Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Blinken akutana na Netanyahu kushinikiza 'hatua madhubuti' kuwalinda raia wa Gaza

Jeshi la Israel lilisema "limekamilisha kuzunguka mji wa Gaza" na limekuwa likishambulia maeneo yanayotumiwa na Hamas.

Moja kwa moja

  1. Waafrika wote sasa kuingia Rwanda bila visa

    Rais wa Rwanda Paul Kagame ameanzisha safari zisizohitaji visa kwa Waafrika wote, na kuifanya Rwanda kuwa nchi ya nne barani Afrika kufanya hivyo.

    “Pia tumeondoa vizuizi vya visa kwa raia wa kila nchi ya Afrika pamoja na mataifa mengine mengi.Mwafrika yeyote anaweza kupanda ndege hadi Rwanda wakati wowote anaotaka na hatalipa chochote kuingia nchini mwetu” Rais Kagame alisema siku ya Alhamisi.

    Aliongeza kuwa hatua hiyo inalenga kufaidisha soko la utalii barani Afrika linalokua, likipigwa jeki na ukuaji wa uchumi wa kati barani humo.

    Rwanda imekuwa kwenye kampeni ya kukuza sekta yake ya utalii, ikishirikiana na vilabu vya soka kama Arsenal na Bayern Munich ili kuitangaza nchi hiyo kama kivutio cha watalii.

    Rwanda sasa inaungana na Ushelisheli, Gambia na Benin, nchi pekee za Kiafrika zinazotoa visa bila malipo kwa raia wote wa Afrika.

    Wiki hii, Rais wa Kenya William Ruto alitangaza kuwa nchi hiyo itamaliza masharti ya visa kwa wageni wote wa Kiafrika ifikapo 2024.

    Nchi kadhaa za Afrika pia zimeingia makubaliano baina ya nchi mbili za usafiri wa bila visa, hivi karibuni Ghana na Afrika Kusini, na Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

    Pia unaweza kusoma

  2. Mkuu wa Hezbollah kuvunja kimya chake juu ya vita

    Hassan Nasrallah, kiongozi wa kundi la waislamu wa Shia nchini Lebanon Hezbollah, anatarajiwa kuhutubia wafuasi wake siku ya Ijumaa, ikiwa ni maoni yake ya kwanza hadharani tangu vita vya Israel na Hamas kuzuka.

    Hotuba hiyo huenda ikaashiria hatua zinazofuata za kundi hilo, kwani wapiganaji wake na jeshi la Israel wanashambuliana vikali kwenye mpaka wa Lebanon na Israel.

    Hili limezusha hofu kwamba eneo hilo linaweza kuwa sehemu nyingine katika mzozo huo.

    Kufikia sasa, hata hivyo, ghasia hizo zimedhibitiw kwa kiasi kikubwa.

    Tangu Hamas ifanye mashambulizi ya Oktoba 7 dhidi ya Israel na kuua zaidi ya watu 1,400, Lebanon imekuwa ikifuatilia kwa karibu Hezbollah.

    Kundi hilo limezidisha mashambulizi yake dhidi ya Israel, ambayo inalipiza kisasi.

    Lakini inaonekana pande zote mbili zimechukua hatua kuepusha ongezeko la hatari, na mashambulizi mengi yamekuwa tu kwenye eneo la mpaka.

    Hii, hata hivyo, inaweza kubadilika.

    Israel inawatuhumu wataalamu wa Umoja wa Mataifa kwa kurudia propaganda za Hamas

    Israel imewashutumu wataalamu wa Umoja wa Mataifa kwa kurudia propaganda za Hamas kuhusu hali ya Gaza, kitu ilichokiita "cha kusikitisha".

    Wataalamu saba wa haki za binadamu waliopewa mamlaka na Umoja wa Mataifa walisema wanaamini kuwa raia wa Gaza wako katika hatari kubwa ya "mauaji ya halaiki" na kwamba muda unazidi kuyoyoma kuzuia hili.

    Kundi hilo la waakilishi maalum lilidai kuwa Israel ilikuwa inapanga "kuangamiza" Ukanda wa Gaza na iliitaka Israel na washirika wake kukubaliana kuhusu usitishaji vita mara moja, na kwa Hamas na wanamgambo wengine kuwaachilia huru raia wote waliochukuliwa mateka.

    "Hali ya Gaza imefikia kilele cha janga," walisema, kulingana na taarifa ya Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa..

    Alipoulizwa kuhusu taarifa hiyo katika mkutano na waandishi wa habari, Stéphane Dujarric, msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres, alisema uamuzi wa mauaji ya kimbari unaweza tu kufanywa na chombo husika cha mahakama cha Umoja wa Mataifa, kulingana na shirika la habari la Reuters.

    Israel pia iliishutumu Hamas kwa kutumia raia kama ngao za binadamu na kugeuza misaada kwa ajili ya operesheni za kigaidi.

    "Vita vya sasa vililetwa juu ya Israeli na magaidi wa Hamas ambao walifanya mauaji mnamo Oktoba 7, wakichinja watu 1,400 na kuwateka nyara watoto 243, wanaume na wanawake," ujumbe wa Israeli katika Umoja wa Mataifa huko Geneva ulisema.

    Unaweza pia kusoma

  3. Kilichotokea Alhamisi

    Huu hapa muhtasari wa yaliyotokea jana Alhamisi

    • Jeshi la Israel lilisema "limekamilisha kuzunguka mji wa Gaza"na limekuwa likishambulia maeneo yanayotumiwa na Hamas. Mji huo ndio mkubwa zaidi katika Ukanda wa Gaza na ulikuwa sehemu yenye watu wengi zaidi katika eneo hilo kabla ya vita kuanza.
    • Umoja wa Mataifa umesema shule zake nne huko Gaza ambazo zilikuwa zikitumika kama makazi zimeharibiwa katika muda wa chini ya saa 24.
    • Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa Kipalestina pia lilibainisha kuwa takriban watu 20 waliripotiwa kufariki katika shule katika kambi ya wakimbizi ya Jabalia.
    • Shule katika kambi ya wakimbizi ya Pwani, na kambi ya Al Bureij, pia ziliharibiwa, na vifo vitatu viliripotiwa.
    • Idadi ndogo ya raia waliweza kuondoka Gaza kupitia kivuko cha Rafah, karibu na mpaka wa Misri, ambao ulifunguliwa siku ya Jumatano.Maafisa wa Misri walisema Wapalestina 21 waliojeruhiwa waliondoka siku ya Alhamisi, pamoja na wamiliki wa pasipoti za kigeni 344, ikiwa ni pamoja na watoto 72.
    • Ofisi ya Mambo ya Nje ya Uingereza ilisema "raia zaidi wa Uingereza" waliweza kuvuka hadi Misri kutoka Gaza, lakini haikutoa idadi, huku Marekani ikisema raia 74 wa Marekani wenye uraia wa nchi mbili waliondoka kupitia kivuko cha Rafah.
    • Wizaraya afya inayoendeshwa na Hamas huko Gaza imesema zaidi ya watu 9,000 wameuawa katika Ukanda wa Gaza tangu tarehe 7 Oktoba, wakati mzozo wa sasa ulipoanza baada ya Hamas kuanzisha mashambulizi yake mabaya dhidi ya Israel na kuua watu 1,400.Tangu wakati huo, Israel imeshambulia Gaza kwa mashambulizi ya anga kama inataka "kuangamiza Hamas"
    • Kundil a Lebanon Hezbollah pia lilisema lilitumia ndege mbili zisizo na rubani zilizojaa vilipuzi kushambulia eneo la jeshi la Israel katika eneo linalozozaniwa la Shebaa Farms/Mlima Dov kwenye mpaka wa Lebanon na Israel.

    Unaweza pia kusoma

  4. Karibu

    Karibu tena kwa matangazo yetu ya moja kwa moja hii leo Ijumaa tarehe tatu Novemba, 2023.

    Mzozo kati ya Israel na Hamas huko Gaza unaendelea na ulichukua sura mpya siku ya Alhamisi wakati jeshi la Israel lilipotangaza kuwa "limekamilisha kuzingira Gaza", mji mkuu wa eneo la Palestina na ngome ya Hamas. Jeshi linasema linajihusisha na mapambano ya karibu na Hamas.

    Shirika la Umoja wa Mataifa linalowasaidia Wapalestina linasema watu 20 waliuawa wakati shule ya Umoja wa Mataifa iliyokuwa inawahifadhi watu waliokimbia makazi yao katika kambi ya wakimbizi ya Jabaliya karibu na Gaza City kuharibiwa kwenye mashambulizi makubwa ya mabomu. Vifo vingine vitatu pia viliripotiwa wakati makazi mengine matatu yaliposhambuliwa

    Endelea kuwa nasi tunapokuletea Habari za matukio hayo na uchambuzi zaidi.