Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Hamas yakubali masharti ya makubaliano ya kusitisha mapigano Gaza

Kundi hilo linasema katika taarifa kwamba limeidhinisha makubaliano yaliyopendekezwa na wapatanishi wa Misri na Qatar.

Moja kwa moja

Asha Juma, Lizzy Masinga and Ambia Hirsi

  1. Serikali ya Kenya yatafuta idhini ya kutumia Sh.Bilioni 10 kukabiliana na mafuriko

    Bunge la taifa nchini Kenya kuidhinisha shilingi bilioni 10.6 kwa ajili ya kukabiliana na dharura ya mafuriko na misaada ya kibinadamu kwasababu ya mvua kubwa inayoendelea kunyesha kote nchini humo.

    Maelezo ya fedha hizo yapo kwenye bajeti ya II ya ziada katika kipindi cha mwaka wa fedha mwaka 2023/2024.

    Kufikia Jumamosi zaidi ya watu 228 walikuwa wamefariki dunia kutokana na mafuriko na maelfu ya watu kujeruhiwa huku wengine wengi wakilazima kuhama makazi yao.

    Mvua hiyo isiyokoma imeharibu mazao na mali huku serikeli ikitenga makazi ya muda kwa watu waliohama makwao.

    Hatua hii inafuatia tangazo ya mamlaka ya hali ya hewa la kunyesha kwa mvua kubwa katika maeneo mengi kote nchini humo.

    Pia unaweza kusoma:

  2. Wanajeshi watatu wa Israel wauawa katika shambulizi la roketi Gaza

    Israel imefunga kivuko cha Kerem Shalom kuelekea Gaza baada ya Hamas kurusha makombora kutoka ndani ya ukanda huo.

    Israel ilisema shambulio hilo liliua wanajeshi wake watatu, na kujeruhi wengine kadhaa.

    Kivuko hicho ni mojawapo ya njia chache za kupeleka misaada ya kibinadamu, ikiwa ni pamoja na chakula na vifaa vya matibabu, hadi Gaza.

    Wapatanishi nchini Misri wamefanya mazungumzo ya siku mbili yenye lengo la kupata makubaliano ya kusitisha mapigano huko Gaza na kuachiliwa kwa mateka wanaoshikiliwa na Hamas.

    Katika taarifa, Hamas ilisema duru ya hivi punde zaidi imekamilika Jumapili na kwamba ujumbe wake sasa utasafiri kutoka Cairo hadi Qatar kushauriana na uongozi wa kundi hilo.

    Mkuu wa CIA William Burns, ambaye pia amehusika katika juhudi za upatanishi, ameondoka katika mji mkuu wa Misri kwa mazungumzo huko Doha, kulingana na ripoti.

    Pendekezo la kusitisha mapigano linaaminika kuhusisha kusitisha mapigano kwa siku 40 huku mateka wakiachiliwa huru, na kuachiliwa kwa idadi ya wafungwa wa Kipalestina wanaozuiliwa katika jela za Israel.

    Hamas ilisema ililitazama pendekezo la sasa katika " mtazamo chanya", lakini jambo muhimu linaloendelea kujitokeza inaonekana kuwa kama makubaliano ya kusitisha mapigano yatakuwa ya kudumu au ya muda mfupi.

    Soma zaidi:

  3. Hujambo na karibu kwa matangazo yetu ya mubashara leo ikiwa nai Jumatatu tarehe 06.05.2024