Kenya na China bado wanajenga reli kwa manufaa ya uchumi wa Afrika

Baada ya uzinduzi wa awamu ya pili wa ujenzi wa reli nchini Kenya iliyotarajiwa kuendelezwa hadi mpaka wa Kenya na Uganda (Malaba) , kulikuwa na hofu huenda uzinduzi huo ukawa mwisho wa mradi mkubwa zaidi baada ya China kudaiwa kuwa wamekataa kuufadhili.
Kufuatia fununu hizo, BBC ilifanya mahojiano na balozi wa China nchini Kenya bwana Wu Peng kuhusu msimamo wao katika mradi huo.
"Tunaamini kuwa ujenzi wa reli kutoka Naivasha mpaka Kisumu utaweza kuinua hali ya uchumi ya Kenya na kuwa kituo cha biashara cha Afrika mashariki.
China itaendelea kuwaunga mkono katika jitihada zote za kukamilisha reli hiyo.
Hatujabadili mawazo yetu katika uwekezaji wetu na wala kutokuwa na imani na hiki kinachoendelea kwa sababu ujenzi huu una manufaa makubwa kwa bara la Afrika".
Balozi huyo aliongeza kuwa China imejizatiti katika uwekezaji huu na vilevile inaheshimu maamuzi ambayo serikali ya Kenya inayatoa katika miradi yake.
"Tunaamini kuwa Kenya inaweza kufanya maamuzi mazuri sana kwa kuzingatia uchumi wake na fedha zilizopo, ila kile ambacho ninachoweza kusema ni kuwa kwa upande wa China na upande wa Kenya zinafanya kazi kwa pamoja ili kuzindua hatua inayofuata ya ujenzi huo."
Unaweza kusoma zaidi:

Balozi Wu Peng alibainisha kuwa wanafanyia kazi ufadhili wa ujenzi huo ingawa kila kitu kina utaratibu.
Alithibitisha kuwa China haina mpango wowote wa kumiliki mali yoyote ya taifa la Kenya kwa kile wanachokifanya.

Tofauti na uzinduzi wa reli ya kutoka Mombasa hadi Nairobi, ilivyozinduliwa kwa mbwembwe mwaka 2017, uzinduzi wa reli hii mpya haujapewa umuhimu mkubwa.
Wachambuzi wanasema Serikali inakabiliwa na wakati mgumu kuelezea faida za kiuchumi za mradi huo kwa sababu baadhi ya vituo havina shughuli nyingi katika mkoa wa bonde la ufa.
Mpango wa kuendeleza ujenzi wa reli hiyo hadi Kisumu, kupitia ziwa Victoria, hadi Uganda umekatizwa na hatua ya China kujiondoa katika ufadhili wake.
Katika kongamano la viongozi wa bara la Afrika na China mjini mataifa ya Afrika mjini Beijing, Serikali ya ilisema itafadhi miradi iliyo na manufaa ya kiuchumi pekee












