Tetesi za Soka Ulaya Jumatano 06.10.2021: Rudiger, Mbappe, Vlahovic, Bremer, McKennie

Chanzo cha picha, Getty Images
Rais wa Real Madrid Florentino Perez ana matumaini Mshambuliaji wa Paris St-Germain, Mfaransa, Kylian Mbappe,22, atajiunga na klabu hiyo mwaka 2022.(El Debate - in Spanish)
Mlinzi wa Ujerumani na klabu ya Chelsea Antonio Rudiger, 28, amesema hatetereshwi na tetesi zinazomhusisha yeye na Bayern Munich. (Mirror)
Wakati mkataba wa Rudiger ukitarajiwa kuisha muda wake majira ya joto yajayo, kocha wa Chelsea Thomas Tuchel anatamani mlinzi huyo wa kati asaini mkataba mpya na mahasimu wao Tottenham kwa ajili ya uhamisho huru. (Express)

Chanzo cha picha, Reuters
Fiorentina imesema mshambuliaji wa Serbia Dusan Vlahovic, 21, anayehusishwa na kuhamia Arsenal na Tottenham, hajakubali mkataba mpya na klabu hiyo ya Serie A. (Evening Standard)
Liverpool bado wana nia na mchezaji wa nafasi ya ulinzi wa Torino Bremer,24, lakini Manchester United na Manchesyer City wamekuwa pia wakimfuatilia Mbrazili huyo. (Calciomercato via TEAMtalk)
Red Bull Salzburg wanahitaji kati ya pauni milioni 25 na milioni 34 kwa ajili ya mshambuliaji wa Kijerumani Karim Adeyemi, ambaye anatolewa macho na klabu ya Liverpool na Bayern Munich. (Sky Germany - in German)

Chanzo cha picha, Getty Images
Juventus wanajiandaa kuachana na kiungo wa kati wa Kimarekani Weston McKennie, ambaye anatakiwa na Tottenham na West Ham. (TEAMtalk)
Mlinda mlango wa Ajax na Cameroon Andre Onana, 25, yuko tayari kujiunga na Inter Milan kama mchezaji huru mwaka 2022. (Fabrizio Romano)

Chanzo cha picha, Getty Images
Barcelona imeendelea na mazungumzo na kiungo wa kati wa zamani, Xavi,41 ili achukue nafasi ya mkufunzi Ronald Koeman, lakini makubaliano na Mhispania huyo hayajafikiwa. (90min)
Bernd Leno, 29, yuko hatarini kuwa chaguo la pili la Ujerumani, ambalo litafanya kuondoka kwake Arsenal Januari kuwa jambo linalowezekana.(Fussball.News, via Star)












