Tanzania na Kenya zawekwa kundi moja AFCON 2019

Mataifa manne kutoka Afrika Mashariki, Tanzania, Kenya, Uganda na Burundi kushiriki michuano hiyo.

Moja kwa moja

  1. Harambee Stars ya kenya yafuzu baada ya miaka 15

    Timu ya taifa ya mpira wa miguu nchini Kenya, Harambee Stars ilifuzu kushiriki michuano ya Mataifa Bingwa Barani Afrika (AFCON) mwaka 2019.

    Thibitisho kwamba Timu ya Taifa Harambee Stars imefuzu kwa michuano hiyo ya 2019 lilitangazwa baada ya kikao kisicho cha kawaida cha siku nzima cha Kamati Kuu ya Shirikisho la Kandanda Barani Afrika (CAF) jijini Accra, Ghana.

    Kikao hicho kilithibitisha uamuzi wa kuitupa nje timu ya taifa ya Sierra Leone kutoka katika mechi za kufuzu kwa dimba hilo baada ya shirikisho lao kupigwa marufuku na Shirikisho la soka duniani FIFA.

    Huku ikiwa imesalia mechi moja ya makundi kukamilika, Shirikisho la CAF liliafikia uamuzi wa kufutilia mbali matokeo yote yaliyohusisha na taifa hilo la Afrika Magharibi na hivyo kuliacha kundi hilo na timu tatu pekee.

    Sierra Leone ilikuwa imecheza mechi mbili katika kampeini yao na kwa sababu haikuwa imekamilisha nusu ya mechi zote za kufuzu,

    Shirikisho la CAF liliamua kufutilia mbali matokeo yote ya awali yaliyohusisha taifa hilo kulingana na kanuni za kufuzu.

    wachezaji wa timu ya kenya harambee stars

    Chanzo cha picha, AFP/GETTY IMAGES

    Maelezo ya picha, wachezaji wa timu ya kenya harambee stars
  2. Taifa Stars yavunja mwiko wa miaka 39

    Taifa Stars
    Maelezo ya picha, Kikosi cha Taifa Stars kilicgoifunga Uganda na kufuzu AFCON 2019

    Timu ya Taifa Tanzania imefuzu katika michuano ya Mataifa ya Afrika (Afcon) kwa mara ya pili baada ya kusubiri kwa miaka 39.

    Mara ya mwisho kwa timu hiyo maarufu kama Taifa Stars ilikuwa 1980, ambapo hakuna hata mchezaji mmoja katika kikosi cha sasa ambaye alikuwa amezaliwa, na kocha wao Mnigeria Emmanuel Amunike alikuwa mtoto wa miaka 10.

    Baada ya safari yao kupitia milima na mabonde,Taifa Stars wamefuzu katika siku ya mwisho kabisa ya mchuano wa makundi Jumapili Machi 24 baada ya kuifunga Uganda 3-0. Ushindi huo uliwafanya Stars kufikisha alama 8 na kujikatia tiketi ya kwenda Misri Juni mwaka huu.

    Habari kamili ya Tanzania ilivyofuzu bonyeza hapa

  3. Nchi nne za Afrika Mashariki kuchuana na nani?

    Muda mfupi ujao droo ya michuano ya Afcon 2019 itapangwa, na kuna uwezekano mkubwa nchi za Afrika Mashariki zikakutana kwenye hatua ya makundi.

    Tayari shirikisho la Mpira wa miguu limeandaa vyungu vinne ambavyo kila chungu kimoja kina mataifa sita ambayo haya takutana kwenye hatua ya makundi.

    Nchi za Afika Mashariki zilizofuzu ni Tanzania, Uganda, Kenya na Burundi.

    Katika timu hizo Kenya na Uganda wapo kwenye chungu namba tatu, hivyo hawatakutana hatua ya makundi.

    Tanzania na Burundi wapo kwenye chungu namba nne, hivyo hawatakutana kwenye hatua ya makundi.

    Hiyo inamaanisha Tanzania au Burundi ziinaweza kupangwa kundi moja na Uganda au Kenya kwenye hatua ya makundi.

    Je unapenda nchi za Afrika Mashariki zikutane mwanzoni kabisa?

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

  4. Karibu katika matangazo ya moja kwa moja ya droo ya Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2019 inayofanyika nchini Misri.