Hujambo na karibu kwa matangazo ya moja kwa moja leo Alhamisi 14.12.2023.
Haya ndio matukio ya hivi punde katika mzozo wa Israel na Palestina kwa ufupi:
- Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel asema Israel itaendeleza vita 'ikiwa itapata au kukosa’ uungwaji mkono wa kimataifa, baada ya kura ya jana usiku ya Umoja wa Mataifa ya kutaka kusitishwa kwa mapigano huko Gaza.
- Wizara ya afya inayoongozwa na Hamas inasema watu 18,608 wameuawa huko Gaza tangu kuanza kwa vita.
- Wakati huo huo, Israel inasema wanajeshi 10 wa IDF wameuawa kaskazini mwa Gaza - na kuifanya kuwa siku mbaya zaidi kwa wanajeshi wake tangu kuanza kwa mashambulizi yake ya ardhini.
- Nchini Marekani, Rais Joe Biden amekutana ana kwa ana kwa mara ya kwanza na familia ya mateka wa Marekani
- Na watu wameansamana nje ya bunge la Israel, wakitaka kuachiliwa huru mateka wote waliosalia wanaoshikiliwa na Hamas huko Gaza.
- Maafisa wa Marekani na Uingereza wametangaza wimbi jipya la vikwazo vinavyolenga watu wanaohusishwa na Hamas
- Wakati Rais wa Kamisheni ya Umoja wa Ulaya ametoa wito wa kuwekewa vikwazo walowezi wa Israel "wenye msimamo mkali", ambao anasema wanahusika na mashambulizi dhidi ya Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi.
- Na onyo limetolewa kuhusu uwezo wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wasaidia wakimbizi wa Kipalestina
