Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Coronavirus: Teknolojia ya simu ya video imekuwa ya lazima sasa
"Nilikuwa ninaongea na simu ya video wiki iliyopita, mara mpenzi wake mfanyakazi mwenzangu akakatisha nyuma yake katikati ya maongezi yetu.
Anakumbuka mshauri wa mawasiliano Jason ....
Alieza jinsi aibu hiyo ilipotokea wakati ambao maelfu ya wafanyakazi wamehamia kutumia simu ya video katika mikutano yao ya kiofisi, ili kazi iweze kuendelea wakati wakifanya kazi nyumbani.
Kiukweli watu wengi wanahitaji msaada katika hili.
Kuna tukio jingine ambapo mfanyakazi wa masuala ya fedha, kompyuta yake ikimuonesha kuwa anaangalia video ya ngono wakati kikao kikao kikiwa kinaendelea.
Mikutano ya simu kwa kutumia programu ya zoom, Microsoft au Google meet imekuwa ikiripoti visa vingi hivi karibuni kipindi ambacho watu wengi wamekuwa wakifanyia kazi nyumbani.
Wengi wetu, tunajaribu kuzoea teknolojia hii ambayo inaonekana kutuaibisha.
Ubora wa mawasiliano, matatizo ya kitekinolojia pamoja na watumiaji wenyewe wanakutana na changamoto hizo.
Wanafanya hali ya mawasiliano katika mkutano kuwa janga.
Ni vyema kila mmoja kuelewa namna teknolojia hii inavyofanya kazi na inavyoweza kuokoa muda mwingi wa kukutana kwa ajili ya kikao.
Baadhi ya wakurugenzi wamegundua namna mikutano inavyokuwa na watu wengi ambao hata sio muhimu kuwepo.
Kupunguza idadi ya watu , inamaanisha kuwa unaweza kupunguza pia kelele ambazo hazihitajiki katika kikao.
Kama vile sauti ya kupumua kwa nguvu, kupiga chafya, kukohoa, sauti za mbwa kubweka, kengele za hodi zinaweza kufungwa kwa kuzima kipaza sauti cha simu (microphone) zao.
Hata kama bila picha za video, mkutano wa simu unaweza kusaidia...
"Ninakumbuka nilikuwa na mteja kwenye simu huku nilikuwa nikisikia maji ya bafuni yakitiririka.
Alipogundua kuwa sauti ilikuwa ikisikika, wakati anaenda kufunga simu ilidondoka bafuni," Neil Henderson anakumbuka
Nani anapaswa kuwa makini katika mikutano ya simu?
Mikutano ya simu inahitaji kuwa na muongozaji wa simu zote ili kuweza kurekebisha au ,kumuelekeza mjumbe wa mkutano pale anapokosea kutumia teknolojia hiyo, kumkaribisha katika mkutano, kuangalia muda ambao utatumika, kukaribisha maswali, kuwafanya washiriki wote wako katika kikao kimoja kwa kuwajumuisha katika hatua zote za maongezi.
Mtaalamu ya masuala ya kidigitali bwana Steve Parks anasema kuwa ni vyema watu wafahamu kuwa mikutano katika simu ni sawa na kupiga simu redioni, wakati wa majadiliano na mtangazaji anapaswa kukukaribisha ili uchangie maoni yako.
Watayarishaji na watangazaji wa vipindi vya televisheni na radio wanatumia mfumo huu wa mawasiliano mara zote katika kuhakikisha kuwa wanatengeneza kipindi au wanaendesha kipindi hewani.
Kila kitu kina lengo na namna ya kuangazia jambo au swali linapotakiwa kuulizwa lazima kusema linaenda kwa nani?
Picha na mwanga wa picha ni muhimu kuzingatiwa katika mkutano wa simu ya video
Kwenye upande wa mwanga katika video, ni muhimu kwa mtu kukaa eneo ambalo ataweza kuonekana vizuri na hata kuwa katika muonekano mzuri.
Picha za mtu uko kitandani na mashuka au mavazi ya bafuni yanapaswa kuepukwa.
Kama mtu hupendi mikutano ya video, kwa wakati huu si rahisi kuiepuka.
Ni teknolojia ambayo inarahisisha watu kufanya kazi nyumbani au katika maeneo ya mbali wakiwa pamoja.