Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Mahakama ya juu nchini Uganda yaidhinisha sheria yenye utata dhidi ya mapenzi ya jinsia moja

Kundi linalojumuisha wanaharakati, viongozi wa kidini na wanasheria wanasema watakata rufaa dhidi ya uamuzi huo.

Moja kwa moja

Abdalla Seif Dzungu and Asha Juma

  1. Rais Zelensky atia saini sheria inayoruhusu watu wenye umri wa miaka 25 na 26 kujumuishwa jeshini

    Rais wa Ukraine Vladimir Zelensky alisaini marekebisho ya Sheria hiyo "Juu ya Wajibu wa Kijeshi na Huduma ya Kijeshi" iliyopitishwa na azimio la Rada ya Verkhovna mwaka 2023, ambalo linapunguza umri wa juu wa kuandikishwa kwa wale wanaowajibika kwa huduma ya jeshi kutoka miaka 27 hadi 25.

    Wakati wa kuandaa muswada huo, Wizara ya Ulinzi ya Ukraine ilihalalisha kupunguzwa kwa kikomo cha umri wa kuandikishwa kwa hitaji la kujaza hifadhi ya kijeshi

    Mabadiliko hayo ya sheria yanawezesha kupanua mduara wa raia ambao wanaweza kuhamasishwa kujumuisha kwa raia wenye umri wa miaka 25 na 26.

    Kabla ya hili, Waukraine kati ya umri wa miaka 27 na 60 walikuwa chini ya sheria ya kuhudumia jeshi hata bila ya uzoefu wa huduma ya kijeshi.

  2. Taylor Swift na Magic Johnson miongoni mwa orodha mpya ya watu matajiri zaidi duniani - Forbes

    Taylor Swift amejiunga na Elon Musk kuwa miongoni mwa watu matajiri zaidi duniani, kulingana na orodha mpya ya matajiri.

    Nyota huyo wa pop wa Marekani aliingia kwenye Orodha ya Mabilionea Duniani ya Forbes kwa mara ya kwanza akiwa na $1.1bn (£877m), pamoja na Sam Altman, muundaji wa Chatbot ya AI kwa $1bn (£800m).

    LVMH Bidhaa za kifahari za Ufaransa Bernard Arnault na familia yake waliongoza orodha hiyo kwa wastani wa $233bn (£185bn).

    Forbes walisema kulikuwa na rekodi ya mabilionea 2,781 mwaka 2024.Idadi hiyo ni 141 zaidi ya mwaka jana na 26 zaidi ya rekodi ya awali iliyowekwa mwaka wa 2021.

    Forbes iliongeza kuwa wasomi hao walikuwa matajiri zaidi kuliko hapo awali - wakiwa na utajiri wa jumla wa $14.2tn (£11.3tn).

    Mwimbaji na mtunzi wa nyimbo Taylor Swift aliingia kwenye orodha ya matajiri baada ya kupata hadhi ya kuwa nyota mkubwa. Alikuwa mwigizaji wa kwanza kushinda tuzo ya albamu ya mwaka mara nne.

    Albamu yake ya 1989 (Taylor's Version) pia ilikuwa katika LP ya vinyl iliyouzwa zaidi mwaka jana.Mafanikio ya Swift sio tu kwenye ulimwengu wa muziki.

    Kuwepo kwake tu katika michezo ya soka ya Marekani ili kumtazama mpenzi wake Travis Kelce kumepewa sifa ya kuinua takwimu za watazamaji wa NFL.

    Linapokuja suala la watu 10 bora zaidi duniani, wanane walioorodheshwa walitoka Marekani - sita kati yao wakipata pesa zao katika tasnia ya teknolojia.

    Baada ya Mfaransa Bw Arnault na familia yake, Bw Musk, mmiliki wa Tesla na X, zamani Twitter, ameorodheshwa wa pili, akiwa na wastani wa utajiri wa $195bn (£155bn).Anafuatwa wa tatu na mmiliki wa Amazon Jeff Bezos.

    Utajiri wa Bw Musk ulipanda kwa 8% kutoka mwaka jana lakini chini ya thamani yake mnamo Novemba 2021, alipokuwa mtu wa kwanza kuwahi kuwa na thamani ya $300bn (£239bn).

    Pia anayejiunga na orodha ya Forbes ni nguli wa mpira wa vikapu Magic Johnson mwenye utajiri wa $1.2bn (£950m) na mtayarishaji wa TV Dick Wolf, pia akiwa na $1.2bn.

  3. Habari za hivi punde, Makumi wajeruhiwa na mtu mmoja kuripotiwa kufariki na tetemeko la ardhi Taiwan

    Idara ya zimamoto ya Taiwan imesema mtu mmoja amefariki na zaidi ya 50 wamejeruhiwa, kulingana na shirika la habari la Reuters.

    Chombo cha habari cha Taiwan UDN kinanukuu Baraza Kuu la Kukabiliana na Maafa na Kuzuia likisema mtu mmoja aliuawa baada ya kuangukiwa na mawe. Bado haijabainika iwapo hiki ni kifo kile kile kilichoripotiwa na Reuters.

    Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Taiwan, polisi wameokoa takriban watu tisa kutoka kwa jengo lililoporomoka kwa sehemu huko Hualien na watu watano bado wanasubiri msaada.

  4. Video: Tazama jinsi gari la wafanyakazi wa misaada lilivyoharibiwa na shambulio la Israel Gaza

  5. Biden 'akasirishwa' na mashambulio ya Israeli dhidi ya wafanyikazi wa misaada Gaza

    Rais wa Marekani Joe Biden amelaani mauaji ya Israel ya wafanyakazi saba wa misaada ya kibinadamu huko Gaza.

    Akisema "amekasirishwa na kuvunjika moyo", aliishutumu Israel kwa kutochukua hatua za kutosha kuwalinda wafanyakazi wa misaada.

    Israel iliahidi uchunguzi huru baada ya Uingereza, Marekani, Canada, Australia na Poland kupoteza raia katika shambulio la Jumatatu.

    Rais wa Israel Isaac Herzog ameomba radhi kwa vifo hivyo.

    Waathiriwa saba, ambao walikuwa wakifanya kazi katika Jiko Kuu la Dunia (WCK), waliuawa wakati msafara wao uliposhambuliwa kutoka angani siku ya Jumatatu.

    Bw Biden alitaka uchunguzi wa Israel ufanywe haraka, na akasema "lazima uwajibikaji" na matokeo yake kuwekwa hadharani.

    Usambazaji wa misaada huko Gaza umekuwa "mgumu sana", alisema, kwa sababu Israel "haijafanya vya kutosha kuwalinda wafanyakazi wa misaada wanaojaribu kutoa msaada unaohitajika sana kwa raia".

    Katika baadhi ya lugha yake kali tangu vita kuanza, Bw Biden pia aliishutumu Israel kwa kutchukuwa hatua za kutosha kuwalinda raia wa Palestina.

    "Marekani mara kwa mara imekuwa ikiitaka Israel kusitisha operesheni zao za kijeshi dhidi ya Hamas, ili kuepusha maafa ya raia," kiongozi huyo wa Marekani alisema.

  6. Tetemeko la ardhi lenye nguvu zaidi katika miaka 25 laikumba Taiwan

    Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 7.4 katika kipimo cha Richter lilitokea kwenye pwani ya mashariki ya Taiwan siku ya Jumatano, na kutoa tahadhari ya tsunami katika kisiwa hicho na nchi jirani.

    Chanzo cha tetemeko hilo kinapatikana takriban 18km (maili 11) kusini mwa mji wa Hualien wa Taiwan, kulingana na Utafiti wa Jiolojia wa Marekani.

    Majengo mengi yameporomoka kwa kiasi huko Hualien na yanaonyeshwa yakiwa yameegemea upnde mmojaNi tetemeko la ardhi lenye nguvu zaidi nchini Taiwan katika miaka 25, wamesema maafisa wa seismolojia.

    Kampuni kubwa ya kutengeneza chipsi ya Taiwani TSMC ilisema imehamisha baadhi ya viwanda vyake huko Hsinchu na kusini mwa Taiwan kwa ajili ya usalama wa wafanyakazi wake, lakini ikaongeza kuwa mifumo yake ya usalama inafanya kazi kama kawaida.

    TSMC ni mzalishaji mkuu wa semiconductors kwa makampuni makubwa ya ya teknolojia ikiwa ni pamoja na Apple na Nvidia.Katika mji mkuu wa Taipei, video zinaonyesha majengo yakitikiswa kwa nguvu, na kusababisha vitu kutuma kiruka na kutapakaa kila mahali.

    Katika maeneo ya ndani ya milima ya Taiwan, video zilizochapishwa kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha tetemeko hilo limesababisha maporomoko makubwa ya ardhi. Kiwango cha uharibifu huo bado hakijajulikana.

    Picha kwenye vyombo vya habari vya ndani zinaonyesha majengo ya makazi yaliyoporomoka na watu wakihamishwa kutoka kwa nyumba na shule zao.

    Athari za tetemeko hilo pia zimevunja magari na kurusha vitu ndani ya maduka, kulingana na video zilizopeperushwa na kituo cha utangazaji cha TVBS.

    Kukatika kwa umeme na kukatika kwa mtandao kumeripotiwa kote kisiwani, kulingana na kikundi cha ufuatiliaji wa mtandao wa NetBlocks.

    Tetemeko la ardhi la Jumatano lilipiga saa 07:58 saa za ndani (23:58 GMT) katika kina cha 15.5km na limesababisha angalau mitetemeko tisa yenye ukubwa wa 4 au zaidi.

  7. Natumai hujambo