Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Virusi vya corona:DRC wataka kujihakikishia usalama wa chanjo
Iliyochapishwa
Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imeahirisha kampeni ya kutoa chanjo ya corona iliyokua ianze leo Jumatatu kwa hofu ya usalama wake.
DRC inaungana na baadhi ya nchi za Ulaya, zilizositisha utoaji wa chanjo hiyo, baada ya baadhi ya watu waliopatiwa kupata athari ya kuganda damu.
Taifa hilo limepokea dozi milioni moja na laki saba ya chanjo hiyo aina ya AstraZeneca na ilikuwa inatarajiwa kuanza zoezi la kuchanja watu leo. DRC inataka kujiridhisha kwanza na usalama wa chanjo hiyo.