Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Emmanuel Macron: Rais wa Ufaransa akutwa na virusi vya corona
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amekutwa na virusi vya corona, taarifa kutoka ofisi yake zimeeleza.
Macron mwenye miaka 42-alifanya vipimo mara tu alipoanza kujisikia daalili, na sasa anajitenga kwa muda wa siku saba, taarifa kutoka Ikulu zimeeleza.
Na kuongeza kusema, Bwana Macron bado anaendelea na shughuli za kuiongoza nchi huku akiwa amejitenga.
Wiki hii, Ufaransa iliweka marufuku ya watu kutotembea muda wa usiku baada ya maambukizi ya corona kuongezeka.
Ufaransa imethibitisha maambukizi milioni mbili tangu janga la corona lilivyoibuka, huku kukiwa na vifo 59,400 kwa mujibu wa data kutoka chuo kikuu cha Johns Hopkins.
"Rais amekutwa na Covid-19 leo," alisema Elysée afisa wa ikulu majira ya asubuhi.
Haijajulikana ni vipi bwana Macron alipata maambukizi hayo na watu waliokutana naye wameainishwa.
Waziri mkuu Jean Castex, 55, pia amejitenga kwasababu walikutana na rais kwa karibu.
Alikuwa anataka kuanzisha sera ya serikali katika chanjo - kwa sasa waziri wa afya Olivier Véran atafanya hivyo.
Bwana Castex haoneshi dalili zozote, maofisa wameeleza.
Taarifa kutoka ofisi ya rais haijasema kama mke wa rais bi. Brigitte, ambaye ana miaka 67, kama alikutwa na virusi vya corona pia.
Bwana Macron ni miongoni mwa viongozi wakubwa duniani waliopata ugonjwa huo.
Rais wa Marekani Donald Trump alipata corona mwezi Oktoba na kumfanya alazwe siku tatu hospitalini.
Waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson pia alipata virusi vya corona na kulazwa mpaka chumba cha wagonjwa mahututi mwezi Machi.
Mapema wiki hii, wakati Ufaransa imeweka marufuku dhidi ya corona kwa awamu ya pili baada ya maabukizi kuongezeka.
Jumatano, Ufaransa imethibitisha zaidi ya maambukizi mapya 17,700.