Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Wakati nyoka aina ya 'Cobra' alipotumiwa kama silaha ya kuua nchini India
Wiki iliyopita mwanaume mmoja nchini India alihukumiwa vifungo viwili vya maisha jela kwa kumuua mkewe kwa kufanya nyoka aina ya cobra amuume.
Mwezi Aprili mwaka uliipita Suraj Kumar mwenye umri wa miaka 28 alilipa dola 92 kumnunua nyoka aina ya cobra mmoja wa nyoka wenye sumu kali zaidi duniani.
Biashara ya kununua na kuuza nyoka ni haramu nchini India kwa hivyo Suraj alimnunua nyoka huyo kutoka kwa mshika nyoka Suresh Kumar kusini kwa jimbo la Kerala.
Suraj akatoboa shimo kwa chombo cha plastiki ili hewa ipate kuingia, akamweka yule nyoka kwenye chombo kile na kisha akampleka nyumbani.
Siku 13 baadaye, akaweka kile chombo kwenye mfuko na kuelekea nyumbani kwa wakwe zake karibu umbali wa kilomita 44 ambapo mke wake Uthra alikuwa akipata nafuu baada ya kumwa na nyoka kwa njia isiyoeleweka.
Suraj na Uthra walikuwa wamekutana miaka miwili kupitia huduma za mpatanishi.
Uthra ambaye alikuwa mdogo kiumri kwa Suraj kwa miaka mitatu, alikumbwa na umelamavu wa kujifunza mambo, alitoka familia iliyokuwa inajiweza kidogo - baba yake alikuwa mfanyabiashara na mama yake alikuwa mwalimu mkuu wa shule mstaafu.
Wakati wawili hao waliofunga ndoa Suraj alikubali mahari kutoka kwa wazazi wa Uthra ambayo ni gramu 768 za dhahabu za thamani ya karibu dola 32,000 kwa thamani ya sasa, gari aina ya Suzuki sedan na rupee 400,000 pesa taslimu. Pia alipokea rupee 8,000 kila mwezi kutoka kwa wazazi wa mke wake kutumia kumtunza binti yao, kwa mujibu wa wachunguzi.
Ni kwa wazazi wake Uthra alirejea baada ya kuondoka hospitalini alikotibiwa kwa kuuma na nyoka. Alikuwa amekaa hosptalini kwa siku 52 na alihitaji kufanywa upasuaji mara tatu kwenye mguu wake.
Alikuwa ameumwa na nyoka aina ya Russell's viper - nyoka mwenye sumu kali ambaye anatajwa kusababisha maelfu ya vifo nchini India kila mwaka.
Kisha usiku wa tarehe 6 Mei, wachunguzi wanasema wakati Uthra alikuwa bado anapata nafuu, alikubali glasi ya kinywaji cha matunda kutoka kwa Suraj yaliyokuwa na yamechangawa na dawa ya usingizi.
Wakati alipatwa na usingizi, Suraj alichomoa chombo alimokuwa cobra na kumrusha yule nyoka kwa mkewe aliyekuwa amelala.
Lakini badada ya yule nyoka kumvamia, alindoka. Suraj akamchukua na kumrudisha kwa Uthra tena lakini tena yule nyoka akaondoka.
Suraj akajaribu kwa mara ya tatu na kwa wakati huu akamshika karibu na kichwa na kuweka kile kichwa karibu na mkono wa kushoto wa mkewe Uthra. Nyoka huyo aliyekuwa amekasirika akamuuma Uthra mara mbili kisha akaondoka kuelekea sehemu moja ya chumba ambako alikaa usiku wote.
"Nyoka aina ya Cobra hawaumi hadi wanapochokozwa, Suraj huenda alimshika na kumlazimisha nyoka amuume mkewe." Alisema Mavish kumar, mtaalamu wa viumbe kama nyoka.
Suraj aliondoa kile kinywaji, akaharibu kijiti alichotumia kumuelekeza yule nyoka na kufuta rekodi za simu kwenye simu yake kwa mujibu wa wachunguzi.
Wakati mama yake Uthra aliingia chumbani asubuhi iliyofuata, aliwaambia polisi kuwa alimkuta bintiye amelala kitandani na mdomo wake ukiwa wazi, mkono wake ulikuwa unaning'inia upande mmoja. Akasema Suraj pia alikuwa chumbani humo.
Familia ilimkimbiza Uthra hospitalini ambapo madaktari walisema alikuwa tayari amekufa kwa sumu na kuwaita polisi.
Ripoti ya upasuaji ilipata majeraha mawili kwenye mkono wake wa kushoto, sampuli za damu zikaonyesha uwepo wa simu ya cobra na dawa za usingizi, sumu ya cobra inaweza kuuwa ndani ya masaa mawili.
Kutokana na malalamiko ya wazazi wa Uthra polisi walimkamata Suraj tarehe 24 Mei kufuatia kifo kisichokuwa cha kawadia cha mke wake. Baada ya uchunguzi wa siku 78 na mashataka ya karibu kurasa 1000 kesi ikaanza.
Zaidi ya watu 90 wakimemo wataalamu wa nyoka na madaktari walitoa ushahidi. Upande wa mashtaka ukaandaa kesi kwa kutumia rekodi za simu za Suraj, historia ya internet, cobra aliyekufa aliyefukuliwa nyuma ya nyumba, dawa za kulala kwenye gari la familia na ushahidi kuwa alinunua nyoka wawili.
Wachunguzi wanasena kuwa Suraj pia alikuwa amenunua nyoka aina wa Russell's viper aliyekuwa amemuuma Uthra miezi kadhaa kabla ya kifo chake.
Suresh, mshika nyoka alimgeuka Suraj na kukiri kuwa ndiye alimuuzia nyoka wote wawili.
Jaji Manoj alimhukumu Suraj kifungo cha maisha akisema alipanga kumuua Uthra na kufanya hali ionekane kama kifo cha kuumwa na cobra kwa bahati mbaya.
Kulingana na wachunguzi, jaribio hilo na kuua kwa kutumia cobra lilikuwa la tatu la Suraj la kutaka kumuua mkewe ndani ya miezi minne.
Suraj aliyekuwa akifanya kazi kama ajenti wa benki, alikutana na mshika nyoka Suresh mwezi Februari mwaka uliopita na kununua nyoka aina ya Russell's viper kutoka kwake kwa rupee 10,000.
Akampeleka nyoka huyo nyumbani kwa chombo cha plastiki na kumficha chini ya chungu la kuni nje ya myumba.
Tarehe 27 Suraj alimuachilia nyoka huyo kwenye chumba cha chini, na kisha kumuomba mkewe kwenda chumba cha juu kumletea siku yake, kulinngana na wachunguzi.
Uthra akamuona nyoka huyo sakafuni na kupiga mayowe, mama yake aliwaambia polisi. Suraj akaja akamchukua yule nyoka kwa kutumia kijiti, akaondoka nyumbani na kumrudisha kwa kile chombo.
Usiku wa tarehe 2 Machi, Suraj akajaribu tena. Akamwekea mkewe dawa za usingizi na kisha kumuachilia yule nyoka kwenye chumba cha kulala mkewe akiwa kwenye usingizi.
Wakati huu wachunguzi wanasema nyoka huyo alimshambulia. Uthra akaamka akipiga nduru kwa maumivu, alikuwa ameumwa mguuni, na Suraj akamtupa nje yule nyoka kupitia dirisha.
"Visa vya kuumwa na nyoka ni vingi Kerala, kwa hivyo hatukushuku kulikuwa na njama fulani hapa," alisema Vijayasenan Vidhyadharan, baba yake Uthra. (Karibu watu 60,000 hufariki kwa kuumwa na nyoka nchini India kila mwaka)
Ilichukua zaidi ya masaa mawili usiku huo kupata hospitali inayoweza kutibu hali kama hiyo. Uthra alikuwa amefura na pia alikuwa akifuja damu.
Akafanyiwa upasuaji mara tatu, akarudi kwa wazazi wake katika kijiji cha verdant huko Kollan kupumzika.
Suraj akabaki na mwanawe na wazazi nyumbani kwake huko Pathanamthitta. Lakini alikuwa tena akipanga njama nyingine.
"Mkewe akiwa hospitalini Suraj alikuwa akitafuta mitandaoni kuhusu namna ya kuwashika nyoka na kuhusu sumu ya nyoka," alisema Anoop Krishna, mmoja wa wachunguzi.
Wachunguzi wanasema Suraj alikuwa akipanga mauaji hayo tangu mwanawe Dhruv alipozaliwa mwaka 2019.
Historia yake mitandaoni ilifichua kuwa alitafuta nyoka wenye simu na kutazama video za nyoka kwenye YouTube.
Inaripotiwa kuwa Suraj aliwaambia marafiki zake kuwa mkewe alikuwa akisumbuliwa na laana ya nyoka ndotoni, ambapo aliota kuwa angekufa kwa kuumwa na nyoka.
Kwa kweli Suraj alikuwa na mpango wa kumuua mke wake, aibe pesa zake na amuoe mke mwingine, kwa mujibu wa wachunguzi.
"Akapanga na akafanikiwa kwa jaribio la tatu" alisema Apukuttan Ashok, afisa wa polisi mkuu wa uchunguzi.
Mwendesha mashtaka Mohanraj Gopalakrishnan alitaja kesi hiyo kama mafanikio makubwa katika uchunguzi wa polisi nchini India, ambapo waendesha mashtaka wanaweza kuonyesha kuwa mnyama alitumiwa kama silaha ya kuua.