Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Lyudmila Pavlichenko : Mlenga shabaha aliyeogopwa na Hitler na Jeshi lake
Simulizi hii inahusu msichana ambaye ana hadhi ya mpiga risasi ama mlenga shabaha hatari zaidi katika historia na ambaye alikabiliana na jeshi la Nazi la Hitler. Akiwa na umri wa miaka 25 tu, Lyudmila alikuwa ameua watu 309, wengi wao wakiwa wanajeshi wa Hitler.
Wakati Vita vya pili vya dunia vilikuwa vikiendelea, Lyudmila Pavlichenko aliwasili Washington mnamo 1942, ingawa wataalam wengi wanaamini kwamba Umoja wa Kisovieti ulitumia suala la Lyudmila kwa minajili ya propaganda. Alitumwa kwenda hata Marekani na Mamlaka za juu za Soviet.
Madhumuni ya kwenda huko ni kupata uungwaji mkono wa Marekani kwenye uwanja wa vita huko Ulaya Magharibi (Western Front.)
Joseph Stalin alitaka majeshi ya Washirika kuivamia Ulaya na pia alikuwa na hamu ya hilo.
Safari ya Marekani
Stalin alitaka kuweka shinikizo kwa Wajerumani kugawanya vikosi vyao ili shinikizo kutoka upande wao ama nguzu zao za jeshi la Soviet lipunguzwe. Kusudi hili la Stalin halikutimizwa hadi miaka mitatu baadaye. Kupitia misheni hii, Pavlichenko aliingia Ikulu. Alikuwa mtu wa kwanza kutoka Soviet kufanya hivyo, ambayo ilipokelewa na Rais Franklin Roosevelt.
Lyudmila Pavlichenko alisafiri nchi nzima na mke wa Rais Roosevelt Eleanor Roosevelt. Wakati huu, alipata fursa na uzoefu wake wa kujiunga na vita kama mwanamke na Wamarekani.
Kujiunga na Chama cha Walenga Shabaha
Katika umri mdogo wa miaka 14, Lyudmila Pavlichenko alilelewa huko Kiev katika maisha yaliyozungwa na silaha. Alikuwa ameishi na familia yake huko Ukraine kutoka kijijini kwao huko Kiev. Kwa mujibu wa kitabu cha Henry Sakada 'Heroines of the Soviet Union', Pavlichenko alifanya kazi katika kiwanda cha silaha.
Akaamua kujiunga na Chama cha walenga shabaha cha Osoawiajim kujifunza namna ya kutumia silaha. Wakati wa ziara ya Marekani, Pavlichenko alisema, "Wakati mvulana anayeishi katika mtaa wangu alipokuwa akijivunia kupiga risasi, ndipo niliona kumbe msichana anaweza kufanya hivyo pia. Kwa hili nilifanya mazoezi kwa bidii."
Ndani ya siku chache, Pavlichenko alijua matumizi ya silaha. Mnamo Juni 22, 1941, Ujerumani ilianzisha Operesheni Barbarossa. Chini ya operesheni hii, Ujerumani iliivamia Umoja wa Soviet.
Mafunzo ya kijeshi
Lyudmila Pavlichenko aliamua kuacha masomo ya historia katika Chuo Kikuu cha Kiev na kujiunga na jeshi ili kutetea nchi yake. Mwanzoni alikataliwa katika jeshi.Lakini alipoonyesha ustadi wake katika upigaji risasi, askari wa jeshi walimpa nafasi ya kuangaliwa kwanza. Katika kitabu chake kuhusu walenga shabaha ama wapiga risasi kiitwacho 'Sniper in Action', Charles Strong alimnukuu Pavlichenko akisema, "Nilichukua mafunzo ya msingi ya kijeshi katika shule ya Kiev, ambapo nilishinda beji katika mashindano ya kanda."
Katika ukaguzi huo ama kuona uwezo wake, Pavlichenko alipewa bunduki na kutakiwa kuwapiga risasi askari wawili wa Kirumi wanaofanya kazi Ujerumani.
Pavlichenko alilenga shabaha vizuri tena kwa urahisi. Hilo lilimfanya aingie katika Kitengo cha Fusiliers cha Chapayev mnamo 25.
Wanazi waliokufa walikuwa hawana madhara'
Akiwa jeshini, alishiriki katika vita huko Ugiriki na Moldova. Aliua wanajeshi 187 wa Wanazi katika siku 75 za kwanza za vita. Baada ya kufanya vizuri katika vita huko Odessa, kusini mwa Ukrane ya leo, alitumwa Crimea kupigana Vita vya Sevastopol.Ilikuwa Oktoba 30, 1941 hadi Julai 4,1942
Alipata majeraha kadhaa kwenye Vita vya Sevastopol, lakini hakuondoka kwenye uwanja wa vita hadi jeshi la Nazi lilipomjeruhi na kupata majeraha makubwa usoni. Kwa sababu ya mafanikio mengi kwenye masuala ya kijeshi, alipandishwa cheo na kuwa luteni na akaanza kuwafunza watu wengine kupiga risasi ama kulenga shabaha. Siku chache baadaye alitumwa Washington.
Wakati wa ziara yake Marekani, alisema, "Kila Mjerumani anayeishi ataua wanawake, watoto na wazee. Ndiyo maana ninaokoa maisha ya watu wengi kwa kuua Wanazi."
Shujaa wa Umoja wa Soviet
Kurudi kwa Umoja wa Kisovieti, Pavlichenko pia alikwenda Uingereza kupata uungwaji mkono mwingine. Baada ya kutunukiwa tuzo ya heshima ya juu ya Vita na shujaa wa Umoja wa Kisovieti, alimaliza mafunzo yake katika Chuo Kikuu cha Kiev na kuanza kazi yake kama mwanahistoria.
Kuanzia 1945 hadi 1953, alifanya kazi na makao makuu ya Jeshi la Wanamaji la Soviet na baadaye kuwa mshiriki hai wa Kamati ya Soviet ya Mashujaa wa Vita. Alikuwa mmoja wa wapiganaji 2,000 waliopigana na Jeshi Nyekundu katika Vita vya pili vya dunai na alikuwa mmoja wa wapiganaji 500 walionusurika vita.
Lakini majeraha yake hayakupona. Alikufa tarehe 10 Oktoba 1974 akiwa na umri wa miaka 58.
Maswali mengi yaibuka kuhusu hadhi yake
Maswali mengi yalizuka juu ya historia yake. Lyuba Vinogradova aliibua maswali kama hayo katika kitabu chake "Aveging Angels".
Alihoji ukweli kwamba Lyudmila Pavlichenko ndiye aliyehusika na vifo vingi, aliandika katika kitabu hicho, "Aliua maadui 187, lakini cha ajabu ni kwamba hakupata medali yoyote huko Odessa."
"Kwa kila maadui 10 wanaouawa au kujeruhiwa, walenga shabaha hutunukiwa nishani ya heshima. Ikiwa umeua maadui 75 inatosha kutunukiwa jina la 'Shujaa wa Umoja wa Kisovieti', sasa kwa nini hajatambulika kwa hilo? Kwa nini hawajampa chochote?"