Tetesi za soka Ulaya Jumamosi tarehe 23.10.2021: Conte, Fonseca, Sanchez, Van de Beek, Saul, Fofana, Rudiger

Meneja wa zamani wa Juventus, Chelsea na Inter Milan Antonio Cont

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Meneja wa zamani wa Juventus, Chelsea na Inter Milan Antonio Cont
Iliyochapishwa

Meneja wa zamani wa Juventus, Chelsea na Inter Milan Antonio Conte "atapenda" kuchukua usuani katika Manchester United iwapo klabu hiyo ya Primia Ligi itamfuta kazi Ole Gunnar Solskjaer. (The Transfer Window Podcast via Star)

Meneja wa zamaniwa Roma Paulo Fonseca, mwenenye umri wa miaka 48, yuko tayari kuteuliwa na Newcastle kama meneja baada ya meneja wa zamani wa Chelsea Frank Lampard kujiondoa katika mbio za kuchukua nafasi ya Steve Bruce katika St James' Park. (Mirror)

mshambuliaji wa Inter Milan na Chile Alexis Sanchez

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mshambuliaji wa Inter Milan na Chile Alexis Sanchez

Everton wanajiandaa kufanya uhamisho kwa ajili ya mshambuliaji wa Inter Milan na Chile Alexis Sanchez, 32, huku mshambuliaji huyo wa zamani Arsenal na Manchester United akiwa huru kuondoka katika klabu ya Italia katika mwezi wa Januari. (InterLive - in Italian)

Chelsea haitatekeleza azimio lake la awali la kusaini mkataba wa kudumu wa pauni milioni 34 na kiungo wa kati wa Atletico Madrid mwenye umri wa miaka 26, Saul Niguez. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uhispania alihangaika kupata mafanikio ya kimchezo tangu alipojiunga na the Blues kwa mkataba wa mkopo katika mwezi wa Agosti. (La Razon - in Spanish)

Kiungo wa kati wa Manchester United Mholanzi Donny van de Bee(jezi nyeusi)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kiungo wa kati wa Manchester United Mholanzi Donny van de Bee(jezi nyeusi)

Kiungo wa kati wa Manchester United na Uholanzi Donny van de Beek, 24, amemuomba wakala wake kupata uhamisho wake wa kuhamia Real Madrid. (Sun)

Mlinzi Muingereza Chris Smalling, 31, anaweza kuwa mmoja wa wachezaji watakaoondoka Roma katika mwezi wa Julai. (Calciomercato - in Italian)

Cristiano Ronaldo, 'aliharibiwa' na 'kuvunja sheria za usawa na unyenyekevu'

Chanzo cha picha, REX FEATURES

Mshambuliaji wa Manchester United na Ureno Cristiano Ronaldo, 36, 'aliharibiwa' na 'kuvunja sheria za usawa na unyenyekevu' katika Juventus. (Mail)

Real Madrid Bayern Munich wanaamini kabisa kuwa watasaini mkataba na kiungo wa safu ya kati-nyuma Mjerumani Antonio Rudiger, mweney umri wa miaka 28 ambaye mazungumzo kuhusu mkataba wake na Chelsea yamefikia kiwango cha kukwama. (ESPN)

Getty

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wesley Fofana

Mchezaji wa safu ya ulinzi wa kikosi cha vijana wenye chini ya umri wa miaka 21 cha Leicester na Ufaransa Wesley Fofana, 20, anazivutia klabu za Manchester United na Newcastle. (But! Football Club via Sport Witness)

mshamuliaji wa Mfaransa Alexandre Lacazette

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mshamuliaji Mfaransa Alexandre Lacazette

Meneja wa Arsenal Mikel Arteta atakataa ofa yoyote ya kumuuza mshambuliaji Mfaransa Alexandre Lacazette, 30, mwezi Januar, na badala yake atamruhusu kuondoka kwa uhuru wakati mkataba wake utakapoisha katika msimu ujao. (Sun)

Kipaumbele cha Rudiger ni kubakia Chelsea, lakini mchuano wa kutaka saini yake 'uko wazi'. (Fabrizio Romano)

Ousmane Dembele

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Ousmane Dembele anasakwa na klabu za Primia Ligi

Manchester City, Tottenham, Liverpool na Newcastle zinamtaka winga Mfaransa Ousmane Dembele, 24, ambaye ana uwezekano wa kuondoka Barcelona msimu ujao. (90Min)

Kiungo wa kati wa England Harry Winks, 25, ameleta mashaka juu ya hali yake ya baadaye katika Tottenham baada ya kukiri kwamba amekuwa aking'ang'ana kurejea katika hali yake bora ya zamani ya kimchezo kama sehemu ya mchezaji wa chini ya Nuno Espirito Santo. (Times - subscription required)

Getty

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Nahodha wa Newcastle na mlinzi Muingereza Jamaal Lascelles,

Nahodha wa Newcastle na mlinzi Muingereza Jamaal Lascelles, 27, anasema wachezaji lazima wawajibike kwa kufukuzwa kazi kwa Steve Bruce. (Mail)

Manchester City wanajiandaa kujiunga na Barcelona katika mbio za kusaini mkataba na winga Mbrazili mwenye umri wa miaka 21, Antony kutoka klabu ya Ajax. (El Nacional - in Spanish)

Mserbia Filip Djuricic

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mserbia Filip Djuricic anasakwa na klabu za Uingereza

West Ham na Southampton wanataka kusaini mkataba na mshambuliaji wa kati wa Sassuolo Mserbia Filip Djuricic, 29, ambaye alicheza nusu ya pili ya msimu wa 2014-15 kwa mkopo katika the Saints. (Calciomercato - in Italian)

Everton wanamtaka kiungo wa Manchester United na England Jesse Lingard, 28, mwezi Januari. (Football Insider)

Kocha wa United Ole Gunnar Solskjaer

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kocha wa manchester United Ole Gunnar Solskjaer

Kocha wa United Ole Gunnar Solskjaer anasema klabu hiyo haijapokea ofa kutoka Everton kwa ajili ya kiungo wake wa Uholanzi Van de Beek, licha ya uwepo wa tetesi nyingi. (RTL7, via Manchester Evening News)