Mahojiano ya Meghan na Harry: Mazungumzo ya dharura ya Ufalme yafanyika juu ya madai ya ubaguzi

Kikao cha dharura kinachowajumuisha maafisa wa ngazi ya juu wa Ufalme wa Uingereza kimefanyika kufuatia mahiojiano ya Mwanamfalme Harry na mkewe Meghan na Oprah Winfrey.
Mwandishi wa BBC wa masuala ya ufalme Daniela Relph amesema kasri la Ufalme -Buckingham Palace " halitataka kuhisi linaharakishwa katika kusema kitu chochote " kuhusu madai ya Mwanamfalme Harry na Meghan.
Mwanamfalme Harry na Meghan walizungumzia kuhusu ubaguzi wa rangi, afya ya akili, vyombo vya habari na mengine mengi katika mahojiano ya watu wa familia ya Ufalme.
Baba yake Meghan Thomas Markle amekosoa muda ambao mahojiano hayo yamefanyika.
Wawili hao wanaofahamika kama-The duchess - ambao ndio familia ya kwanza yenye mchanganyiko wa rangi-kizazi cha kisasa cha Familia ya Ufalme -wamesema kuwa kilichowasikitisha ni pale Harry alipoulizwa na mmoja wa watu wa familia ya Ufalme ambaye hakutajwa jina ''jinsi gani ngozi inavyoweza kuwa nyeusi " ya mtoto wao wa kiume Archie.
Mwanamfalme Harry baadaye alimthibitishia Oprah kwamba maoni hayo hayakutolewa na Malkia au mumewe Mfalme wa Edinbugh.
Wakati huohuo, msemaji wa rais wa Marekani Joe Biden amesema angemsifu mtu yeyote kwa kuwa na ujasili wa kuzungumzia wazi kuhusu afya ya akili.
Afisa wa mawasiliano wa Ikulu ya White House Jen Psaki alimuelezea Mwanamfalme Harry, 36, na Meghan, 39, kama "raia binafsi" ambao walikuwa "wanashirikisha Umma hadithi yao katika mapambano yao".

Chanzo cha picha, PA Media
Zaidi ya watu milioni 11 nchini Uingereza wameangalia mahojiano ya saa mbili wakati yalipotangazwa kwenye televisheni ya ITV nchini humo Jumatatu baada ya kutangazwa nchini Marekani na televisheini ya CBS Jumapili.
Katika mahojiano hayo, Bi Meghan alisema kuwa alibaini kuwa maisha ya Kifalme yalikuwa magumu sana na wakati mwingine ''hakutaka kuwa hai tena'', na alipowasiliana na taasisi hiyo ya Ufalme kwa ajili ya kupata msaada, hakuupata.
Kiongozi wa chama cha Sir Keir Starmer amesema kuwa madai ya Meghan ya ubaguzi wa rangi na ukosefu wa masula ya afya ya akili yanapaswa kuchukuliwa "kwa umuhimu sana".
Waziri Mkuu Boris Johnson alikataa kutoa maoni juu ya madai hayo, lakini akasema "kila mara amekuwa akimuhusudu kwa kiwango cha juu Malkia na kazi yake ya kuunganisha taifa ambayo amekuwa akiifanya ".
Alisema "inapokuja katika suala la Familia ya Ufalme, jambo linalofaa kwa mawaziri wakuu kufanya ni kutosema lolote", baada ya kuulizwa iwapo ana amini Familia ya Ufalme ina ubaguzi wa rangi.
Wakati wa mahojiano, Meghan au the duchess aliulizwa ni kwanini alifikiri Familia ya Ufalme haikumfanya mwanae Archie Mwanamfalme- jambo ambalo Meghan alilitaka ili aweze kupewa ulinzi wa polisi.
Meghan alisema alitaka iwe hivyo ilia pate ulinzi wa polisi.
"Katika miezi hiyo nilipokuwa mjamzito, wakati wote kwa hiyo tulikuwa katika mazungumzo ya jinsi ambavyo hatapewa usalama, hatapewa cheo, na pia hofu na mazungumzo kuhusu jinsi ngozi yake inavyoweza kuwa nyeusi atakapozaliwa ," alisema Meghan.
Alisema kauli juu ya rangi ya ngozi ilitolewa kwa Harry na Harry akaiwasilisha kwake.
Mtoto wa Harry na Meghan hawawi Wanamfalme moja kwa moja kutokana na sheria ambayo imekuwepo tangu mwaka 1917-isipokuwa tu Malkia aamue kuingilia kati na kuwatangaza kuchukua hadhi hizo.
'Kuharibu'
Alipoulizwa na Oprah iwapo kulikuwa na hofu kwamba mtoto wao angekuwa na ngozi ya "kahawia sana" na hilo lingeleta tatizo, Meghan alisema: "Kama hiyo ndio dhana yako , hilo ni salama kabisa ."
Aliposukumwa ajibu kwa ufasaha alichokimaanisha, alikataa kufichua maelezo zaidi juu ya mtu aliyesema ni nani, akisema: "Ninafikiria hiyo itawaharibu sana ."
Mwanamfalme Harry pia alikataa kutoa maelezo zaidi, akisema : "Mazungumzo yale, sitayashirikisha kamwe ."
"Wakati mwingine ilikuwa ni ujinga, Nilishituka kidogo," aliongeza.

Chanzo cha picha, MISAN HARRIMAN/THE DUKE AND DUCHESS OF SUSSEX
Mwanamfalme Prince Harry alisema hakuna yeyote miongoni mwa ndugu zake aliyezungumza wazi kumuunga mkono Meghan kuhusu vichwa vya habari na makala ya "ubaguzi wa rangi wa kikoloni " .
"Hakuna hata mmoja katika familia yangu aliyezungumza kamwe kwa kipindi cha miaka hiyo mitatu," alisema.
Wawili hao walihamia California Marekani baada ya kuondoka rasmi katika majukumu ya Ufalme mwezi Machi 2020, na ilitangazwa mwezi uliopita kwamba hawatarudi tena kufanya kazi kama watu wa Familia ya Kifalme .
Katika picha ambazo hazikujumuishwa katika mahojiano asilia, Mwanamfalme Harry alisema ubaguzi kutoka kwa magazeti ya habari ambayo yaliufikia jamii yalikuwa "kwa kiasi kikubwa" ya kwanini yeye na mke wake waliondoaka Uingereza.
Chama cha wahariri kilisema "haikubaliki" kudai baadhi ya magazeti yalimshambulia "bila kutoa ushahidi wa kuunga mkono" madai hayo.
Mbunge wa chama cha Labour Diane Abbott alisema anaweza kutoa mfano wa "taarifa baada ya taarifa wakati Meghan alipochukuliwa tofauti na wajumbe wengine wazungu wa familia ya ufalme ".
Bi Abbott alielezea athari ya kuzungumziwa katika magazeti aliyopata kama ya "kuumiza", akiongeza kuwa: "Ni ubaguzi na mwisho wake, inakufanya mwenyewe usijiamini ."

Mambo mengine muhimu yaliyofichuliwa katika mahojiano
• Wanandoa hao walitangaza mtoto wao wa pili, ambaye wanatarajia kumpata katika msimu wa kiangazi, ni msichana
• Walioana katika sherehe iliyoongozwa na Askofu wa Canterbury katika "makazi yao "siku tatu kabla ya kuoana kisheria katika harusi yao iliyofanyika mbele ya umma mwezi Mei 2018
• Mwanamfalme Harry alisema kuwa kaka yake na baba yake "walikwama ndani ya mfumo " wa Familia ya Ufalme
• Alisema familia yake ilisitisha msaada wa kifedha mwanzoni mwa mwaka jana na familia yake ikaacha kupokea simu zake
• Lakini mwanamfalme alisema anampenda kaka yake "sana" na anataka kuponya uhusiano kati yake na kaka na baba yake
Meghan alisema alimpigia Malkia wakati Mfalme Philip alipokwenda hospitalini mwezi uliopita
Katika maelezo zaidi, Meghana alimwambia Oprah alihisi kusalitiwa na mienendo ya baba yake Thomas Markle kabla ya harusi yake na Harry mwaka 2018
Bw Markle amekiambia kipindi cha ITV cha Good Morning Britain Jumanne kwamba mahojiano yalikuwa ya kwanza akimsikia binti yake akizungumza kwa mara ya kwanza baada ya miaka kadhaa
"Ninasikitishwa sana kuhusu mahojiano. Nimeomba msamaha kuhusu hiki kiti, kile kilichotokea, walau mara 100 au zaidi ," alisema
Aliyaelezea mahojiano kama "yaliyozidi kiwango" na ambayo yamekuja wakati mbaya, lakini akasema haamini Familia ya Ufalme ni wabaguzi wa rangi na kwamba maoni kuhusu rangi ya mwili ya Archie huenda lilikuwa "swali la kawaida ".
Alipoulizwa kuhusu madai ya Meghan kwamba alikuwa''amempoteza' baba yake, Bwana Markle alisema: "Nippo wakati wote tunaweza kukutana pamoja.Ningependa kukutana nae. Kusema kweli ningependa kumuona mjukuu wangu wa kiume."
Alikosoa pia usaidizi kutoka kwa Kasri wakati yeye na familia yake walipokuwa wakichunguzwa na vyombo vya habari, akisema kuwa: "Hakuna yeyote aliyekuwa pale kutujali, hakuna aliyetusaidia ."












