Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Kombora la Israel lashambulia Iran, maafisa wa Marekani wathibitisha

Maafisa wawili wa Marekani wamethibitisha shambulio la Israeil dhidi ya Iran kwa mshirika wa BBC wa Marekani CBS News huku milipuko ikiripotiwa karibu na Isfahan.

Moja kwa moja

Ambia Hirsi, Abdalla Seif Dzungu and Dinah Gahamanyi

  1. BBC idhaa ya Kiajemi imepokea video kutoka kwa wakazi wa Isfahan

    Idhaa ya Kiajemi ya BBC inaripoti kwamba imetumwa video kadhaa zilizochukuliwa na wakaazi wa mkoa wa Isfahan katikati mwa Iran usiku kucha, ambapo vyombo vya habari vya serikali ya Iran vinaripoti kuwa milipuko imesikika.

    Katika video moja iliyowekwa kwenye akaunti ya Instagram ya BBC Persian, sauti za kile kinachoonekana kuwa bunduki za kukinga mashambulizi zinaweza kusikika.

  2. Habari za hivi punde, Safari za ndege zasitishwa katika miji ya Iran - Serikali

    Safari za ndege za kibiashara zimesitishwa katika miji mikuu ya Iran, ikiwa ni pamoja na Isfahan, Shirax na Tehran, vyombo vya habari vya nchi hiyo vinaripoti, kulingana na shirika la habari la Reuters.

    Isfahan ni mji wa kati ambapo milipuko iliripotiwa na vyombo vya habari vya Iran.

    Imeripotiwa pia kuwa wasafirishaji wa Mashariki ya Kati Emirates na Fly Dubai walianza kuelekeza safari zao za ndege magharibi mwa Iran mapema Ijumaa asubuhi, bila maelezo.

  3. Habari za hivi punde, Kombora la Israel lashambulia Iran, maafisa wa Marekani waiambia CBS

    Kombora la Israel limeipiga Iran, maafisa wawili wa Marekani wameambia kitui cha habari cha CBS News.

    Vyombo vya habari vya serikali ya Iran vinaripoti kwamba safari za ndege zimesitishwa katika miji kadhaa, kulingana na chombo cha habari cha Associated Press.

    Iran imekuwa katika hali ya tahadhari baada ya Israel kusema kuwa itajibu mashambulizi dhidi yake Jumamosi usiku.

  4. Hujambo na Karibu.