Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Simulizi ya mwanaharakati wa watu wanene anayetaka usawa
Megan Jayne Crabbe alianza kupambana na mwili wake akiwa na umri wa miaka mitano.
Siku ya kwanza alipoanza shule alizingatia kujilinganisha na watoto wenzie waliokuwa wakimtania kuwa yeye ni kibonge badala ya kutengeneza marafiki wapya.
Kwa sasa Megan anafuatiliwa na watu zaidi ya milioni moja katika ukurasa wake wa Instagram.
Hivi karibuni ametoa wito kwa kuliambia bunge kuwa hofu ya mtu kuwa mnene ni jambo ambalo linapaswa kufuatiliwa kwa ukaribu na kupatiwa suluhisho.
Ilimchukua karibu miongo miwili kuukubali mwili wake,miaka ambayo alipambana na utaratibu wa mlo wake na kutafuta tiba.
Akiwa na miaka 21, aliacha chuo kwa ajili ya kufikia malengo yake ya kupungua uzito na kufanikiwa lakini bado alikuwa anajichukia.
Unaweza kusoma kuhusu:
"Ninajua sasa kuwa haijalishi uzito gani ninao, siwezi kuridhika ," alisema Megan, ambaye sasa na 26. "Siwezi kuendelea na aina hiyo ya maisha. Ninajua kuwa kuna vya zaidi. Niliharibu utaratibu wangu wa kula na kunigharimu sana na hata nilipoteza muda na nmekataa kuendelea kutojikubali".
"Niliweka picha ya mwanamke katika kwenye kurasa yangu ya Instagram akiwa amevaa nguo ya kuogelea huku akionyesha muonekano wa furaha kuwa anakubali mwili wake - na kusema kuwa hakuna haja ya kupunguza kiasi cha chakula nnachokula na kufurahia maisha. Kabla sikuwahi kuona kuwa hiyo ndio njia mbadala kwangu."
Megan alianza kuweka picha za mwili wake akiwa ameweka ujumbe chanya kuhusu unene na kuwavutia maelfu ya watu.
Megan anajitambulisha kuwa msichana kibonge na marafiki zake wanafurahi lugha anayoitumia.
" Neno unene lilikuwa na nguvu ya nguvu kubwa ambayo inaweza kunitoa kwenye baridi. Nimeishi maisha yangu kwa hofu ya kuitwa mnene, nilikuwa hata siwezi kuliona neno hilo ," alisema. " Lakini wakati nilipobaini kuwa ni vyema kuwa na mtazamo chanya, nilifunguka na namna mpya ya kuishi na kuona unene kuwa jambo zuri. Hiyo ni namna tu ya kuuelezea mwili wako kwa namna tofauti."
Megan alianza kupunguza kiwango cha chakula akiwa na umri wa miaka 10 na kuwaambia wazazi wake kuwa anataka kuwa na afya njema lakini baadae aligundua kuwa anahatarisha maisha yake.
Akiwa na miaka 14, aliugua mpaka akalazwa hospitalini kwa kushindwa kula chakula vizuri na akiwa na umri wa miaka 20 , alizidi kuchukia muonekano wa mwili wake.
Chuki aliyokuwa nayo kwa mwili wake ilimpelekea akaacha masomo yake na kuchukua jukumu la kumlea dada yake ambaye alikuwa ana utindio wa ubongo.
Kwa sasa anajitambulisha kuwa mwanaharakati , mwana mitindo, muandishi na muhamasishaji wa umma.
Megan, ambaye anaishi Colchester huko Essex, alialikwa bungeni hivi karibuni kuzungumzia usawa kwa watu wanene.
"Hatuwezi kuzungumzia kuhusu picha inayotaka hofu ya unene unene bila kuangazia ubaguzi ambao upo kila siku unaowafanya watu wanene wanyanyaswe na jamii, kuna watu wengi hawana amani kwa sababu wana hofu kwa kuwa wao ni wanene."
Megan huwa anakosolewa pia mtandaoni kwa wale ambao wanaamini kuwa watu wanaoamini kwenye picha anahamasisha mtindo wa maisha ambao sio rafiki.
Anaamini kuwa mazungumzo kuhusu uzito wa mwili wake na kuelimisha watoto shuleni kwa sababu hali inatisha na watu wanaaibishwa.
Matarajio yake Megan ni kuona watu wakipenda muonekano wa miili yao na kuwa na malengo ya kuheshimiwa.
" Ninajihisi kuwa mtu ambaye nina bahati na kuanzisha harakati hizi katika umri huu ni kwa sababu ninapata jumbe kutoka kwa wanawake wazee wakisimulia namna walivyokuwa wanachukia miili yao na sasa wanajifunza kujikubali".
Nikiwa na umri wa miaka mitano, nilihisi kuwa mnene ni jambo baya zaidi duniani, nimetoka mbali sana .Maisha yangu karibu yote nmekuwa nikijichukia na sitaki mtu mwingine apitie kile ambacho knilikipitia.