Ujenzi wa mji ulioganda kwa barafu nchini China
Tamasha la kimataifa la 37 la Harbin, China limefunguliwa kwa ajili ya wageni.

Chanzo cha picha, Shutterstock
Msimu wa mapumziko katika mji wa Harbin ulioko mashariki magharibi mwa jimbo la Heilongjiang, ambalo ni kubwa na la aina yake.
Mji huo wa theluji umetengenezwa michezo mbalimbali ya kwenye barafu.

Chanzo cha picha, Shutterstock
Kutokana na kuepo kwa marufuku ya kuingia nchini China kutokana na janga la virusi vya corona, watalii wa ndani wanatarajiwa kuziba pengo hilo.

Chanzo cha picha, Shutterstock

Chanzo cha picha, Getty Images

Chanzo cha picha, Shutterstock

Chanzo cha picha, Getty Images
Mji huu umeanza kuwa wa kitalii kuanzia mwaka 1963 na shughuli za kitamaduni za China zilivuruga shuguli za matamasha ya hapo na kuanza tena msimu wa kutembelea eneo hilo kuanzia mwaka 1985.

Chanzo cha picha, Getty Images

Chanzo cha picha, Shutterstock

Chanzo cha picha, Getty Images
Mwezi Desemba, wachimbaji wa barafu wapatao 300, wengi wao wakiwa wao wakiwa wafanyakazi na wakulima, walijenga jengo la kufanya tamasha katika eneo hilo.

Chanzo cha picha, Carlos Garcia Rawlins / Reuters

Chanzo cha picha, Carlos Garcia Rawlins / Reuters

Chanzo cha picha, Carlos Garcia Rawlins / Reuters
Kujengwa kwa mji wa barafu , makumi maelfu ya matofali yalitengenezwa kilomita chache kutokea kwenye mto uliokuwa na barafu wa Songhua, huko Harbin.

Chanzo cha picha, Carlos Garcia Rawlins / Reuters
Matofali hayo yalipelekwa katika eneo husika kwa kutumia gari, ambapo yalitumika kujengea daraja, migahawa na maeneo mengine ya mapumziko.

Chanzo cha picha, Carlos Garcia Rawlins / Reuters
Mchimbaji wa barafu ,Wang Qiusheng aliiambia Reuters sababu ya kutumia barafu kutoka kwenye mto ni kutokana na uzito na uimara wa matofali katika kukabiliana na upepo.
Wafanyakazi ambao walikuwa wanafanya ujenzi huo walikuwa wamevalia mavazi ya kuzia baridi mwili mzima, kuanzia kichwani, mikononi mpaka miguuni.

Chanzo cha picha, Carlos Garcia Rawlins / Reuters
"Tunafika hapa saa 12 asubuhi kila siku," Zhang Wei aliiambia Reuters.
"Mara nyngine tunafanya zaidi ya muda wa kazi tunajenga mpaka saa tatu usiku au saa sita usiku."
Matofali haya ya barafu yanajenga ukuta vizuri.

Chanzo cha picha, Carlos Garcia Rawlins / Reuters

Chanzo cha picha, Carlos Garcia Rawlins / Reuters

Chanzo cha picha, Carlos Garcia Rawlins / Reuters
Wakati wanafanya kazi hiyo, huwa wana muda wa mapumziko kwa ajili ya chakula cha mchana na wanaenda kwa awamu katika mgahawa ambao unawapa chakula kilichofungwa katika mifuko ya plastiki.

Chanzo cha picha, Carlos Garcia Rawlins / Reuters
Vilevile mji huo umewekwa taa za rangi mbalimbali.

Chanzo cha picha, Carlos Garcia Rawlins / Reuters
Tamasha la barafu la Harbin linaendelea kama kawaida mpaka Februari,25 mwaka 2021.

Chanzo cha picha, Getty Images