Matokeo ya uchaguzi Marekani 2020: Biden: Trump kukataa kushindwa 'ni aibu'

Iliyochapishwa

Joe Biden amesema hatua ya Rais Donald Trump kukubali kushindwa katika uchaguzi wa urais wa wiki iliyopita ni "aibu".

Lakini rais huyo mteule wa Marekani- ambaye amekuwa akiwasiliana na viongozi wa kimataifa - amesisitiza kwamba hakuna kitu kitakachozuia uhamisho wa madaraka.

Huku hayo yakijiri Bw. Trump aliweka ujumbe kwenye mtandao wake wa Twitter akisema atashinda kinyang'anyiro hicho cha uchaguzi ambacho kilibashiriwa na vituo vikuu vya televisheni kwamba atashindwa.

Kama inavyofanyika kila miaka minne, vyombo vya habari vya Marekani hubashiri mshindi.

Mpaka sasa matokeo ya uchaguzi kutoka majimbo ya Marekani hayajaidhinishwa, kura bado zinahesabiwa, lakini matokeo yatatolewa rasmi wajumbe maalum watakapokutana Disemba, 14.

Biden amesema nini?

Rais mteule aliulizwa na waandishi wa habari siku ya Jumanne kile anachofikiria kuhusu hatua ya Rais Trump kukubali kwamba alishindwa kaika uchaguzi.

"Nadhani ni aibu, kusema kweli," Bw. Biden, mwanachama wa Democratic, alisema mjini Wilmington, Delaware.

"Kile ninachoweza kusema, kwa heshima, Nadhani hatua hiyo haitasaidia kudumisha hadhi ya rais atakapoondoka madarakani."

"Mwisho wa siku, mbivu na mbichi itajulikana Januari 20," alisema akiashiria siku ya kuapishwa.

Bw. Biden amekuwa akiwasiliana kwa njia ya simu na viongozi wa kigeni anapojiandaa kuingia rasmi ofisini.

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson, Kiongozi wa Ireland Taoiseach Micheál Martin, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ni miongoni wa viongozi aliosema nao siku ya Jumanne.

Akiashiria mawasiliano hayo ya simu, Bw. Biden alisema: "Nawafahamisha kwamba Marekani imerejea tena ulingoni. Tunarudi tena katika nafasi yetu mchezoni."

Yeye na Makamu wa Rais mteule Kamala Harris wanaendelea mbele na mpango wa kuingia mamlakani. Lakini shirika dogo linaloongozwa na washirika wa Trump linadiwa kulemaza mpango huo.

Shirika hilo linalosimamia huduma zote za serikali kuu ikiwa ni pamoja na kufadhili na kusaidia utawala mpya unaoingia madarakani kufikia idara za serikali, mpaka sasa limekataa kumtambua rasmi Bw. Biden kama rais mteule.

Hata hivvyo, rais mteule amesema: "Hatuoni kitu chochote kikirudisha nyuma mipango yetu, kusema kweli."

Trump na washirika wake wamesema nini?

Siku ya Jumanne, Bw. Trump aliweka ujumbe mara kadhaa katika mtandao wa Twitter kwa kutumia herufi kubwa akisema jinsi "shughuli ya kuhesabu kura ilivuyokumbwa na udanganyifumassive," na kusema kwa majigambo: "Tutashinda!"

Mitandao ya kijamii ziliorodhesha ujumbe wake kuwa wenye utata.

Rais amekuwa akitoa madai ambayo hayajathibitishwa akisema Bw. Biden anaweza tu kushinda uchaguzi ambao umechakachuliwa kwa nhjia ya ufisadi, lakini hakuna ushahidi wowote uliotolewa kuthibitisha madai hayo.

Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo, ambaye ni mshirika wa karibu wa Trump, alisema katika mkutano wa wanahabari siku ya Jumanne, ofisi ya Idara ya mambo ya nje kwamba baada ya kura zote "halali" kuhesabiwa "muhula wa pili wa utawala wa Trump" utaanza.

Washirika wengine wa Bw. Trump kutoka chama cha Republican hawajatambua ushindi wa Biden.

Alipoulizwa kwanini hajampongeza rais mteule, Seneta wa Democratic jimbo la Wisconsin, Ron Johnson alisema: " hakuna kitu kinachostahili kupongezwa."

Seneta wa Missouri Roy Blunt amesema Bw. Trump "huenda kamwe hakushindwa".

Kiongozi wa Republican katika Bunge la Seneti Mitch McConnell amehasema Bw. Trump ana haji y akupinga listeria matokeo ya uchaguzi katika majimbo kadhaa yaliyokuwa na ushindani mkali kama vile Pennsylvania.

Uchambuzi: Kwa nini baadhi ya Warepublican wamesalia kimya?

Ni Warepublican wachache wanataka kijiingiza katika mzozo na rais kwa kukubali hadharani kwamba Joe Biden ameshinda uchaguzi. Wale ambao wamezungumzia suala hilo na kutangaza misimamu yao kama - Maseneta Susan Collins, Ben Sasse na Mitt Romney miongoni mea wengine - walikosana na Trump muda mrefu uliyopita.

Kwa wengine, rais bado ana uwezo na ushawishi mkubwa katika chama ambao anaweza kutumia dhidi yao - inasadikiwa tayari amechukua hatua dhidi ya wale wanaoonekana kutokuwa na uaminifu kwake.

Kinachoendelea kwa sasa, kuanzia kwa kiongozi wa wengi wa Republican katiaka bunge la Seneti Mitch McConnell hadi kwa viongozi wengine jina la sarakasi hii ni kuwa na subira.

Kubali rais ana haki ya kutoa madai, mpe muda wa kuelezea ghadhabu yake lakini ujue hakuna ushahidi wa kutosha kubainisha madai hayo kiasi cha kubadilisha matokea ya uchaguzi.

Kupitia mated yao, hata kama sio kupitia matamshi, wanachama wenza wa rais wa Republican wanakubaliana kuwa kufikia Januari, kutakuwa na rais mpya. Bw. Trump, pia, ataondoka tu.