasi yake kwani hakuna kinachozuia.

Kulinganisha na nchi jirani kama China na North Korea, serikali ya korea kusini imeweka huduma za internet bure bila malipo yoyote na kutokana na hilo raia wamekuwa na ushiriki mkubwa katika matatizo ya kijamiidi.