Vita vya Gaza: Mateka wanane wa Israel waachiliwa huru na Hamas Gaza

Chanzo cha picha, Reuters
Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) limetangazalinasema kuwa kwamba mateka sita wa Israel waliokuwa wameshikiliwa na kundi la Hamas wameachiliwa huru sasa wako wako Telaviv.
"Kulingana na taarifa iliyotolewa na Shirika la Msalaba Mwekundu, mateka wanane wa Israel wako njiani kuelekea Israel," IDF lilichapisha kwenye mitanao yake ya kijamii
Mateka wawili waliachiliwa awali, na hivyo jumla ya mateka walioachiliwa na Hamas kufikia sasa wanane.
Wafungwa wengine thelathini wa Kipalestina wameachiliwa na kutoka magereza ya Israel kama malipo.
Majina ya mateka wa Israel walioachiliwa huru na Hamas na wamerejea ndani ya Israel yalitangazwa kuwa ni:
- Shani Goren, 29
- Nili Margalit, 41
- Ilana Gritzewsky, 30
- Sapir Cohen, 29
- Bilal Zyadna, 18
- Aisha Zyadna, 16
Wengine walioachiliwa ni:
- Mia Shem, 21
- Amit Soussana, 40
Wizara ya mambo ya nje ya Qatar imethibitisha kuwa jumla ya watu10 waliotekwa nyara imefikiwa, kwa sababu raia wawili wa Urusi na Israel walioachiliwa Jumatano wamejumuishwa katika hesabu ya Alhamisi.
Ofisi ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu imetoa taarifa ya kuwakaribisha waliorudishwa hivi karibuni:
Ilisema :''Serikali ya Israeli inakumbatia raia wetu sita ambao wamerejea hivi punde katika eneo la Israeli. Familia zao zimesasishwa na mamlaka zinazohusika kwamba wamerejea nchini. Serikali ya Israel imejitolea kuwarejesha mateka wote na waliopotea''.
Majina ya Wapalestina walioachiliwa bado hayajatolewa.
