Sanchez Vergara Brayan mshindi wa mzunguko wa kwanza wa Tour du Rwanda

Sanchez Vergara Brayan wa timu ya Medellin ya nchini Colombia

Chanzo cha picha, Ferwacy

    • Author, Yves Bucyana
    • Nafasi, BBC Africa, Kigali
  • Iliyochapishwa

Sanchez Vergara Brayan wa timu ya Medellin ya nchini Colombia ndiye mshindi wa mzunguko wa kwanza wa mashindano ya mbio za baiskeli maarufu 'Tour du Rwanda' yaliyoanza leo nchini Rwanda.

Brayan Sanchez,28 ametumia muda wa saa 2 dakika 33 na sekunde 43 kumaliza mzunguko huo wa umbali wa kilomita 115.6

Sanchez Vergara Brayan mshindi wa mbio za baiskeli za Tour du Rwanda

Chanzo cha picha, Ferwacy

Waendeshabaskeli 44 kutoka timu 16 zikiwemo nyingi kutoka bara ulaya ndio wanashiriki mashindano hayo yaliyoanzia ambayo mzunguko wa kwanza ulianzia mjini Kigali na kuishia katika mji wa Rwamagana mashariki mwa Rwanda.

Ushindani mkali umeanza kujitokeza baina ya waendeshabaiskeli kutoka Colombia walioko katika timu ya Medellin,timu ya taifa ya Eritrea, Tarteletto-Isorex ya Ubelgiji,bila kusahau waendeshabaiskeli kutoka Rwanda ambao walishinda mashindano haya miaka ya nyuma.

Waendesha baiskeli wakichuana vikali

Chanzo cha picha, Ferwacy

Mbali na timu za ulaya na Marekani zinashiriki tu nchi 3 za Afrika,ambazo ni Algeria, Eritrea na wenyeji Rwanda.

Brayan Sanchez,28 ametumia muda wa saa 2 dakika 33 na sekunde 43 kumaliza mzunguko huo wa umbali wa kilomita 115.6

Chanzo cha picha, Ferwacy

Kesho watashindana katika mzunguko wa pili ambapo watatoka mjini Kigali kuelekea katika mji wa Huye umbali wa kilomita 120.5

Shindano a Tour du Rwanda ni miongoni mwa mashindano 2 makubwa barani Afrika sawa na shindano la Tropical Amissa Bongo la Gabon.

Mashindano hayo yako kwenye kiwango kinachofahamika kama 2.1 kama inavyotambuliwa kwenye kalenda ya mashindano ya mbio za baiskeli duniani .