Matokeo ya uchaguzi Marekani 2020:Trump amfuta kazi afisa wa uchaguzi aliyepinga madai yake

Donald Trump shakes hands with Chris Krebs

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Chris Krebs alikuwa ameteuliwa na Trump
Iliyochapishwa

Rais Trump amesema "amemfuta kazi " mkuu wa usalama wa mtandao na shirika la usalama wa miundo mbinu ya uchaguzi (Cisa) Chris Krebs kwa taarifa zake "zisizo sahihi kwa kiwango cha juu " kuhusu maadili ya kura.

Bwana Trump amekataa kukubali kushindwa katika uchaguzi wa Marekani, akitoa madai yasiyo na ushahidi ya wizi "mkubwa " wa kura

Maafisa wa uchaguzi wanasema kura ya mwaka huu ilikuwa "moja ya kura salama zaidi " katika historia ya Marekani.

Wiki iliyopita Rais Trump alimfuta kazi waziri wa ulinzi Mark Esper, huku kukiwa na ripoti kwamba alikuwa na wasiwasi juu ya utiifu wa mkuu huyo wa Pentagon.

Kuna tetesi mjini Washington DC kwamba kabla ya Trump kuondoka madarakani mwezi Januari , Mkuu wa CIA Gina Haspel na mkurugeni wa FBI Christopher Wray huenda wakawa miongoni mwa wale watakaofutwa kazi na Trump.

Chris Krebs speaks in 2018

Chanzo cha picha, Reuters

1px transparent line

Sawa na wengine wengi waliofutwa kazi na Bw Trump, Bw Krebs alifahamu kwamba amefutwa kazi alipoona tweet ya Trump Jumanne, licha ya kwamba alikuwa mtu wake wa karibu, kulingana na taarifa ya shirika la habari la Reuters.

Lakini baada ya kufutwa kazi, Mkurugenzi huyo mtendaji wa zamani wa kampuni ya hakuonekana kujuta.

Kwanini Krebs alifutwa kazi?

Anaripotiwa kutofurahishwa na kutoridhishwa kwa Ikulu ya White kuhusu wavuti wa Cisa unaoitwa udhibiti wa taarifa za tetesi- Rumor Control, ambao ulipinga taarifa za upotoshaji , ambazo nyingi zilivumishwa na rais mwenyewe.

Taarifa za Reuters zinasema kuwa White House haikufurahishwa hasa na ujumbe wake wa mtandao ambao ulipinga dhana potofu uliodai kwamba kuna kompyuta maalumu za kiintelijensia zilizotumika kuhesabu kura zinazofahamika kama Hammer na Scorecard ambazo ziliingilia na kuvuruga hesabu ya kura za taifa.

Bw Krebs na maafisa wengine wa Marekani wamesema kuwa hakuna mifumo ya aina hiyo.

Muda mfupi kabla ya kufutwa kazi , alituma tweet iliyoonekana kuyalenga madai ya Trump kwamba mashine za kupigia kura katika majimbo kadhaa zilibadilisha kura zake na kuzipeleka kwa hasimu wake Joe Biden.

Bw Krebs alitweet kwamba: "ICYMI: Kuhusu madai kwamba mifumo ya uchaguzi iliingiliwa, mahsirika yote 59 ya wataalamu wa usalama yanakubali , ' kwa kila tunalolielewa, madai haya hayana ushahidi au hayana usahihi wa kiufundi .' #Protect2020".

Alikuwa ni mmoja wa maafisa wa ngazi ya juu kutoka Wizara ya mambo ya ndani na usalma ambao wiki iliyopita walitangaza kuwa uchaguzi mkuu wa Marekani wa tarehe 3 Novemba "ulilindwa zaidi kuliko uchaguzi mwingine wowote ule katika historia ya Marekani ", huku wakipinga "madai yasiyo na msingi".

Ingawa taarifa yao haikumtaja jina Bw Trump moja kwa moja , katika siku hiyo hiyo Bw Krebs alishirikisha umma ujumbe wa Twitter uliotumwa na mtaalamu wa uchaguzi uliosema: "Tafadhalini msishirikishe tweet zenye madai yasiyo na msingi kuhusu mashine za kupigia kura , hata kama yaketolewa na rais ."

Nini kilichosemwa kuhusiana na kufutwa kazi kwa Bw Krebs?

Hatua ya rais kumfuta kazi Bw Krebs imelaanniwa vikali na kamati ya usalama wa ndani ya nchi ya bunge la wawakilishi linalodhibitiwa na Democratic.

Kiongozi wa kamati hiyo amesema kuwa uamuzi wa Bw Trump unaifanya Marekani "kukosa usalama kamili" na hautasaidia kulilinda taifa dhidi ya "kampeni mbaya za kimtandao kutoka Urusi, China na Iran ".

"Ukweli ni kwamba, tangu siku ya uchaguzi, Rais Trump amekuwa akitafuta kubatilisha majtokeo ya uchaguzi kwa kuhusika katika kampeni ambayo inaweza kusababisha umma kukosa imani katika uchaguzi wetu kwa vizazi ," walisema wajumbe wa kamati