Israel yawaambia raia kuondoka katika maeneo ya kusini mwa Gaza huku mapigano yakianza tena
Wizara ya afya inayosimamiwa na Hamas yasema watu kadhaa wameuawa tangu mapigano kuanza tena, huku makombora yakirushwa pia kusini mwa Israel.
Moja kwa moja
Dinah Gahamanyi, Ambia Hirsi and Asha Juma
Hali ya kibinaadamu Gaza huenda ikazidi kuwa mbaya huku vita vikiendelea kushika kasi

Chanzo cha picha, Reuters
Makubaliano ya Israel na Hamas, ambayo yalisababisha usitishaji vita kwa siku saba huko Gaza, yalipelekea kuachiliwa kwa mateka 110 waliotekwa nyara katika mashambulizi ya Hamas tarehe 7 Oktoba. Kwa upande wake, wafungwa wa Kipalestina waliokuwa wakishikiliwa katika jela za Israel waliachiliwa, na misaada iliyohitajika sana ya kibinadamu iliingia Gaza kwa wingi zaidi.
Baada ya mapatano kumalizika, Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu aliishutumu Hamas kwa kukiuka makubaliano hayo, akisema haijawaachilia wanawake wote waliotekwa nyara leo, na kwa kurusha makombora dhidi ya Israel. Hamas kwa upande wake ilisema Israel imekiuka makubaliano hayo, kwa kutoruhusu mafuta kupelekwa kaskazini mwa Gaza.
Kuanza tena kwa mapigano kunaweza kuzidisha mgogoro wa kibinadamu huko Gaza. Usitishaji huo wa mapigano ulikuwa umeruhusu ongezeko la idadi ya malori yenye usaidizi kuingia katika eneo hilo.
Sasa, hali hii inaweza kuwa hatari zaidi. Mashambulizi ya Israel pia yanaweza kusababisha wimbi jipya la watu kuyahama makazi yao, kwani huenda mwelekeo wa wanajeshi ukawa katika maeneo ya kusini ambayo yanachukuliwa kuwa salama.
Na, cha kuhuzunisha, majeruhi wapya wataweka shinikizo upya kwa mfumo wa afya ambao tayari uko karibu kuporomoka. Wizara ya afya inayosimamiwa na Hamas imesema takriban watu 54 wameuawa tangu kumalizika kwa mapatano hayo.
Soma zaidi:
- Wapalestina walioachiliwa wadai kunyanyaswa katika jela za Israel
- Qatar yathibitisha kuwa mazungumzo mapya ya kusitisha mapigano yanaendelea
- Mashambulizi makubwa ya anga yatokea kaskazini mwa Gaza huku makombora yakirushwa Israel
- Vipeperushi vyatolewa na IDF kuwataka watu kuondoka Khan Younis
- Jinsi Hamas walivyounda jeshi la kushambulia Israel tarehe 7 Oktoba
- Jinsi mzozo wa mateka wa Israeli utakavyoubadili ulimwengu milele" - The Telegraph
- Netanyahu anasema Hamas ilivunja mapatano kwa kukataa kuwaachilia mateka zaidi
Wapalestina walioachiliwa wadai kunyanyaswa katika jela za Israel

Maelezo ya picha, Mohammed Nazzal anasema alipigwa na walinzi wa magereza wa Israel Wafungwa wa Kipalestina walioachiliwa kutoka jela za Israel wameiambia BBC kwamba walinzi waliwanyanyasa na kuwapa adhabu ya pamoja wiki chache baada ya mashambulizi ya Hamas dhidi ya Israel tarehe 7 Oktoba.
Wafungwa hao - ambao waliachiliwa wiki iliyopita kama sehemu ya makubaliano ya mateka ambayo sasa yamekamilika - wameelezea kuchapwa kwa fimbo, kuwekewa mbwa waliofungwa midomo, na nguo zao, chakula na blanketi kuchukuliwa.
Mfungwa mmoja wa kike amesema alitishiwa kubakwa, na kwamba walinzi waliwarushia mabomu ya kutoa machozi mara mbili ndani ya seli.
BBC ilizungumza na watu sita kwa jumla, ambao wote walisema walipigwa kabla ya kuondoka jela.
Jumuiya ya Wafungwa wa Kipalestina inasema baadhi ya walinzi wanadaiwa kuwakojolea wafungwa waliofungwa pingu na kwamba wafungwa sita walifariki wakiwa jela.
Kujibu madai hayo, Jeshi la Magereza la Israel liliambia BBC wafungwa wote walizuiliwa kwa mujibu wa sheria na walikuwa na haki zao zote za kimsingi zinazohitajika kisheria.
"Hatujui madai uliyoelezea," ilisema katika taarifa. "Hata hivyo, wafungwa na waliozuiliwa wana haki ya kuwasilisha malalamiko ambayo yatachunguzwa kikamilifu na mamlaka rasmi."
Israel haikuzungumzia swali letu kuhusu vifo wakiwa kizuizini moja kwa moja, lakini ilisema kuwa wafungwa wanne walifariki kwa tarehe nne tofauti katika wiki zilizopita, na kwamba huduma ya magereza haikuwa na ufahamu wa sababu za kifo.
Soma zaidi:
- Qatar yathibitisha kuwa mazungumzo mapya ya kusitisha mapigano yanaendelea
- Mashambulizi makubwa ya anga yatokea kaskazini mwa Gaza huku makombora yakirushwa Israel
- Vipeperushi vyatolewa na IDF kuwataka watu kuondoka Khan Younis
- Jinsi Hamas walivyounda jeshi la kushambulia Israel tarehe 7 Oktoba
- Jinsi mzozo wa mateka wa Israeli utakavyoubadili ulimwengu milele" - The Telegraph
- Netanyahu anasema Hamas ilivunja mapatano kwa kukataa kuwaachilia mateka zaidi
Tanzania yatia saini moja ya mkataba mkubwa wa mazingira unaohusisha hifadhi za taifa

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Shirika la usimamizi wa mbuga za Tanzania na jamii za mitaa zitapokea baadhi ya mapato kutokana na mradi wa kukabiliana na kaboni Tanzania imetia saini mkataba wa moja ya miradi mikubwa ya upunguzaji wa hewa ukaa Afrika Mashariki.
Tanzania, ambayo ina raslimali ya misitu yenye takribani hekta milioni 48, imeibuka kuwa miongoni mwa wahusika wakuu wa Afrika katika biashara ya kimataifa ya kufidia uchafuzi wa mazingira.
Mradi huu unahusisha hifadhi sita za taifa, zenye ukubwa wa hekta milio ni 1.8 (ekari milioni 4.4).
Tangazo hilo linakuja huku viongozi wa dunia wakikutana mjini Dubai kwa ajili ya mkutano wa COP28 unaolenga kutafuta njia za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Miradi ya kukabiliana na uchafuzi wa mazingira: ni kwamba shirika ambalo linachafua mazingira linaweza kulipia mradi wa upanzi wa miti wenye thamani ya tani moja ya hewa ukaa.
Pesa zinazolipwa na shirika zinakusudiwa kwenda kwenye miradi ya kupunguza hewa ukaa, kwa hiyo kwa kila tani ya hewa ukaa iliyotolewa, mradi huo unawakilisha tani ya hewa ukaa ambayo ilinaswa.
Kwa njia hii, kiasi cha jumla cha hewa ukaana uchafuzi mwingine unaozalishwa unatakiwa kukaa sawa, au hata kupunguzwa.
Mkataba huo mpya ni muungano kati ya mamlaka ya hifadhi za taifa nchini Tanzania, Tanapa, na kampuni ya Carbon Tanzania, nchini humo.
Baadhi ya mapato kutokana na mradi wa fidia juu ya uchafuzj wa mazingira yataenda kwa Tanapa na jamii za mitaa, Carbon Tanzania ilisema Alhamisi.
Qatar yathibitisha kuwa mazungumzo mapya ya kusitisha mapigano yanaendelea

Chanzo cha picha, Reuters
Serikali ya Qatar imethibitisha mazungumzo kati ya Hamas na Israel ili kurejesha usitishaji mapigano yanaendelea.
Katika taarifa, wizara ya mambo ya nje ya Qatar inaeleza "masikitiko makubwa kwa kuanza tena uvamizi wa Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza".
Inaongeza kuwa Qatar imejitolea "kuendeleza juhudi zilizosababisha kusitishwa kwa misaada ya kibinadamu" pamoja na washirika wake katika upatanishi kati ya Hamas na Israel.
Lakini taarifa hiyo pia inasema kuwa kuanza tena kwa mashambulizi ya mabomu huko Gaza baada ya kumalizika kwa usitishaji mapigano "kunatatiza juhudi za upatanishi na kuzidisha maafa ya kibinadamu".
Qatar iliongoza juhudi za upatanishi ili kupata na kupanua mkataba wa wiki moja wa kubadilishana mateka, uliomalizika asubuhi ya leo.
Soma zaidi:
- Qatar yathibitisha kuwa mazungumzo mapya ya kusitisha mapigano yanaendelea
- Mashambulizi makubwa ya anga yatokea kaskazini mwa Gaza huku makombora yakirushwa Israel
Vita vya Ukraine: Zelensky asema kuimarisha safu za ulinzi vitani lazima kuharakishwe

Chanzo cha picha, PRESIDENTIAL PRESS SERVICE HANDOUT HANDOUT/EPA
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema ulinzi lazima uimarishwe haraka vitani, baada ya kukutana na makamanda katika baadhi ya vituo vyenye shinikizo kusini na mashariki.
"Katika sekta zote kuu ambapo uimarishaji unahitajika, [lazima] tuharakishe ujenzi wa miundo," alisema katika hotuba yake ya kila usiku.
Vikosi vya Urusi vinajaribu kuuzingira mji wa mashariki wa Avdiivka.
Na wanalenga mikoa ya kusini ya Kherson na Zaporizhzhia.
Usiku wa kuamkia jana jeshi la anga la Ukraine lilisema kuwa limeangusha ndege 18 kati ya 25 za Urusi na moja ya makombora mawili ya masafa mafupi.
Huku halijoto ikishuka chini ya baridi kali kupindukia na Ukraine ikifunikwa na theluji, Rais Zelensky amesema "majira ya baridi kwa ujumla ni awamu mpya ya vita".
Kiongozi huyo wa Ukraine alisema "uangalifu wa hali ya juu" utatolewa kwa miji ya mashariki inayokabiliwa na mzozo katika eneo la Donetsk pamoja na safu kuu ya ulinzi kaskazini-mashariki kati ya Kupyansk na Lyman.
Alijumuisha pia eneo karibu na mji mkuu wa Kyiv ambapo ngome zingeimarishwa.
Msisitizo wa Rais Zelensky juu ya kuimarisha safu za ulinzi unaweza kutoa uzito kwa hofu ya mzozo unaozidi, licha ya mapigano makali kuendelea.
Upinzani upande wa Ukraine tangu msimu wa kiangazi unatazamwa na watu wengi kuwa umeshindwa kuleta mafanikio yaliyotarajiwa.
Soma zaidi:
Joshua Cheptegei: Eliud Kipchoge aunga mkono Uganda kuchukua ubingwa kabla ya kuanza kwa marathon
Maelezo kuhusu taarifa - Author, Michelle Katami
- Nafasi, BBC Sport Africa

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Joshua Cheptegei anakimbia marathon yake ya kwanza Jumapili huko Valencia Joshua Cheptegei bado hajawahi kukimbia marathon lakini bingwa mara mbili wa Olimpiki Eliud Kipchoge anaamini kuwa Mganda huyo anaweza kuwa mwanariadha mwenye kasi zaidi duniani kwa zaidi ya maili 26.2.
Cheptegei alishinda medali ya dhahabu ya mita 5,000 katika Michezo ya Tokyo 2020 na anashikilia rekodi ya ulimwengu kwa umbali huo na mita 10,000.
Kipchoge, ambaye ndiye anayempa hamasa, sasa anamuunga mkono Cheptegei kabla ya mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 27 kuanza kukimbia mbio za marathon kwa mara ya kwanza mjini Valencia Jumapili.
"Tayari anashikilia rekodi katika nyanja zingine na ana nafasi kubwa ya kuvunja rekodi ya ulimwengu katika mbio za marathon," Kipchoge aliambia BBC Sport Africa.
"Joshua ana kipaji na nidhamu. Pia anajifunza vyema.
"Nina furaha Joshua anajaribu kitu kipya. Nitakuwa nikitazama na kumpa motisha kama kawaida."
Cheptegei anachukuliwa kuwa mmoja wa wakimbiaji bora zaidi wa mbio za masafa marefu duniani, akiwa na mataji matatu ya dunia ya mita 10,000 na taji la dunia la mbio za nyika pamoja na dhahabu ya Olimpiki.
Hapo awali alishikilia rekodi za dunia za mbio za kilomita 5 na 10 na akafunzwa na Kipchoge, ambaye alivunja rekodi ya marathon mara mbili, mnamo 2015 huko Kaptagat.
Mkenya huyo anasema "ukuaji" wa Cheptegei umetokana na umbali mbalimbali wa mbio alizokimbia, lakini kijana huyo mwenye umri wa miaka 39 amemshauri raia huyo wa Uganda kukimbia mbio zake binafsi siku ya Jumapili.
"Kipchoge alinitia moyo sana nilipokuwa nikianza taaluma yangu, urithi wake unanitia moyo," Cheptegei alisema.
"Maneno yake ya ukarimu siku zote yameweza kuniongoza kwa siku na miaka. Eliud huwa ananifuatilia, anatuongoza katika njia nzuri.
"Ni heshima kubwa kujifunza kutoka kwa wakuu. Kwa heshima hii maalum, ninatazamia kutumia kile tunachoshirikishana pamoja kila wakati."
Pia unaweza kusoma:
Taarifa za hivi punde baada ya usitishaji mapigano kwa muda kuisha

Chanzo cha picha, Reuters
Ndio tu adhuhuri imeingia nchini Israel na Gaza baada ya asubuhi iliyochafuka kufuatia mapigano kuanza tena saa za mapema. Haya ndiyo matukio yote muhimu kufikia sasa:
- Mapigano yameanza tena huko Gaza baada ya kusitishwa kwa mapigano kwa muda na Hamas kufuatia siku saba za kuachiliwa kwa mateka.
- Huko Gaza milio mikubwa ya risasi na mashambulizi mengi makubwa ya anga yameonekana na kusikika, huku makombora yakirushwa kuelekea kusini mwa Israel kutoka Ukanda wa Gaza.
- Jeshi la Israel limeilaumu Hamas kwa kukiuka masharti ya mapatano kwa kushindwa kuwaachilia mateka wote wa kike na watoto wanaoshikiliwa huko Gaza.
- Vilevile, Hamas imelaumu Israel kwa kuvunja makubaliano ya kusitisha mapigano, ikisema ilikuwa inazuia usambazaji wa mafuta kufika kaskazini mwa Gaza.
Watu kadhaa waripotiwa kuuawa
- Wizara ya afya ya Gaza inayoendeshwa na Hamas imesema takriban watu 30 wameuawa na mashambulizi ya anga saa chache tangu mapigano kuanza tena.
- Vipeperushi vimetupwa vikiwaonya watu mashariki mwa mji wa Khan Younis, kusini mwa mji wa kusini kuelekea Rafah, karibu na mpaka wa Misri.
- IDF imeunda ramani mpya inayogawanya Gaza katika mamia ya kanda, ambayo inasemekana itatumika kuwaonya raia kuhusu maeneo wanayohitaji kuhama ili "kujiandaa kwa hatua inayofuata ya vita"
Mazungumzo yanaendelea na Marekani inatoa onyo
·Mazungumzo magumu ya kuanza tena kusitisha mapigano yanaendelea nchini Qatar, duru zimeiambia BBC
- Kabla ya mapigano kuanza tena, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken aliiambia Israel kwamba inabidi kuwalinda raia kwa njia tofauti wakati huu, akisema idadi kubwa ya vifo vya raia na watu wengi kuhama makwao kaskazini mwa Gaza haiwezi kurudiwa tena kusini.
- Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto limetahadharisha kuhusu janga la kibinadamu, isipokuwa kama usitishaji huo utaanza tena. Msemaji wa Unicef katika hospitali moja kusini mwa Gaza alielezea hali hiyo kuwa ya kuogofya
Mashambulizi makubwa ya anga yatokea kaskazini mwa Gaza huku makombora yakirushwa Israel

Chanzo cha picha, Reuters
Muda mchache uliopita, mashambulizi makubwa kadhaa ya anga na moshi mwingi umeonekana ukipanda juu angani kaskazini mwa Ukanda wa Gaza.
Tumeona pia na kusikia makombora yakirushwa kutoka ndani ya Gaza kuelekea Israel, huku moshi ukionekana angani kutoka kwenye sehemu za mfumo wa Israel wa kujilinda dhidi ya makombora wa Iron Dome.
Hakuna dalili hata kidogo kwamba mapigano ni ya kiwango cha chini baada ya kusitisha mapigano, badala yake hapa ni kama ilivyokuwa wakati wa awali wa operesheni ya ardhini ya wanajeshi wa Israel (IDF).
Soma zaidi:
- Vipeperushi vyatolewa na IDF kuwataka watu kuondoka Khan Younis
- Jinsi Hamas walivyounda jeshi la kushambulia Israel tarehe 7 Oktoba
- Jinsi mzozo wa mateka wa Israeli utakavyoubadili ulimwengu milele" - The Telegraph
- Netanyahu anasema Hamas ilivunja mapatano kwa kukataa kuwaachilia mateka zaidi
Vipeperushi vyatolewa na IDF kuwataka watu kuondoka Khan Younis

Jeshi la Israel linaonekana kuangusha vipeperushi vya kuwaonya wakaazi wa Khan Younis kusini mwa Gaza kuelekea kusini zaidi kwa usalama wao.
Picha zinasambazwa kwenye mitandao ya kijamii za kipeperushi hicho, ambacho kinasema Khan Younis ni "eneo hatari la mapigano" na kuwaambia watu katika maeneo ya mashariki mwa jiji kuelekea kwenye makazi karibu na Rafah - karibu na mpaka wa Misri.
Vipeperushi sawa vya onyo vimeangushwa katika baadhi ya maeneo tangu vita vilipoanza, kama sehemu ya kile IDF inasema ni "njia mbalimbali za kuepuka kuwadhuru raia katika Ukanda wa Gaza".
Pia unaweza kusoma:
- Jinsi Hamas walivyounda jeshi la kushambulia Israel tarehe 7 Oktoba
- Jinsi mzozo wa mateka wa Israeli utakavyoubadili ulimwengu milele" - The Telegraph
- Netanyahu anasema Hamas ilivunja mapatano kwa kukataa kuwaachilia mateka zaidi
Habari za hivi punde, Wizara ya afya inayoendeshwa na Hamas huko Gaza yasema watu 32 wamefariki katika muda wa saa tatu
Taarifa za hivi punde kutoka wizara ya afya inayoendeshwa na Hamas huko Gaza, imesema watu 32 wameuawa tangu mapigano kuanza tena karibu saa nne zilizopita.
'Tutasimamia maslahi ya klabu zetu za Afrika' - Hersi A. Said

Chanzo cha picha, Young Africans
Rais wa klabu ya soka ya Tanzania, Young Africans, Hersi A. Said amesema kuwa uongozi mpya wa Shirikisho la Vilabu Afrika litasimamia maslahi ya klabu za Afrika, na kubuni jukwaa litakaloangalia changamoto zinazozikabili klabu na kuzitafutia suluhu.
’’...kuhusu hilo tutaweza kupaza sauti zetu katika viwango vya CAF, kwahiyo hili ndilo jukumu langu la kwanza…’’, amesema
Bw Hersi ameyasema hayo baada ya kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa kwanza wa Shirikisho la vilabu Afrika (ACA).
Hersi alichaguliwa katika mkutano wa uzinduzi wa Chama cha Vilabu vya Afrika uliofanyika mjini Cairo Misri Alhamisi
Mkutano wa uzinduzi wa Shirikisho la vilabu Afrika uliongozwa na Rais wa CAF Dk Patrice Motsepe ambaye aliona haja ya Vilabu vya Soka vya Afrika kuwa na jukwaa na muundo ambapo wanaweza kuwa na sauti katika soka la Afrika.
Atahudumu na manaibu wawili: Jessica Motaung kutoka Kaizer Chiefs (Afrika Kusini) na Paul Bassey wa Nigeria kutoka Akwa United.
Bodi Kamili: Chama cha Vilabu vya Afrika
Maeneo ya UNAF:
- Khaled Abdelkader (Al Ahly, Misri)
- Taha Diay (Raja, Morocco)
WAFU A:
- Rodney Edmond Michael (Mighty Blackpool FC, Sierra Leone)
- Famakan Dembele (AS Real Bamako, Mali)
WAFU B
- Ayibatin Wilfrido (AS Loto FC, Benin)
- Paul Bassey (Akwa United, Nigeria)
CEFA:
- Hersi A. Said (Young Africans, Tanzania)
- Hassan Ali Eissa (Al Hilal, Sudan)
COSAFA:
- Jessica Motaung (Kaizer Chiefs, Afrika Kusini)
- Salamo Newboy Hei (African Stars, Namibia)
UNIFFAC
- Ravel Mondjo Mbouloungou (CS de Bendje, Gabon)
- Guy Kapya Kilongozi (AS Maniema Union, DRC)
Milio ya risasi imesikika katika mji mkuu wa Guinea-Bissau

Chanzo cha picha, AFP
Maelezo ya picha, Milio ya risasi ilisikika Ijumaa asubuhi (picha ya maktaba) Makabiliano makali ya risasi yameripotiwa katika mji mkuu wa Guinea-Bissau mapema Ijumaa asubuhi baada ya walinzi wa vikosi maalum walipokwenda kuwatoa kizuizini waziri na kiongozi wa ngazi ya juu serikalini.
Walinzi hao wa Kitaifa waliwachukua maafisa hao kabla ya kurejea kambini kusini mwa mji mkuu.
Vikosi maalum viliingilia kati baada ya mazungumzo ya kuwaachia huru kukwama, na kuishia kutokea kwa makabiliano ya risasi.
Utulivu unasemekana kurejeshwa baadaye.
Kiongozi wa kundi la wanajeshi waliokuwa wakijaribu kuwaachilia watu hao wawili sasa anashikiliwa na jeshi na "hali imedhibitiwa kabisa", shirika la habari la AFP linamnukuu msemaji wa jeshi akisema.
Waziri wa fedha, Souleiman Seidi, na katibu wa hazina kuu ya serikali, Antonio Monteiro, walikuwa wamezuiliwa huku kukiwa na uchunguzi wa madai ya kutolewa kwa dola milioni 10 ya fedha za serikali kwa njia isiyo ya kawaida.
Walihojiwa Alhamisi alasiri na uchunguzi kuanzishwa dhidi yao kubaini malipo kwa kampuni 11 yalivyofikiwa.
Katika kikao cha bunge siku ya Jumatatu, kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini humo alidai kuwa wamiliki wa kampuni hizo walikuwa karibu na viongozi wa muungano unaotawala nchini humo.
Bw Seidi alitetea malipo hayo kuwa halali.
Katika picha: Matukio Gaza baada ya kumalizika kwa muda wa usitishaji mapigano
Tumepata baadhi ya picha kutoka Gaza baada ya Israel kuanza tena mashambulizi dhidi ya Hamas.
Usitishaji vita wa muda wa siku saba umemalizika, lakini kama mwandishi wetu wa Gaza Rushdi Abu Alouf alivyoripoti awali, afisa wa Palestina anasema wapatanishi wanaendelea na juhudi za kufikia makubaliano kati ya pande hizo mbili, hata kama mapigano yanaanza tena.

Chanzo cha picha, Getty Images

Chanzo cha picha, Picha za Getty

Chanzo cha picha, Picha za Getty

Chanzo cha picha, Picha za Getty
Netanyahu anasema Hamas ilivunja mapatano kwa kukataa kuwaachilia mateka zaidi

Chanzo cha picha, EPA
Katika saa iliyopita, Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema Hamas haikukubali kuwaachilia mateka zaidi, jambo ambalo lilikiuka masharti ya makubaliano ya kusitisha mapigano.
Hamas haikuwaachilia mateka wanawake wote kama ilivyokubaliwa na badala yake ikaishambulia Israel kwa roketi asubuhi ya leo, ofisi ya Netanyahu inaongeza.
Katika taarifa yake kwenye mitandao ya kijamii, ofisi yake inasema Israel imeendelea kuwa na nia ya kufikia malengo yake - kuwaachilia mateka, kuwaondoa Hamas na "kuhakikisha kuwa Gaza haitawahi kuwa tishio kwa wakaazi wa Israel".
Unaweza kusoma:
- Jinsi Hamas walivyounda jeshi la kushambulia Israel tarehe 7 Oktoba
- Jinsi mzozo wa mateka wa Israeli utakavyoubadili ulimwengu milele" - The Telegraph
Seneta wa Marekani amuokoa mbunge mwenzake aliyepaliwa na chakula

Chanzo cha picha, ANNA MONEYMAKER
Seneta wa Marekani alimuokoa mbunge mwenzake alikuwa amepaliwa na chakula wakati wa chakula cha mchana.
Rand Paul wa Kentucky alitumia mbinu ya Heimlich kumsaidia Seneta Joni Ernst wa Republica kutoka jimbo la Iowa.
Bw Paul alitekeleza hatua hiyo ya kuokoa maisha wakati Bi Ernst alipowaandalia chakula cha mchana wenzake wa chama cha Republican.
Haikubainika ni chakula gani kilikuwa kimezuia njia ya hewa ya Bi Ernst, lakini wafanyakazi wenzake walimsifu Bw Paul kwa hatua hiyo ya haraka.
Seneta Lindsey Graham, Mrepublican wa South Carolina ambaye hugombana mara kwa mara na Seneta huyo wa Kentucky, alisema: "Mungu ambariki Rand Paul. Sikuwahi kufikiria ningesema hivyo." Sio kila mtu alishuhudia tukio hilo.
Maseneta hao wawili walisimama kueleza kilichotokea na kuwakumbusha waliohudhuria umuhimu wa kujifunza njia za kuokoa maisha.
Habari za hivi punde, Mzozo wa Israel na Palestina: Israel yasema mapigano yameanza tena

Chanzo cha picha, Reuters
Jeshi la Israel sasa limesema limeanza tena mapigano na Hamas mjini Gaza.
Katika chapisho kwenye X, Vikosi vya Ulinzi vya Israeli vilisema kuwa Hamas walifyatua risasi dhidi ya Israel, na hivyo kukiuka masharti ya makubaliano ya kusitisha mapigano.
Awali Israel ilisema ilizuia roketi iliyorushwa kutoka Gaza huku vyombo vya habari vinavyoshirikiana na kundi la Hamas vikiripoti milipuko na milio ya risasi kaskazini mwa Gaza.
Makubaliano ya kusitisha mapigano hayo yalipangwa kudumu kwa siku nne lakini muda uliongezwa mara mbili.
Hadi kufikia Alhamisi, mateka 110 waliokuwa wameshikiliwa huko Gaza wameachiwa huru tangu kuanza kwa mapatano hayo tarehe 24 Novemba, huku Israel ikiwa imewaachia huru wafungwa 240 wa Kipalestina.
Mashambulizi ya Hamas dhidi ya Israel tarehe 7 Oktoba yaliua watu 1,200.
Tangu wakati huo, wizara ya afya ya Gaza inayoendeshwa na Hamas inasema zaidi ya watu 14,800 wameuawa katika mashambulizi ya kulipiza kisasi ya Israel, wakiwemo watoto wapatao 6,000.
Unaweza kusoma:
Milipuko na milio ya risasi yasikika kaskazini mwa Gaza - ripoti
Mashirika ya habari ya Reuters na Al Jazeera ,yanaripoti kwamba milipuko na milio ya risasi imesikika kaskazini mwa Ukanda wa Gaza, haswa kaskazini magharibi mwa mji wa Gaza, yakinukuu vyombo vya habari vinavyohusiana na Hamas.
"Tukio hili liliambatana na kuruka kwa ndege za kijeshi za Israel na ndege za kivita katika anga ya Ukanda wa Gaza," alisema mwandishi wa Al Jazeera Tareq Abu Azzoum Azzoum, ambaye alikuwa akiripoti kutoka Khan Younis kusini mwa Gaza.
Na AFP ilinukuu watu walioshuhudia wakiripoti shughuli za ndege nzito na ndege zisizo na rubani kaskazini magharibi mwa Gaza
Hapo awali, jeshi la israel lilisema limenasa roketi karibu na mpaka na Gaza.
Huku hayo yakijiri Waziri wa mambo ya nje wa Marekani alitoa ujumbe mzito kwa Israel kuhusu jinsi ya kuendelea mbele na oparesheni yake.
Anthony Blinken amesema Benjamin Netanyahu ameweka wazi kuwa Israel inakusudia kurejelea operesheni zake za kijeshi, jambo ambalo linaweza kufanyika ndani ya siku chache.
Lakini Blinken alisema oparesheni hiyo haiwezi kuwa marudio ya majuma ya kwanza ya mashambulizi ya kikatili ya Israel dhidi ya Gaza.
Beyoncé na Swift wang’ara katika onyesho la kwanza la filamu la Renaissance.

Chanzo cha picha, Getty Images
Beyoncé aliwaambia mashabiki wanapaswa "kudensi, kuimba, kucheka na kulia" walipokuwa wakitazama onyesho la kwanza la London la filamu yake ya ziara ya Renaissance.
Akiwa amevalia suti nyeupe, nyota huyo alijitokeza kwa muda mfupi mbele ya fonyesho hilo liliyodumu kwa saa tatu, na kuwaambia watazamaji "wajisikie huru".
Taylor Swift, ambaye filamu yake ya tamasha ilivunja rekodi mapema mwaka huu, pia alikuwepo.
Binti yake Beyoncé Blue Ivy pia alihudhuria hafla hiyo.
Wageni wengine ni pamoja na nyota wa Destiny's Child Michelle Williams, mwanamuziki will.i,am, mhariri wa zamani wa jarida la mitindo Vogue Edward Enniful, na muigizaji Vivica A. Fox.
Wote walivaa "vazi rasmi la kifahari" waliloomba kulivaa kwa ajili ya tukio hilo.
Muonekano wa Swift ulikuja baada ya Beyoncé kuhudhuria onyesho lake la kwanza la tamasha la Hollywood lililoitwa Eras Tour y tarehe 11 Oktoba.
Mambo matano unayopaswa kufanya iwapo unalipwa mshahara mdogo

Idadi kubwa ya watu wanaofanya kazi ulimwenguni hupokea mshahara, wakilalamika kuwa mshahara hautoshi kwa maisha yao.
Baadhi ya watu wanapaswa kuchukua mikopo ili kuishi maisha ya kuridhisha, na wanapaswa kutulia kwa muda mrefu.
Kwa mujibu wa watu wengi wanaokabiliwa na tatizo hili, inachukua muda mrefu kulipa madeni hayo, jambo linalowatumbukizakatika maisha ya dhiki, kwa kulipa madeni. Kulingana na wataalamu wa masuala ya fedha ukifanya haya unaweza kuondokana na adha ya kuishiwa:
- Epuka madeni kadri uwezavyo.
- Panga jinsi utakavyolipa bili zako kabla ya kulipwa mshahara
- Weka akiba na uwekeza hata kama ni kiasi kidogo cha pesa
- Tengeneza chanzo au vyanzo vingine vya pesa
- Achana na tabia ya matumizi yasiyo ya lazima ya pesa zako
