Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Virusi vya corona: Waziri wa Afya Mutahi Kagwe alaumu msimu wa baridi kuwa sababu ya ongezeko la corona Kenya.
Msimu wa baridi unaoendelea huenda unachangia pakubwa ongezeko la watu wanaoambukizwa virusi vya corona nchini Kenya.
Akizungumza baada ya kutangaza idadi mpya ya wagonjwa 544 waliothibitishwa kuwa na virusi vya corona nchini humo baada ya saa 24, waziri Afya Mutahi Kagwe amewataka Wakenya kutokongamana.
Idadi hiyo amesema inajumlisha idadi ya watu walioambukizwa virusi hivyo nchini Kenya kufikia 19,125.
Wagonjwa hao wapya wanatokana na sampuli 5,259 zilizofanyiwa vipimo katika kipindi cha saa 24.
Hiyo ina maana kwamba takriban watu 289,759 wamepimwa virusi vya corona nchini Kenya.
Akizungumza katika makao makuu ya maafisa wa Afya mjini Nairobi, Kagwe amesema kwamba kijinsia walioambukizwa ni wanaume 340 na wanawake 204.
lakini wagonjwa wengine 12 wameripotiwa kufariki kutokana maradhi hayo na hivyobasi kuongeza jumla ya watu waliofariki kutokana na ugonjwa huo kufikia 311.
Habari njema hatahivyo ni kwamba wagonjwa 113 wamepona na kuweka idadi waliopona kufikia 8,021.
Awaonya madaktari
Waziri huyo amewashukuru maafisa wa Afya kwa kazi nzuri wakati wa mlipuko huu, lakini pia akatoa onyo kwa madaktari ambao hawafuati masharti ya Covid-19.
Alifichua kwamba, katika tukio moja kwamba daktari anayefanya kazi atika hospitali ya Kenyatta hivi majuzi alisafiri lakini akakosa kujitenga baadaye.
Daktari huyo baadaye alienda kuandaa upasuaji lakini akaripotiwa na mwenzake na akazuiwa kuendelea na upasuaji huo.
Pia unaweza kusoma:
Pia alizungumzia tukio jingine ambapo daktari mwengine alikutwa na corona lakini akaamua kuendelea na kazi.
''Maafisa wa Afya ndio walinzi wetu katika vita dhidi ya ugonjwa huu na hivyobasi wanapaswa kuwa na nidhamu'', aliwaambia madaktari.