Tetesi za soka Ulaya Jumanne 14.07.2020: Guardiola, Neymar, Messi, Mbappe, Ndombele

Chanzo cha picha, AFP
Rais wa Barcelona Josep Maria Bartomeu amekataa uwezekano wa mshambuliaji wa Paris St-Germain Neymar,28, kurejea Nou Camp lakini amesema klabu inafikiria uhamisho wa mshambuliajji wa Inter Milan Muajentina Laitaro Martinez, 22. (TV3 Mundo Deportivo)
Bartomeu pia amesema ana ''uhakika'' mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi,33, atasalia Nou Camp zaidi ya mwaka ujao. (TV3 via Evening Standard)
Manchester City itatoa ofa kwa kocha Pep Guardiola ya mkataba wa muda muda mrefu baada ya marufuku dhidi ya klabu hiyo kufutwa. (Mirror)

Guardiola atapatiwa karibu kitita cha pauni milioni 150 kwa ajili ya kukipa nguvu kikosi cha City. (Guradian)
Real Madrid inaamini kuwa mshambuliaji Kylian Mbappe ,21, atakuwa na mazungumzo nao kuhusu uhamisho kutoka Paris St-Germain. (Marca)
Liverpool ina mpango wa kumuuza beki wake Dejan Lovren,31, ingawa anatafuta kuongeza mkataba wake. (Goal)

Bayern Munich wanajiandaa kuanza mchakato wa kumnasa Tanguy Ndombele ,23, wa Tottenham na Mfaransa mwenzie anayecheza katika nafasi ya kiungo cha kati katika klabu ya Monaco, Tiemoue Bakayoko,25. (Le 10 Sport via Daily Mail)
Nice imetoa ofa kwa kiungo wa kati Mhispania Rony Lopes anayekipiga Sevilla. (RMC Sport-in French)
Mkurugenzi wa michezo katika klabu ya Norwich Stuart Webber amesema kwamba kandarasi ombi la kutaka kumnunua mchezaji kinda mwenye kipaji mwisho wa msimu litaanza kwa dau la £20m . (Norwich Evening News)

Chanzo cha picha, Getty Images
Brentford inamlenga winga wa Portsmouth Ronan Curtis,24 kwa ajili ya kuchukua nafasi ya Said Benrahma ikiwa ataondoka kwenye klabu hiyo. (The News, Portsmouth)
TETESI ZA JUMATATU
Inter Milan wanafikiria kumnunua kiungo wa kati, Mfaransa N'Golo Kante huku Blues wakiwa tayari kusikiliza ofa kwa ajili ya kumuuza mchezaji huyo wa Ufaransa, 29. (Gazzetta dello Sport, via Metro)
Zenit St Petersburg wameeleza nia yao ya kumsajili beki anayekipiga katika klabu ya Liverpool Dejan Lovren, 31. (Liverpool Echo)
AC Milan wanafiukiria kumnunua mashambuliaji wa Real Madrid raia wa Serbia Luca Jovic, 22, ambaye anatekodolewa macho na Leicester City na Arsenal. (Calciomercato,via Leicester Mercury)

Chanzo cha picha, Getty Images
Kai Havertz anataka kuondoka Bayer Leverkusen kwasababu walishindwa kufuzu katika michunao ya klabu bingwa Ulaya hivyobasi Chelsea watalazimika kuhakikisha wanafuzu katika michuano hiyo ili kumshawishi kiungo huyo wa Ujerumain 21 kujiunga na timu hiyo.. (Bild)
Bayern Munich wana mpango wa kuwanasa viungo wawili wanaocheza ligi kuu ya Ufaransa, Tonguy Ndombele wa Tottenham, 23, na Tiemoue Bakayoko. (Le 10Sport)
Mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic, 38, amesema hana uhakika kuhusu mustakabali wake ndani ya AC Milan kwa kuwa hakuna mazungumzo yoyote yaliofanyika kuhusu mkataba ikiwa sasa ni chini ya mwezi mmoja kabla ya mkataba wake kufikia ukingoni. (Sky Sports)
Mashabiki 5,000 waliruhusiwa kuingia uwanjani kutazama mechi ya kirafiki ya Paris St Germain, mechi iliyoitoa kifua mbele kwa 9-0 dhidi ya wenyeji Le Havre. (France 24)












