Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Mapigano yaripotiwa mashariki mwa Rafah huku Israel ikifungua tena kivuko cha msaada cha Kerem Shalom

Kumekuwa na mapigano makali na mashambulizi ya mabomu karibu na mji wa kusini wa Gaza wa Rafah, huku Israel ikisema kivuko muhimu cha Kerem Shalom kimefunguliwa tena kwa ajili ya msaada.

Moja kwa moja

Asha Juma, Lizzy Masinga and Ambia Hirsi

  1. Vita vya Gaza: Wito waongezeka kwa Israeli kufungua vivuko vya mpaka ili kuruhusu misaada

    Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameonya kwamba hali "inakwenda katika njia mbaya" huko Gaza kufuatia Israel kuivamia Rafah, kimbilio la mwisho la Wapalestina ambalo limekumbwa na mashambulizi makali ya kijeshi na ambayo maelfu wanakimbia.

    Mkuu wa sera za mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell amesema "licha ya maombi yote ya jumuiya ya kimataifa" kwa Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kutoshambulia Rafah, shambulio hilo limeendelea.

    "Ninaogopa kwamba hii itasababisha, tena, majeruhi wengi," Borrell alisema.

    "Hakuna maeneo salama huko Gaza," aliongeza.

    Wakati huo huo Kamanda mkuu wa Kamandi Kuu ya Jeshi la Marekani (CENTCOM) ametembelea Misri, ambako alijadili usalama wa kikanda na "kupunguza mateso ya kibinadamu huko Gaza" na viongozi wa kijeshi wa nchi hiyo.

    Erik Kurilla alisema kuwa Misri imekuwa "chombo" katika kuwezesha "msaada wa kibinadamu kwa watu wa Gaza".

    "Mikutano kama ya leo ni muhimu katika kujenga uelewa wa kina wa changamoto za kikanda na kudumisha uhusiano unaohitajika ili kuboresha usalama," alisema.

    Soma zaidi:

  2. Hujambo na karibu katika matangazo yetu mubashara ikiwa ni tarehe 08/05/2024