COP26 : ‘Tulipeni au mfe pamoja nasi’-ujumbe wa rais wa Malawi kwa nchi tajiri

Iliyochapishwa

Rais wa Malawi ana ujumbe mzito kwa mataifa tajiri, yaliyoendelea ambayo bado hayajatimiza ahadi ya kulipa £100bn kwa nchi maskini kila mwaka ili kukabiliana na mabadiliko ya hali ya mabadiliko ya tabia nchi

"Si kitendo cha hisani. Kwa hivyo lipeni au muangamie pamoja nasi," Lazarus Chakwera aliambia BBC Africa.

Muda mrefu uliopita kama 2009, nchi zilizoendelea ziliahidi kwamba zitakusanya fedha hizo hiyo ifikapo 2020 ili kusaidia nchi ambazo hazijaendelea kukabiliana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa na kujenga uchumi wa kijani.

Lakini lengo hili bado halijafikiwa na serikali ya Uingereza, ambayo ni mwenyeji wa mkutano huu, sasa inasema kuna uwezekano fedha hizo hazitatolewa hadi mwaka wa 2023.

Kwa nchi nyingi, hili ndilo suala kubwa zaidi kusuluhisha - na maskini zaidi wanadai hatua katika mkutano wa Glasgow. Wanasema wale ambao wana jukumu la kihistoria la mabadiliko ya hali tabia nchi wanapaswa kulipa zaidi ili kukabiliana nayo.

Chakwera anasema: "Tunaposema timiza ahadi yako, si swala la hisani, ni kulipa ada ya kusafisha. Ikiwa umehusika kuleta ardhi tunaiita nyumbani katika hali hii, tuisafishe; lakini lazima uwajibike."

Mkutano waanza

Wageni toka nchi 200 Ulimwenguni kote wataazimia kwa pamoja mpango wa 2030 kuisaidia Dunia na majanga ya tabia nchi.

Kutokana na ongezeko la joto Duniani na shughuli za uuzaji wa mafuta, wanasayansi wanaonya kwamba hatua za haraka zinahitajika ili kuepuka janga la mabadiliko ya tabia ya nchi.

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson mkutano huu ndio utakaotoa muelekeo wa nini kifanyike Duniani

Akizungumza kabla ya kongamano wiki mbili kabla, aliwataka viongozi kuutumia vyema: "Swali ambalo kila mtu anauliza ni iwapo tutaafiki kwa pamoja au tuache kulishughulikia mapema."

Siku ya kwanza kutakuwa na usomaji wa taarifa ya ripoti ya mabadiliko ya tabia nchi iliyotolewa na Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO).

Ripoti ya muda ya WMO ya wanasayansi wa hali ya hewa italinganisha viwango vya joto duniani mwaka huu na miaka iliyopita.

Matukio makubwa ya hali ya hewa yanayohusishwa na mabadiliko ya tabia nchi - ikiwa ni pamoja na mawimbi ya joto, mafuriko na moto unaoukumba misitu kuongezeka.

Rekodi zimeonyesha kuwa muongo uliopita ulikuwa wa joto zaidi jambo lililohitaji zaidi hatua za haraka na pamoja.

Mkutano wa Umoja wa Mataifa ni moja ya mikutano mikubwa zaidi ambayo Uingereza imewahi kuandaa, na ilicheleweshwa kwa mwaka mmoja kwa sababu ya janga hilo. COP inasimamia 'mkutano wa nchi wanachama' na ni mkutano wa 26.

Viongozi wengi watawasili leo Jumapili jioni. Wengi wanasafiri kutoka mkutano mwingine wa G20, huko Roma.

Jumapili kwa kiasi kikubwa ni siku ya ufunguzi wa mkutano huo, na hotuba mbalimbali kutoka kwa watu akiwemo Abdulla Shahid, rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Maldives.

Visiwa vya chini vya Maldives vinatishiwa na mabadiliko ya hali ya hewa kwa sababu ya kuongezeka kwa viwango vya bahari.

Nchi zote wanachama duniani zitakuwa na wawakilishi mjini Glasgow, tayari kujadili mipango yao ya kupunguza hewa chafu ifikapo 2030.