Mamia wakamatwa baada ya kunaswa kwa mawasiliano ya uhalifu wa kimtandao

Chanzo cha picha, Essex Police
Mfumo wa mawasiliano wa siri unaotumiwa na wahalifu wa biashara haramu ya mihadarati na silaha umenaswa na Shirika la taifa la kupambana na uhalifu.
Shirika la taifa la kupambana na uhalifu lilishirikiana na vikosi vya maeneo ya Ulaya katika oparesheni kubwa Uingereza.
Uhalifu mkubwa ulikuwa ni miongoni mwa watu 746 waliokamatwa katika nchi za Ulaya baada ya ujumbe kwenye mtandao wa mawasiliano wa EncroChat kudukuliwa na kurekodiwa.
Zaidi ya tani mbili za dawa za kulevya, bunduki kadhaa na pauni milioni 54 pesa taslim zimenaswa, Shirika la kupambana na uhalifu limesema.

Chanzo cha picha, NCA
Maafisa wamesema kuwa walifanikiwa kuzuia watu kadhaa kuuawa baada ya kufuatilia mashambulio yaliyokuwa yamepangwa na ujumbe wa kutishia maisha katika mfumo huo wa mawasiliano.
Shirika la taifa la kupambana na uhalifu limesema kuwa oparesheni kubwa kote Ulaya ambayo ilidumu kwa zaidi ya miezi mitatu na kujumuisha maafisa wa polisi kote Uingereza, imekuwa na athari kubwa kwa magenge yanayopanga uhalifu ambayo hayajawahi kushuhudiwa.
Kamishena wa polisi wa mji, Dame Cressida Dick, ambaye kikosi chake kilikamata watu 132 na kunasa pauni milioni 13.3 pesa taslim, alielezea oparesheni hiyo kama kama mapinduzi.
Alisema kwamba: "Huu ni mwanzo tu. Tutaendelea kuvuruga mitandao ya uhalifu uliopangwa kwa sababu ya oparesheni hizi ama kwa wiki, miezi au hata ikiwezekana miaka ijayo."
'Soko la uhalifu'
Inasemekana kwamba watu 60,000 miongoni mwao hadi raia 10,000 wa Uingereza, walijiandikisha kupokea huduma za mtandao wa EncroChat ambayo makao yake ni Ufaransa, lakini kwa sasa imefutwa kabisa.
Mfumo huo wa mawasiliano ulifanyakazi katika simu za Android na kulingana na tovuti ya mtandao huo, ilitoa huduma ya usalama wa mawasiliano bila malipo.
Wateja walikuwa wanaweza kupata huduma kama ujumbe mbaya uliofutika kutoka kwa simu ya aliyeupokea baada ya kipindi fulani.
Pia ulikuwa unaweza kufuta data zote kwenye kifaa kama simu kwa kuingiza msimbo yaani code kwa kiingereza ya namba nne kutoka kwa skrini iliyojifunga.

Chanzo cha picha, NCA
Pia ilikua na sehemu ambayo ilimwezesha mtumiaji kufuta ujumbe akiwa na hofuulikuwa na hofu huenda mtambo umedukuliwa, ambapo data zone katika kifaa hicho ingelifutwa kwa kubofya nambari nne za siri kwenye skrini.
NCA linasema mfumo huo wa mawasiliano kwa njia ya ujumbe umekuwa ukitumiwa kama "soko la uhalifu" kupanga na kusambaza dawa za kulevya za kiwango cha juu kote duniani na kuagiza silaha hatari.
Mashirika ya kupambana na uhalifu yalianza kupata data kutoka kwa mtandao huo Aprili mosi baada ya kufanikiwa kuudukua mwezi Machi.
Inasadikiwa kwamba magenge ya uhalifu yalikuwa yakitumia kifaa hicho kinachoshikiliwa mkononi kupanga mashambulio dhidi ya makundi hasimu , kupanga jinsi ya kufuatilia ulipaji deni na kupanga jinsi ya kushughulikia fedha zilizopatikana kwa njia za ulaghai.
Ujumbe wa vitisho vilivyojumuisha shambulio la tindikali na kukatwa viungo vya mwili ulipatikana katika mtandao huo.
Makundi kadhaa ya uhalifu wa kupanga yamevunjwa, kwa mujibu wa NCA, huku sehemu kubwa ya waliokamatwa wakipatikana London na kaskazini magharibi mwa England.
Amri ya kutotoka nje iliowekwa kudhibiti maambukizi ya corona "ilitusaidia sana", linasema shirika hilo, likiongeza kuwa washukiwa wengi walikuwa nyumbani msako wa kuwakamata ulipoanzishwa.













