Tetesi za soka Ulaya Ijumaa 31.12.2021: Laporte, Saka, Botman, Kessie, Dembele

Manchester City defender Aymeric Laporte

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Beki wa Manchester City Aymeric Laporte
Iliyochapishwa

Barcelona wanataka kumsajili beki wa Manchester City na Uhispania Aymeric Laporte mwenye umri wa miaka 27 msimu ujao. (Sun)

Liverpool wanavutiwa na winga wa Arsenal na England Bukayo Saka, 20, ambaye kandarasi yake huko Emirates inamalizika 2024. . (Transfer Window podcast, via Express)

Liverpool pia wametoa ofa ya mkataba kwa kiungo wa kati wa AC Milan wa Ivory Coast Franck Kessie, 25, ambaye mkataba wake San Siro unakamilika mwishoni mwa msimu huu. (Ansa - in Italian)

Bukayo Saka celebrates scoring for England against Andorra in a World Cup qualifying match

Chanzo cha picha, Getty Images

Newcastle wanakaribia kumnunua mlinzi wa Lille Mholanzi aliyekadiriwa kuwa na thamani ya pauni milioni 30 Sven Botman, 21, kama sehemu muhimu ya biashara yao ya uhamisho wa Januari. (Mail)

The Magpies pia wanamfuatilia kiungo wa Juventus kutoka Wales Aaron Ramsey, 31, huku West Ham na Everton pia wakimtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31. (Sun)

th

Chanzo cha picha, Barcelona fc

Newcastle wameweka ofa ya kandarasi ya "kubwa" kwa winga wa Barcelona ambaye hana utulivu Ousmane Dembele, 24. (Rudy Galetti on Twitter)

Arsenal imewatambua Mchezaji wa Real Sociedad na Uswidi Alexander Isak, 22, na nyota wa Lille na Canada Jonathan David, 21 kama chaguo linalowezekana ili kuimarisha safu yao ya ushambuliaji. (The Athletic - subscription required)

Chelsea wanakaribia kumnunua kiungo wa kati wa Monaco Mfaransa Aurelien Tchouameni, 21, ambaye anaweza kuwa chaguo nafuu kuliko nyota wa West Ham na England Declan Rice, 22. (Daily Telegraph's Matt Law on the London is Blue podcast, via Chelsea Chronicle)

th

Chanzo cha picha, AFP

Lyon wamekataa jaribio la Chelsea la kutaka kumuita beki wa kushoto wa Italia Emerson Palmieri, 27, ambaye yuko kwa mkopo katika klabu hiyo ya Ligue 1. (L'Equipe, via Get French Football News)

Leeds wanataka kumsajili mshambuliaji wa Argentina, Giovanni Simeone, 26, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo Verona kutoka Cagliari, majira ya joto. (L'Arena, via Sport Witness)

Barcelona wamemfanya mshambuliaji wa zamani wa Chelsea, Alvaro Morata, 29, ambaye kwa sasa yuko Juventus kwa mkopo kutoka Atletico Madrid, kuwa lengo lao kuu la Januari. (AS - in Spanish)